RALC255
New Member
- May 11, 2025
- 4
- 4
UKAMATAJI, KIZUIZI NA MIPAKA YA MAMLAKA: HAKI ZA MSINGI KATIKA SHERIA YA TANZANIA
Katika mazingira ya kawaida ya maisha ya kila siku, si jambo la ajabu kusikia mtu amekamatwa either barabarani, ofisini au hata nyumbani kwake mbele ya familia. Wapo waliowahi kushuhudia mtu akibebwa kimya kimya usiku wa manane, wengine mchana kweupe wakiwa kazini. Lakini mara nyingi, kinachokosekana si tukio lenyewe, bali uelewa sahihi wa kile kinachoendelea. Ndipo swali la msingi huibuka: Sheria inasemaje kuhusu ukamataji na kizuizi cha mtu?
Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kila mtu ana haki ya kuheshimiwa utu wake na kulindwa dhidi ya kizuizi kisicho halali. Hii ni haki ya msingi, si zawadi au hisani ya mamlaka.
Ni kwasababu hii ndio maana kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), Sura ya 20 ya Sheria za Tanzania, ukamataji lazima ufanywe kwa kuzingatia sheria ikiwemo askari kujitambulisha kwa jina, cheo, kitambulisho na kueleza kituo anachofanyia kazi kabla ya kukamata.
Mara Baada ya Kukamatwa: Nini Kinapaswa Kutokea? Sheria imeweka wazi kuwa mtu anayekamatwa anapaswa:

- Kuambiwa sababu ya kukamatwa kwake kwa lugha anayoielewa, bila kuchelewa.
- Kuchukuliwa maelezo ndani ya muda usiozidi masaa manne (4) tangu alipowasili kituoni;
- Kufikishwa mbele ya mahakama ndani ya saa ishirini na nne (24) tangu alipokamatwa, isipokuwa kama kuna sababu halali ya kisheria ya kuchelewesha hilo.
ZINGATIA: Endapo masharti haya hayatazingatiwa, kuna uwezekano wa ukamataji huo kuwa kinyume cha sheria.
Je, Kushikiliwa Kinyume cha Sheria Kuna Madhara? Jibu ni ndiyo. Ni kinyume na haki ya uhuru wa mtu, hivyo haipaswi mtu kukamatwa ama kushikiriwa tu pasipo sababu; pia sheria haitaki mtu ashikiliwe kwa muda usio halali. Kumzuia mtu bila msingi wa kisheria au kumfikisha mahakamani baada ya muda unaoruhusiwa kunaweza kuwa na madhara ya kisheria kwa waliohusika.
Katika mazingira fulani, mtu anaweza kufungua mashauri ya madai mahakamani dhidi ya aliyemkamata au kumzuia, hasa kama hatua hizo zilichukuliwa bila sababu halali. Madai haya yanaweza kujengwa kwa misingi mbalimbali ya kisheria, ikiwemo:

1. Malicious Prosecution (Kushtakiwa kwa Nia Ovu)
Hii hutokea pale mtu anaposhtakiwa pasipo sababu ya msingi, kwa nia ya kumdhalilisha au kumharibia sifa. Ili hoja hii ikubalike mahakamani, huwa inapaswa kuonyesha mambo kama:
- Kwamba mlalamikaji aliwahi kushtakiwa;
- Kwamba mashtaka hayo yalimalizika kwa faida yake (yaliyofutwa au alishinda);
- Kwamba hakukuwa na sababu halali ya kisheria kumshtaki;
- Kwamba aliyemshtaki alikusudia kumuumiza au kumharibia.
2. False Imprisonment (Kufungwa au Kuzuiwa Kinyume cha Sheria)
Hii hutokea pale mtu anapozuiliwa bila amri ya mahakama au bila msingi wa kisheria. Kwa mfano:
- Kushikiliwa kwa zaidi ya saa 24 bila kufikishwa mahakamani;
- Kukamatwa bila kuonyeshwa sababu au hati halali;
- Kuzuiwa bila kumruhusu kuwasiliana na wakili au ndugu.
Katika mazingira haya, mtu anaweza kudai kuwa haki yake ya msingi ya uhuru wa mwili (personal liberty) imekiukwa.
Changamoto za kiutendaji zinaweza kutokea mathalan kuchelewa kwa usafiri wa kumfikisha mtu mahakamani au upungufu wa watumishi. Lakini hata hivyo, haki za mtu anayekamatwa haziwezi kufutwa kwa sababu ya changamoto hizo. Ndiyo maana ni muhimu kwa raia kuelewa mipaka ya mamlaka ya vyombo vya dola, pamoja na haki zao wanapokumbana na hali kama hizo.
Kwa ujumla, ukamataji si tukio linalopaswa kufanywa kwa misingi ya hisia, chuki au makisio. Ni hatua ya kisheria inayopaswa kufuata taratibu maalumu, kwa heshima na kwa mujibu wa sheria.
Kwa ambaye amewahi kukamatwa au kushikiliwa kinyume na utaratibu, sheria bado ina nafasi ya kurekebisha madhara yaliyotokea kwa njia ya haki na kwa kuheshimu utu wa mtu.

TANBIHI MUHIMU:
Maelezo haya yametolewa kwa madhumuni ya kuelimisha umma kuhusu haki za kisheria na hayalengi kuwa ushauri wa kisheria wa moja kwa moja. Kwa ushauri mahsusi, inashauriwa kuwasiliana na wakili aliyesajiliwa kwa mujibu wa sheria.

IMEANDALIWA NA
Robik Attorneys & Legal Consultants (RALC)
Near Ubungo Plaza, Dar Es Salaam
🌐 www.ralc.co.tz | Instagram ralc255