Je, serikali yetu inawajali watu wake kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, serikali yetu inawajali watu wake kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magobe T, Jun 20, 2009.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kuna watu wanaosema Serikali ya Tanzania inawajali watu wake. Lakini ukiangalia jinsi watu hao wanavyonyanyaswa na vyombo vya dola utasindwa kuamini maneno hayo. Mfano, watu wananyang’anywa ardhi na kupewa wawekezaji au kuamishwa kwa nguvu bila kufidiwa vizuri ipasavyo na bila kufikiria ni kwa kiasi gani watu hao watateseka.

  Pia inapotokea raia wa kawaida amekosa, sheria inachukua mkondo wake, wakati kama ni kigogo aliyevunja sheria mambo yake yanafanywa kwa uangalifu mkubwa. Hata ile ‘treatment’ yake inakuwa tofauti na watu wa kawaida. Mwananchi wa kawaida atanyanyaswa lakini kigogo ataheshimiwa.

  Wiki iliyopita Waziri wa Fedha aliwasilisha bajeti ya serikali Bungeni ya 2009/10 na moja ya vitu vilivyosemwa ni kuondoa msamaha wa kodi kwenye madhehebu ya dini na NGOs zinazosaidia maendeleo ya nchi. Hoja ilikuwa kwamba misamaha hiyo inatumiwa vibaya na kuliko itumike vibaya ‘heri kodi iondolewe ili huduma za jamii ziende chini na wananchi walie na kusaga meno.’ [Msisitizo ni wa kwangu]

  Baadaye, watu mbalimbali walitoa maoni yao kuhusu kuondolewa kwa msamaha huo na ambavyo nchi itakavyoathirika. Hatimaye, Serikali ikaamua kusitisha mpango huo na tafsiri ikaja ya kwamba Serikali ina usikivu, imesikia maoni ya watu wake na kuona umuhimu wa kubadili msimamo ili ubaki uleule wa zamani. Ila ilishauriwa kuwa wale wanaotumia msamaha wa kodi vibaya watashughulikiwa wao wenyewe kuliko kuadhibu taasisi zote kwa makosa ya walio wachache.

  Ni kweli Serikali imefanya vizuri kutofuta msamaha wa kodi kwa madhehebu ya dini na NGOs zinazosaidia maendeleo. Matokeo yake yangekuwa kuanguka kwa chama tawala kwenye uchaguzi ujao!

  Hivyo, naona hii ilikuwa mbinu tu ya kuwafanya watu waamini kuwa Serikali inasikia kilio cha watu wake kwa maana kama ingekuwa inatambua mchango unaoletwa na madhebu ya dini kila sehemu isingepeleka hoja hiyo Bungeni kabisa.

  Kama Serikali yetu ni makini na inasikiliza kilio cha watu wake, kweli haikuona kuwa kuondoa msamaha wa kodi kwa taasisi za dini na NGOs kutaongeza makali ya maisha ya wananchi wa kawaida na kudumaza maendeleo?

  Serikali imeshindwa kudhibiti uozo (ufisadi) Serikalini sasa inababaikababaika na kutaka kuonea wanyonge. Kama Serikali ingekuwa makini na inayowajibika vizuri, ingedhibiti mianya ya rushwa serikalini na kuwafanya watumishi wake wafanye kazi kwa juhudi na maarifa.

  Inawezekana kabisa Serikali ilipanga kuwa italeta hoja hiyo Bungeni ili iiondoe na baadaye na wasiofikiri vizuri (wanaoamini Serikali ni sikivu) wadhani Serikali imesikia kilio cha watu wake. Siyo kweli kabisa! Serikali ingekuwa inasikia kilio cha wananchi tunsingekuwa tunaona wananchi wananyanyasika hivyo kwa kunyang’anywa ardhi yao bila kufidiwa ipasavyo.

  Ipo siku Chama cha Mapinduzi kitaachia ngazi. Kwani nani alijua Malawi Congress Party (MCP) itashindwa siku moja chini ya Dr Kamuzu Banda aliyekuwa akiita na wafuasi wake na wananchi kwa ujumla ‘life President’? Kama MCP ilifika mahali ikashidnwa, hata CCM itafika mahali itashindwa tu! Waendelee kufanya madudu na wataona watakavyoanguka baadaye!
   
 2. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2009
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Magobe hoja yako imetulia na nakunukuu Hatimaye, Serikali ikaamua kusitisha mpango huo na tafsiri ikaja ya kwamba Serikali ina usikivu, imesikia maoni ya watu wake na kuona umuhimu wa kubadili msimamo ili ubaki uleule wa zamani...

  Hilo la wananchi kutopewa fidia ya kuridhisha linatokana na sheria mgandamizo. Kuna waumini wa serikali ambao hata miaka 10 baadaye bado wanasisitiza sheria ya ardhi Na. 4 ya 1999 ni sheria mpya na ya kisasa. Vipengele vinavyotumiwa kukadiria fidia na maana ya fidia katika sheria ile ni tatizo kubwa. Na hili linaeleweka kama ukitafakari kwamba mchakato wa kuandaa sheria ile ulijikita kipindi kile tukiwa bado na ukili wa siasa za ujamaa.
  Nakuunga mkono kwa hoja kwamba serikali haijali watu wake na inatumia vigezo vya sheria mbovu kama ile aliyotumia Mkulo kuondoa ushuru wa forodha katika mafuta, kama ile waliyotumia kina Mkapa kutoa misamaha ya kodi nk. Hata ukiangalia sheria za mwenendo wa kesi za jinai, zinakiuka misingi ya haki (natural justice), mahakama inaweza ikamfutia mtu mashtaka, lakini prosecutors/police wanaweza wakamkamata hata kabla hajatoka nje ya mahakama. Waweza kutafakari yaliyompata Liyumba. Bunge na mahakama zina jukumu kubwa la kuzipitia sheria na kuchambua zipi ambazo zinamsonga mwananchi.

  Mwisho ni Tanzania pekee duniani ambapo mtanzania anaweza kunyanyaswa nje ya nchi na serikali ikawa kimya. Majanga makubwa yaweza kutokea, viongozi wa serikali bado wanaendelea na mambo yao...afadhali Kikwete mwanzoni alikuwa akikimbilia kwenye kila ajali, mahospitali nk, siku hizi mhhhhhhhh
   
 3. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kweli?
  Wanasheria mnasemaje?
   
Loading...