Je ratiba ya waajiriwa(wanawake) inawapa nafasi ya kutimiza majukumu yao ya ndoa? Je ratiba ipangiliwe vipi ili majukumu ya ndoa yatimizwe?

Je ratiba ya waajiriwa(wanawake) inawapa nafasi ya kutimiza majukumu yao ya ndoa? Je ratiba ipangiliwe vipi ili majukumu ya ndoa yatimizwe?

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,672
Reaction score
4,560
Amebarikiwa mwanamke anayerudi nyumbani kabla jua halijazama na kupika chakula Cha mumewe,hii ni Kulingana na kikao Cha wanaume.Lakini wanawake hao wamekuwa adimu sana zaidi ya almasi za mwadui.Zimekuwepo nyuzi nyingi zinazopinga wanaume kuoa wafanyakazi.Pia wengi wamejikita kuangalia ugumu wa kuishi na muajiriwa nawaalika tuangalie ratiba yao ya siku na tuone kama Kwa jinsi gani watatimiza wajibu wao wa ndoa.Kwenye jamii zetu suala la mume kupikiwa,kufuliwa nguo zake ,KUPEWA n

Fikiria una mke anafanya kazi Posta ,na mnaishi pembezoni tuseme Kimara au Tabata Kila siku ratiba itakuwa kama Kwenye masaa 24 ya siku atakuwa kazini masaa 9,atatumia masaa mawili Hadi matatu kwenda na kurudi,Akilala masaa 7 anabakiwa na masaa manne,Tuseme katika hayo naye anahitaji hata saa Moja kupumzika, Kwahiyo una masaa matatu tu Kila siku za katikati ya wiki kuwa naye katika urulivu wa kutosha.

1.Kuamka saa 11 asubuhi,yaani akili ishazoea hivyo Ili ajiandae na afike ofisini Kwa wakati.Hapa mechi za asubuhi zinakuwa hazina ubora maana akili inawaza asiharibu Kazini kwa HR.

2.Kurudi USIKU,Kwa Dar na foleni yake awe na usafiri au asiwe nao foleni Iko palepale, kurudi ni usiku guaranteed kabisa.Akiwahi saa tatu kasoro,atakupikia saa ngapi au atapika 'dada wa kazi'.Fahamu kwamba majukumu mengi ya nyumbani yatamalizwa na dada wa kazi (housegirl).


3.Ratiba na shughuli za Ofisi zinawafanya kuwaheshimu zaidi maboss kuliko mume,Hapa itategemea zaidi tabia ya mhusika lakini wafanyakazi wengi wanaogopa Sana kupoteza kibarua hii huwafanya kuwaheshimu mno na wakati mwingine kujipendekeza kwao.

4.Akiwa na mtoto au watoto hapo sasa vaa viatu vyake kuigawanya attention yake kazini Kwa mumewe na Kwa watoto yaani siyo rahisi.

Usishangae kuona kwanini wanawake wengi walioajiriwa ni single mothers,ratiba zao ni ngumu Sana zinahitaji uvumilivu wa hali ya juu.

6.Weekend hapa kidogo utampata,japo pia Kuna ratiba za saluni ,ibada na maandalizi ya wiki inayofuata.

TUPENI UZOEFU,Kwa wanawake mnawezaje kupangilia ratiba zenu hasa nyie corporate/government workers,Kwa wanaume je mshazoea hali hii au vipi?
Kwa maHR mliopo humu mnafanyaje kuweka ratiba nzuri inayowezesha ustawi wa ndoa?Maana kazi zingine zinalazimisha kuchagua kati ya ndoa na kazi

Karibuni.
 
Binafsi I just need an hour to make my day colourful to my partner.....

Sio lazima nishinde nae kutwaaaa

Sio lazima anipikie deileee.....anaweza kupika twice in a week, the cooking which makes great memory...

We have to learn to be adaptive with the situations
 
Ni vile tu maisha na ile kutaka 50 kwa 50 !

Mwanamke yafaa awe mama na mlezi wa familia,,,, ! Baba amka katafute ulishe familia yake !

Lakini kuna watu wake zao wanaingia night shift na wako fresh tu, usiku unaambiwa good night kumbe huku kuna mtu anaambiwa vp babe umechoka tupumzike,,,,, !

Life
 
Mbona rahisi sana kuishi na mke mfanyakazi. Kitu unatakiwa kufanya ni kuhakikisha mke wako ana wasaidizi na visaidizi. Maisha yanasonga
Wasaidizi na visaidizi unamaanisha nyumba ndogo mkuu?
 
Kimsingi ni mateso zaidi kwao.

Wakizaa ule msoto wanaopitia kupambana na wadada wa kazi namna ya kuwahandle watoto, utawaonea huruma. Unakuta kila wiki hakosi ED kazini kwake.
Ndiyo maana nimeuliza wanafanyaje siyo rahisi kabisa
 
Yn muajiri aangalie ratiba yako ya kuhudumia ndoa ili apange ratiba ya kazi 😂
Ufanisi wa kazi unaanza na kuweka mazingira rafiki ya wafanyakazi,Kuna kampuni Zina maeneo ya kulelea watoto wadogo.Kumpa nafasi mama kufanya kazi Kwa ufanisi
 
Binafsi I just need an hour to make my day colourful to my partner.....

Sio lazima nishinde nae kutwaaaa

Sio lazima anipikie deileee.....anaweza kupika twice in a week, the cooking which makes great memory...

We have to learn to be adaptive with the situations
Kaka,Kuna tofauti ya kula chakula Cha housegirl na mother house,Kwa ulivyoongea unapika wewe au unakula mgahawami
 
Ufanisi wa kazi unaanza na kuweka mazingira rafiki ya wafanyakazi,Kuna kampuni Zina maeneo ya kulelea watoto wadogo.Kumpa nafasi mama kufanya kazi Kwa ufanisi
Tatizo n kutaka kulazimisha mambo ya kizungu kuyafanya yawe ya kibongo, em nambie hapa Afrika kuna nchi yoyote ina kampuni yenye kufanya hvy? Ht huko mbele tuu n nchi chache mno zinafanya hvy
 
Back
Top Bottom