Wana JF tufahamu kuwa uchaguzi mkuu unakaribia. Kama kawaida ya wagombea wetu, rushwa mbele ili wapate ubunge then maslahi ya wapiga kura wao nyuma. Serukamba, ninavyomfahamu, aliupata ubunge katika jimbo la kigoma mjini baada ya wananchi kumchoka aliyekuwa Mhe. Kaburu, wakaona bora wampe yeyote yule hata kama ni ganda la nazi. Sasa ganda la nazi ndio hilo tunaliona, badala ya kuupiga vita ufisadi na mafisadi, Serukamba, anauunga mkono, kuunga kwake mkono sio bure, ni maandalizi ya kutafuta fedha za kampeni. Kwani hapa TZ fedha hizo atazipata wapi kama si kwa hao mafisadi? Naona ndio sababu ya huyo jamaa kuwapiga vita akina Sitta na Dr. Mwakyembe. Niungane na Sevrine hapo juu, ni kwamba, Serukamba kamwe hatauona ubunge wa kuchaguliwa katika jimbo analilishikilia kwa sasa.