Je, Rais Magufuli hakuwa na ujumbe wowote wa mwaka mpya kulihutubia taifa?

Hotuba za kuandikiwa hapendi kuzitumia,labda awe ameandika mwenyewe!
 
02777b85341d690dc30f81b5de82cb32.jpg
Alieandaa hii picha amemkejeli Rais pakubwa sana...
 
Mkuu hivi unataka usikie nini kutoka kwa Mh?
Mkuu swali lako ni zuri sana.
Unajua inatiaga moyo sana wakati kiongozi analipa taifa MATUMAINI.
Hasa ukiangalia kuwa watu wanalia,
Mara UCHUMI ni mbaya
Mara AJIRA hakuna,
Mara freeze ya PROMOTIONS,
Mara MIKOPO.
Mambo kama haya ni CHANGAMOTO zinazohitaji JIBU na suluhisho na TUMAINI Kisiasa na Kiutawala.
Kama viongozi wote duniani including Papa Francis ametoa na kuwapa matumaini waumini wake sembuse na sisi?
Hii hutolewa kabla ya mwaka haujaingia.
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Aliyokuwa nayo alishahutubia, kuyarudia anajua anaamsha hisia hasi kwa watu, kumbuka kuna wale waliokataa hadi sauti yake isiigizwe!
 
mhh Wanyama wengi kwenye picha moja
Mkuu nmecheka sana, unajua ukiwauliza thematically walioyengeneza hii kadi wanataka kufikisha ujumbe gani sijui kama wanajua, la muhimu wao wamewajibu wale jamaa wa jirani waliotaka kuiba mlima wetu hahaaaa...hapa kazi tu
 
Mazoea yana shida, nihatari na aibu kuwa na akili isiyojitegemea, Marais wa Mataifa mengine wakihutubia juu mwaka mpya kumbe lazima JPM naye afanye hivyo? Poor thinking capacity, kwa hakika huu ni Udumavu wa kufikiri, Rais ni hivi karibuni tu alitoa ufafanuzi juu ya yote aliyoyaongelea mleta post, kwa vile alizoeshwa kuhutubiwa kila mwezi, akili yake ilishakariri kusikia hotuba za marais. Mleta post chapa kazi kwa ufanisi hapo ndipo utarekebisha maisha yako. Acha kukariri.
 
All in the wheel of life, nothing exist, yu elect the hyena to take care for a goat, and when goat consumed u wonder why?
 
Wanajamvi wa JF,

Wakati Marais wa Africa Mashariki leo WAMEHUTUBIA wananchi wao kupitia Radio na Televisheni wakigusia mafanikio na changamoto na nini wanataka kutimiza mwaka wa 2017.

Mimi sijamsikia rais Magufuli akiongea nasi leo sijui ni kwa nini.
RWANDA:
Rais Kagame aliongea kuhusu mafanikio yake akiwaambia VIONGOZI kuwa WANANCHI wana HAKI ya kuuliza MASWALI na KUPEWA MAJIBU ipasavyo pasipo KUSUMBULIWA ili wewe kiongozi uwasaidie.

Wananchi ni HAKI yao kupata HUDUMA BORA na hilo wewe kama kiongozi ni lazima UWAJIBIKE.

UGANDA:
Rais Museveni alianza kwa kutoa RAMBIRAMBI kwa wananchi wote wa Uganda waliofiwa na wapendwa wao mwaka uliopita wa 2016.

Akizungumzia nini atafanya mwaka huu wa 2017 alisema nchi inachangamoto ya maji safi.Na mwaka huu ataweka Water schemes/Maji MABWAWA/ VISIMA katika sehemu100 alizozitaja zitakazotoondoa TATIZO la maji safi nchini mwake.

Aligusia kufufuliwa kwa shirika la ndege na kuhakikisha maisha ya wananchi yana BOREKA zaidi. Aligusia Uchumi, Mafuta na KUSHUSHA gharama za UMEME nk.
KENYA:
Rais Kenyatta aliwashukuru wananchi na kuwatakia mwaka mpya wa baraka. Huku akiwaambia WAPINZANI, "Tufanye kazi pamoja bila kugonganisha wananchi.CHAGUZI huja na kwenda taifa hubaki"

Aliwaambia kwa kuwa ni mwaka wa uchaguzi watu waombe kura kwa amani bila mivurugano.
Kuhusu UFISADI aliwaambia wananchi "Mtaanza kuona watu WAKIFUNGWA" hasa kwa sababu JAJI MKUU mpya ana ARI na NIA ya kupambana na UFISADI.

TANZANIA:
2017 Rais Magufuli HAKUTUHUTUBIA ili tumsililize kama TAIFA ili KUTUPATIA mwelekeo wa mwaka 2017.

Hata jamani kutuambia TUFANYE nini ama serikali inafanya nini ili kuzikabili changamoto tulizonazo kama taifa na KUTUPA MATUMAINI tunapoingia mwaka 2017?
Ni nini kinaendelea ama it is NOT that important?
Acha kukariri.... Acha maisha ya kuiga....Ishi maisha yako.... akili za yule na yule changanya na zako.. ndio ufanye maamuzi... usifanye kwa kutumia akili zao...
 
Kwa namna hii ya majungu, sidhani kama kuna siku watanzania tutaamka na kutegemea akili zetu. Kuhutubia kuna umuhimu gani katika siku hiyo?
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom