Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
Taasisi ya TWAWEZA ambayo hufanya tafiti kwa kukusanya maoni ya wananchi leo inazindua awamu ya tano ya Tathmini ya Uwezo ya kupima watoto wa miaka 7 hadi 16 ili kubaini uwezo wao katika kusoma na kufanya hesabu.
Ripoti yaonesha, ufaulu wa wanafunzi hutegemea hali ya kijamii na kiuchumi ya kaya anayotoka. Ripoti pia yaonesha kuna tofauti kubwa katika viwango ufaulu kimkoa, Rukwa imeshika mkia katika majaribio ya Kiingereza na Hesabu huku Dar es Salaam na Arusha zikifanya vizuri sana.
Je hii inaashiria nini katika jamii yetu? Je sera ya Elimu Bure haina tija kama hali za Wananchi zisipoboreshwa?
Tunakaribisha maoni yako.
Baadhi ya Matokeo mengine ya Ripoti hiyo ni kama yafuatayo:-
1. Watoto ambao waliacha shule, 62% ni wavulana na 38% ni wasichana.
2. Kiwango cha elimu ya mama kina uhusiano na uwezo wa watoto kujifunza.
3. Lengo la 6 kimataifa la kutoa Elimu Bora kwa Wote halijafikiwa
4. 31% ya walimu hakuwepo shule siku ya tathmini ya Uwezo, kiwango cha juu cha utoro kilikuwa Singida (58%) na cha chini Ruvuma (17%)
5. Wanafunzi walikuwa na majibu tofauti walipoulizwa kuhusu uwepo wa walimu darasani
6. Uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu umeongezeka mara mbili zaidi ya ule wa mwaka 2013
7. Kuna upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo kwenye shule
8. Kumeendelea kutokuwa na uwiano sawa kwenye mikoa katika idadi ya walimu, vifaa na rasilimali za shule.