Je, Rais Samia alitaka CHADEMA Wahudhurie huku Uongozi wao Ukiwa Locked-Up Arusha?

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
"Yaani leo Umfunge Baba yangu Gerezani,kisha Kesho Nije kukupigia Makofi?"

Nimeshangaa kwa kumsikia Rais Samia akiwapiga vijembe Chadema, ikiwa pia ni ishara ya kuonyesha kukerwa kwake na hatua ya chama hicho kutokuwa sehemu ya washiriki wa mkutano huo.

Rais ameongea lakini hotuba yake imeacha maswali mengi kuliko majibu! Ameongelea kuhusu matusi kutoka kwa wanasiasa wa upinzani. Lakini pia anashindwa kutofautisha na kufafanua maana halisi ya matusi hayo ni yapi?

Je, kuongelea ufisadi uliokubuhu serikalini kwake ndio matusi? Au kushangaa mtoto wake Abdul kuonekana akifanya mazungumzo na Rais Museveni kuhusu masuala ya umeme wetu huko nchini Uganda.Ilhali yeye Abdul ni mtoto wa Samia na sio Afisa wa serikali ya JMT. Kwamba hayo ndio matusi kwa Samia?

Je! Wapinzani kuhoji na kuuchambua mkataba wa kifedhuli wa uuzwaji wa Bandari zetu kwa DP-WORLD ndio matusi hayo?

Au kuhoji kuhusu sababu za serikali kukataa taasisi kubwa za kimataifa na kitaifa kama vile Bunge la Ulaya na Chadema kutoingia Ngorongoro ili kujua kiini cha mgogoro wa jamii ya wamasai au kuongea na wananchi ndio Matusi kwake?

Rais anaongea kwa kuzunguka mbuyu,anaongea bila aibu.Badala ya kujiuliza ni nini kiini cha haya yoote kama sio hila mbovu na ufisadi unaofanywa na serikali ya Chama chake CCM.

Hivi mama anawachukuliaje watanzania?

Anaongea Kuhusu maadili wakati wavunja maadili na wavunja katiba ni wao CCM na serikali yake hasa hasa kupitia Jeshi la Polisi.

Wanakamata watu kihuni kama watekaji nyara na kuwaficha sehemu za siri kama magaidi,kinyume na PGO inavyoelekeza.

Tulitarajia kumsikia Rais kutoa kauli akiwakemea Polisi hao kwa ukiukwaji mkubwa wa maadili ya kiutendaji badala ya kuzunguka mbuyu.

Imetosha!

IMG-20230203-WA0002.jpg
 
"Yaani leo Umfunge Baba yangu Gerezani,kisha Kesho Nije kukupigia Makofi?"
Nimeshangaa kwa kumsikia Rais Samia akiwapiga vijembe Chadema,ikiwa pia ni ishara ya kuonyesha kukerwa kwake na hatua ya chama hicho kutokuwa sehemu ya washiriki wa mkutano huo...
Kwa CCM matusi ni kama:
1. Kudai katiba mpya
2. Kukataa ardhi yetu kuporwa
3. Kukataa kubambikiwa kesi
4. Kukataa kutekwa
5. Kukataa kikokotoo
6. Kukataa mauaji au kupigwa risasi
7. Kukataa kuporwa berue de change
9. Kukataa kuporwa kwa fedha za umma na ccm
10. Kutaka huduma nzuri za kijamii
11. Kukataa kuporwa uchaguzi
Endelea
 
Anajifunzia shabaha sehemu isiyo mbali sana.Angelenga kichwani.
Tafsiri ni kwamba Serikali inajipiga risasi kidole gumba mkono wake wa kulia,jambo ambalo litafanya mguu huo kutofanya kazi kwa maana kwamba serikali inajikwamisha yenyewe na hivyo Samia asitafute mchawi ilhali mchawi wake ni DP-WORLD na ubadhirifu TAMISEMI.
 
Back
Top Bottom