Je, Simba SC tunalo la kujifunza kutoka kwa Yanga SC?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Sio Kwa Ubaya, Nikiri Wazi Mimi ni Shabiki Kindakindaki wa Simba Sc. Naipenda Hii Timu mnoo. Ila Katika mpira au Biashara yoyote ya Ushindani Ni Vizuri kujifunza Mpinzani wako wa Karibu yeye anafanye ili uweze kufika Mbali.

Timu Za Simba Na Yanga Zote zilifanya Usajiri kwa Muda unao fanana na Vikosi vyote viliungana kwa Muda Unaofanana. Lakini niwe Muwazi, Kuanzia Ngao Ya Jamii, Usajiri walio ufanya Yanga Sc Wachezaji wake Wameonekana Kuingia Haraka Kwenye Mfumo wa Timu kuliko Usajiri wa Simba ambao Hadi sasa bado wachezaji wapya na walio kuwepo wanajitafuta katika Mfumo.

Sio Vibaya Sisi Kama Simba Tukajifunza Kwanini Wachezaji wapya Walio Sajiriwa Yanga Sc Wamewahi sanaa kuingia Kwenye Mfumo wa Timu kuliko wachezaji Wa Simba? Changamoto ni nini?

Angalia Namna ambavyo Pacome, Yao, Max, Skudu, Konkon nk walivyo wahi kuingia Kwenye kuliko akina Luis, Onana, Kramo, Ngoma nk. Ni kama Kocha wetu wa Simba Bado anaomba Mechi Nyingi zaidi ili timu iweze kukaa sawa Wakati wapinzani wetu ni Kama Wamejitafuta na wamesha Jipata.

Ukiangalia Mechi 2 za Ligi alicho cheza Simba Sc na Mechi Moja Ya Ligi Aliyo Cheza Yanga, Ukiongeza Na Mecho moja Ya Kimataifa ni dhahiri utaona kwamba Timu ya Yanga Sc tayari ina muunganiko ambao Simba Wanategemea Kuja kuupata, Changamoto ni nini? Katika Mechi 2 za Simba Chama Amesha Chezeshwa Namba Karibia 3 tofauti na Moja Imeonesha Kuzaa Matunda Ile ya Kumuacha awe free bila Kuingiliwa na Saido. Onana, Luis bado kocha anajitafuta wakati Kramo Hajaingia hata Uwanjani Kabisa.

Simba Sc Tusione Aibu kujifunza Kwa Yanga, Ni hayo tuu.
 
987AC938-4258-424C-A095-304E07699159.jpeg
 
Simba ni Simba na Yanga ni Yanga, hata jezi zao zipo tofauti. Ni ujinga kuwaza ulivyo waza.

Ikiwa una mahaba na Yanga songa mbele na Yanga yako, tuachie Simba yetu.
Huyu ni simba tangu zamani na humu anajulikana labda wewe hujui .

Amesema ukweli sababu ana uchungu na team yake tutolee ushabiki wa kipumbavu hapa pokeeni ushauri hapo.
 
Sio Kwa Ubaya, Nikiri Wazi Mimi ni Shabiki Kindakindaki wa Simba Sc. Naipenda Hii Timu mnoo. Ila Katika mpira au Biashara yoyote ya Ushindani Ni Vizuri kujifunza Mpinzani wako wa Karibu yeye anafanye ili uweze kufika Mbali.
Hatuna la kujifunza toka kwa UTOPOLO, nyie UTOPOLO ndio mmekuwa mkijifunza toka kwetu toka kuanza kuvaa jezi, kuvaa viatu vya mpira, kumiliki basi la Club, kucheza Fainali CAF, Kucheza nusu fainali Club Bingwa, kumiliki uwanja wa Mazoezi wa kwetu, kuanzisha Matamasha ya siku ya simba day....huko kwenu Utopoloni wenye Akili ni wawili tu...
 
Sasa goli tano tu match moja unataka tutafute cha kujifunza kwa utopolo? Hizo ni tamaa za waziwazi 😅 focus na concentrate kwenye project yako mzee siku yanga akifa tatu bila utakuja kututaka tujifunze tena kwake 😂😂?
 
Kwani wanaocheza vizuri kuliko Simba wanataji gani mpaka sasa au ndo kumfunga KMC goli 5?... Na yule golikipa wa KMC sio bure kuna namna pale yani kuna goli 3 alizofungwa zinawalakini... Halafu Simba inayojitafuta (kwa mujibu wa mleta uzi), tayari wanayo Ngao ya Jamii hivi siku wakijipata itakuaje sasa?...
 
Back
Top Bottom