Je, Serikali inahusika katika utekaji nyara na kupotea kwa raia kunakoendelea nchini?

Je serikali inahusika katika utekaji nyara na kupotea kwa raia kunakoendelea nchini?

  • Ndiyo

  • Hapana

  • Sijui

Results are only viewable after voting.

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,096
22,823
Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini ni vigumu kutoihusisha serikali na vitendo vya uvamizi, utekaji nyara na kupotea kwa raia nchini.

Matokeo ya kura hii yatatupa taswira ya hali hii iliyojaa utatanishi mkubwa na kuwatia woga raia wema wa taifa hili.

Hakuna haja ya kuandika mengi, piga kura yako kulingana na unavyoamini halafu kaa umbali wa mita mia mbili usubiri matokeo!

Update...

Nawashukuru sana wote walioweza kupiga kura zao na matokeo rasmi ndio haya...
Swali: Je serikali inahusika katika utekaji nyara na kupotea kwa raia kunakoendelea nchini?

1. Ndiyo: 81.5%
2. Hapana: 8.6%
3. Sijui: 9.9%

Sisi Jamii Forums tumemaliza kazi na sasa tuachane na kumponda nyoka mkia, hatutamdhuru. Ukitaka kumuua nyoka unamponda kichwa.
 
Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini ni vigumu kutoihusisha serikali na vitendo vya uvamizi, utekaji nyara na kupotea kwa raia nchini. Matokeo ya kura hii yatatupa taswira ya hali hii iliyojaa utatanishi mkubwa na kuwatia woga raia wema wa taifa hili. Hakuna haja ya kuandika mengi, piga kura yako kulingana na unavyoamini halafu kaa umbali wa mita mia mbili usubiri matokeo!
Ungeliongeza option ya inawezekana, maana kusema for sure si rahisi kuwa ndiyo/hapana.. preponderance, likelihood. Inawezekana na isiwezekane, hivyo weka option ya inawezekana (this will cater for both inawzekana/haiwezekama)
 
Chadema na mbowe ndio wanahusika ili kuichafua serikali
Kwa hiyo serikali hii imeafiki kuchafuliwa na Chadema na Mbowe? Bila shaka ukijiuliza hilo swali utapata jibu...
 
Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini ni vigumu kutoihusisha serikali na vitendo vya uvamizi, utekaji nyara na kupotea kwa raia nchini. Matokeo ya kura hii yatatupa taswira ya hali hii iliyojaa utatanishi mkubwa na kuwatia woga raia wema wa taifa hili. Hakuna haja ya kuandika mengi, piga kura yako kulingana na unavyoamini halafu kaa umbali wa mita mia mbili usubiri matokeo!
Weka poll sheet hapo juu watu wapige kura na inahesabu yenyewe.
 
Kura ya maoni nchi hii bado sana; matokeo yake hayawezi kuaminika kwa namna yoyote ile. Badala ya kuwa objective, watu wanasukumwa na ushabiki wa kipuuzi zaidi. Tatizo uelewa wa mambo ni wa kiwango duni kuliko mahali pengine popote duniani.
 
Kwa kutotaka kuchafuliwa, wahusika wangeshughulikiwa kwa nguvu na kuwa weka wazi hadharani ili wabaki wasafi na wajionyeshe uwezo wao wa kulinda RAIA.
 
Kwa utaalam uliopo wa uchunguzi ambao vyombo vya dola vinao; na kwa teknolojia ya mawasiliano iliyopo inayowezesha kupatikana kwa mawasiliano ya watu pamoja na kutambua maeneo waliopo muda wote wanapotumia huduma za simu na internet, HAKUNA kitu kinachoitwa "mtu kupotea"!
 
Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini ni vigumu kutoihusisha serikali na vitendo vya uvamizi, utekaji nyara na kupotea kwa raia nchini.

Matokeo ya kura hii yatatupa taswira ya hali hii iliyojaa utatanishi mkubwa na kuwatia woga raia wema wa taifa hili.

Hakuna haja ya kuandika mengi, piga kura yako kulingana na unavyoamini halafu kaa umbali wa mita mia mbili usubiri matokeo!

Hata mtoto wa chekechea anaelewa kinachoendelea.

TUNAISHI RWANDA YA KAGAME.

Msijiulize USHAURI huyu bwana anatoa wapi.
 
Kwa nini serikali imteke Roma, Roma hajawahi kuwa tishio kwa serikali na wala si tishio kwa serikali. Kwa nini wasimteke mtu kama Lissu ambaye ni tishio kwao waje kumteka Roma au Ben ?

Ni wazi huu utekaji lengo ni kuichafua serikali, ni vyema vyombo vya dola vikawa makini sana na hili suala, wahakikishe yoyote anayehusika apatikane kwa gharama yoyote. Narudia Roma hajawahi na si tishio kwa serikali, sidhani hata wakuu wa vyombo vya usalama hao wazee walikuwa wanajua kuna mtu anaitwa Roma.
 
Piga kura yako kama unaamini hivyo...
 
Back
Top Bottom