ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Chanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia
Twitter: @gajetek
Twitter: @gajetek
Baina ya miaka kumi na kumi na tano nyuma simu nzuri ilikuwa ni ile isiyojaa kwenye kiganja, yaani ndogo mno. Ukiwa na simu kubwa kidogo unaambiwa una kitofali. Sasa mambo yanabadilika kwa kasi, HTC miaka ya 2005 walitoa Touch ikiwa na skrini yenye inchi 2.5" , Blackberry nayo wakati huo ikijulikana kama RIM walitoa simu ya ukubwa kama huo tofauti yake ikiwa na kibodi na upana mkubwa, zote zlikonga nyoyo za watuamiaji ewake wakati huo. Mafanikio ya mauzo ya HTC Touch ikaifanya kampuni ya HTC kutoa simu yenye zenye ukubwa wa 5", ikiwemo simu ya HTC Advantage na Advantage X. Hata hivyo simu hizi hazikupata umaarufu mkubwa kwani waliotumia simu hizi ni wachache waliopenda teknolojia kupita kiasi wakati huo.
Mwaka 2007 iPhone ikatoka ikiwa na skrini yenye ukubwa wa 3.5", watengeneza simu wote wakaanza kutoa simu zenye ukuwa unaokaribiana na huo. Hadi kufikia 2010 kampuni mbali mbali kama vile Motorola, Samsung, HTC na LG wakaanza kutoa simu zenye skrini za ukubwa wa 3.7", 4" na 4.2", simu kama vile Galaxy S ya mwanzo, Motorola MT710 Zhilling, Sony Erricson Xperia X10, Nokia E7 na HTC HD2.
Viroja vimeanza 2012 na 2013 ambapo watengeneza simu wanaokena kuchanganyikiwa juu ya mpaka baina ya ukubwa wa simu na tablet, hadi sasa hakuna mpaka baina ya ukubwa wa simu na tableti. Miaka miwili mitatu nyuma kulikuwa na tablet za ukubwa wa 6", lakini mwaka huu Asus wametoa simu walioiita FonePad ambapo jina la simu hiyo linadhihirisha kuchanganyikiwa tunakokuzungumzia, Simu hiyo ina ukubwa wa 7". Sisi katika Gajetek tukadhani simu hii itaweka rekodi ya kuwa simu kubwa kuliko zote ulimwenguni kwa mwaka 2013, sasa hivi Samsung wameomba usajili na kupasishwa kwa kifaa chenye chip za simu ambacho kina ukubwa wa 8", inaaminika kifaa hichi kitakuwa ni simu badala ya tableti ya 3G/4G. LG na Huawei nao wametoa simu zenye ukubwa wa 6".
Hoja ya msingi tunalilozungumzia ni kwamba mpaka sasa hakuna mpaka baina ya vitu viwili hivi kwenye zuala la ukubwa na udogo, lakini kivutio kikubwa kinachopelekea watengeza simu na tableti kuvutika kutengezeza bidhaa kubwa zaidi na zaidi kila siku ni kwamba; watu sasa hawajali kubeba tableti zao kila mahala, na hasa kwa vile ukubwa wa skrini unatoa nafasi ya mtumiaji kusoma vitabu na kutumia intaneti kwa ufanisi zaidi. Je simu zitatoweka na kuwa na kifaa kimoja tu ambacho kama wadau katika gajeti na teknolojia wanavyokiita kifaa hicho Phablet? Yaani "phone tablet".
Ni vigumu kutabiri wapi tunakwenda, kwani ukisogea juu kidogo sasa hivi tablet nazo zinaingiliana na laptop. Kuna laptop zenye ukubwa wa 10.1" na kuna tablet zenye ukubwa wa 11". Ukisogea juu tena unakutana na Lenovo Ideacentre yenye ukubwa wa inchi 27 kama Pc lakini inabadilika na kuwa tableti unapoitoa stendi, kompyuta hiyo ina betri hivyo inaweza kutumia bila ya umeme. Ukweli ni kwamba watengeneza vifaa hawatambui mipaka ya vifaa hivi na upo uwezekano wa tablet kupelekea kutoweka kwa ama simu au laptop kama daynasoo walivyotoweka ulimwenguni.