Kwa maana nyingine kama kuna ufisadi umefanyika basi wabunge wanyamaze kimya tu ili kuacha mchakato uliojaa ufisadi uendelee tu!!! Bunge letu linahitaji spika mpya ambaye atawapa uhuru Wabunge kujadili lolote lile bila ya kuleta udikteta kama afanyavyo dikteta Sitta.
[Date::2/11/2009
Spika azima hoja binafsi toka kwa Slaa, Mdee na Mohamed
Na Leon Bahati, Dodoma
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta jana alizima hoja tatu binafsi za wabunge wa upinzani bungeni, ikiwemo ya Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa (Chadema) kuhusu tuhuma dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, kuingilia mchakato wa zabuni ya uchapishaji wa vitambulisho vya taifa.
Hoja nyingine iliyopanguliwa ni ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF), aliyekuwa na pendekezo la kubadili katiba ili viwemo vifungu vya kumbana rais, kwa kuwa na ukomo wa idadi ya mawaziri kwenye serikali yake.
Akielezea juu ya kuizuia hoja ya Dk. Slaa, Spika alisema kamati imemshauri kuwa ni busara mchakato wa zabuni hiyo, kuendelea hadi mwisho ndipo iangaliwe uwezekano wa wazo la mbunge huyo wa Karatu kuzungumzwa.
"Kamati imenishauri kuwa ni busara mradi huo usichelewe, uachwe uendelee hadi mwisho, kama itaonekana kuna tatizo, kamati itarejea kuijadili (hoja ya Dk. Slaa)," alisema Sitta.
Kuhusu hoja ya Mohamed, alisema aliizima kwa sababu mabadiliko ya katiba, hayafanywi kwa mbunge kuwasilisha hoja binafsi.
Hoja nyingine iliyopanguliwa na Spika ni ile ya Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee (Chadema) juu ya mgogoro wa ardhi katika aneo la Boko-Chasimba, jijini Dar es Salaam .
Sitta alisema suala hilo haliwezi kujadiliwa bungeni, kwa sababu liko mahakamani.
Hata hivyo, Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF), alipinga maelezo ya spika nje ya bunge kwa maelezo kuwa ametangaza jambo ambalo Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ambayo ilijadili hoja ya Dk. Slaa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Khalifa alisema yeye ni mmoja wa wajumbe katika kamati hiyo na kwamba hawakujadili kuhusu kumshauri spika, asimamishe hoja ya Dk. Slaa hadi mchakato wa zabuni ya vitambulisho vya taifa ukamilike.
"Naona maneno hayo yalitokana na vikao vyao walivyofanya na kukubaliana hivyo na kamwe si wazo la kamati," alisema Khalifa.
Khalifa alisema bado walikuwa wanaendelea kuijadili hoja hiyo na kwamba ilikuwa haijafikia.