Je, Rais Magufuli Atagombea Urais 2020? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Rais Magufuli Atagombea Urais 2020?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanahabari Huru, Oct 7, 2017.

 1. Mwanahabari Huru

  Mwanahabari Huru JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2017
  Joined: Mar 9, 2015
  Messages: 12,722
  Likes Received: 22,035
  Trophy Points: 280
  JE, MAGUFULI ATAGOMBEA URAIS 2020?

  Mtawala anayevunja #Haki na kuleta mdororo wa #Uchumi hawezi kushinda Uchaguzi 2020.
  -----------------------------------
  Ni dhahiri kwamba Rais Magufuli hawezi kushinda Uchaguzi wa 2020 kama atagombea na kama ataendelea na sera zake za ukandamizaji wa haki na kutokuwa na umakini katika sera za kiuchumi, biashara na kodi. Atashindwa uchaguzi 2020! Atashindwa! Na ameshashindwa!

  "JPM, Kama atagombea tena Urais mwaka 2020, hawezi kushinda kwenye uchaguzi ulio huru, haki na uwazi. Mhariri wa gazeti lililofungiwa hivi karibuni la Raia Mwema alipata pia kutanabaisha kwenye safu yake, kwamba uchaguzi wa mwaka 2020 utaamuliwa na ajenda mbili kuu za msingi, HAKI na UCHUMI" .

  Kwa nini #Haki na #Uchumi ni mtihani kwa Magufuli?
  -----------------------------------
  Hapana shaka ya chembe kwamba utawala wa Magufuli unaongoza kwa kuvunja haki za watu kwa kiwango cha juu sana ambacho hatujawahi kukishuhudia huko nyuma katika nchi yetu.

  Vilio na machozi ya wanaovunjiwa nyumba bila fidia ilhali kukiwa na zuio la mahakama, watu wanaouwawa hovyo na wengine kuokotwa kwenye fukwe za bahari utadhani ni samaki waliokufa kwa kukosa hewa, watu wanaoshambuliwa hovyo kwa kutoa mawazo yao tu dhidi ya Serikali, watu wanaoswekwa ndani kwenye magereza bila makosa, tabia ya visasi dhidi ya watu mbalimbali na wakosoaji wa sera zake, na uvunjifu wa haki nyingine za Kikatiba kama uhuru wa mawazo, kauli zinazovunja nguvu watumishi/wafanyakazi juu ya nyongeza ya ujira na stahiki zao nyingine, uhuru wa kukusanyika, uhuru wa kufanya shughuli za siasa, haki ya kupata Katiba mpya na Haki za Wazanzibari kutokana na sintofahamu ya uchaguzi wa Mwaka 2015.

  Hayo pamoja na mambo mengine ni mifano michache tu inayoonesha ubinywaji wa haki kinyume kabisa na Katiba ya nchi yetu, Katiba ambayo Rais aliapa kuilinda.

  Je, ni wananchi wa namna gani wanaweza kumchagua Rais wa namna hiyo endapo atagombea tena mwaka 2020? Bila shaka hakuna! Unabii utatimia!

  #Uchumi wetu una hali gani na unakwenda wapi?
  -----------------------------
  Licha ya takwimu kuonyesha kasi ya ukuaji wa uchumi kuwa kubwa kwa kiwango cha 7%, si jambo la kuficha kwamba wachumi wanajua kuwa shughuli za uchumi zimedora na kutia mashaka na hicho kiwango cha wastani wa 7% ni maendeleo ya sera za awamu ya nne ambayo sasa yanaanza kukatika.

  Baadhi ya taarifa zinaonesha kuwa, tayari makadirio ya kasi ya ukuaji wa uchumi yameshushwa mpaka 6% mwaka 2017 na 5% mwaka 2018. Ikifika mwaka 2020 kasi ya ukuaji wa uchumi itakuwa karibu sawa na kasi ya ukuaji wa idadi ya watu (2%) na hapo ndio tutaona ongezeko la familia zinazolala bila kula, matumizi ya bidhaa kushuka na mdororo wa uchumi kushika kasi(Zitto Kabwe)

  Hivi sasa hali ya maisha imekuwa ngumu kwa wananchi, mauzo ya bidhaa za viwanda nje kwaajili ya fedha za kigeni yameshuka kwa zaidi ya nusu, malipo yetu nje yamekuwa na urari hasi kwa sababu ya #Maamuzi ya hovyo ya miradi mikubwa kama ndege na Reli (miradi muhimu iliyotekelezwa bila weledi wa maarifa ya uchumi wa dunia unavyoendeshwa).

  Sekta ya Kilimo imeshuka mpaka kiwango cha kabla ya Uhuru, kwani kasi ya ukuaji wa sekta ya Kilimo mwaka 2016 ilikuwa 1.6% tu. Wakulima wa Korosho hawajapewa pembejeo, hivyo uzalishaji wa zao linalotuingia mapato ya Kigeni zaidi nchini utashuka msimu huu wa mavuno, Tumbaku (zao la pili Kwa kuingiza Fedha za kigeni) tayari wakulima wanalia, mazao ya choroko na kunde bei imeshuka kwa zaidi ya 500%, Pamba uzalishaji umeshuka Kwa 63% kati ya mwaka 2015 na 2017 (miaka miwili ya Magufuli), na mauzo Nje ya dhahabu kuanza kushuka kwa sababu mbalimbali na hivyo kupelekea shilingi kushuka thamani na hivyo mfumuko wa bei kupanda kwa kasi.

  Kutokana na shughuli za Uchumi kudorora, Mapato ya Serikali kwa mwezi yameanza kushuka kufikia chini ya makusanyo aliyoacha Rais wa Awamu ya Nne.

  Je, mtu anayeangusha uchumi kwa kasi ya "jet" ya namna hiyo anawezaje kuchaguliwa tena na Watanzania kuwa Rais?

  Tatizo kubwa la utawala wa awamu ya tano ni kuamini kwamba maamuzi ya 'kibabe' yasiyozingatia haki, sera za kiuchumi, biashara na kodi yanaweza kulinusuru taifa hili, huko ni kukosa weledi katika mambo haya, ni kujifunga kitambaa cheusi usoni!

  Mtawala yeyote anayetumia ghiriba kwa kutaja kila mara kwamba yupo kwa ajili ya wanyonge ilhali wanyonge hao ndio wanaoendelea kuathirika kwa kasi ya ajabu, ni wa kumuogopa, ni kushindwa katika uchaguzi! Ninadhani sasa wanyonge hawa wanamuelewa kweli kweli!

  Nimetimiza wajibu.

  #TuendeleeKumwambiaUkweli

  #PrayforTunduLissu

  2017 October 7

  N:B Swali la Kizushi: "WATU WASIOJULIKANA NDIO WALE WATU WA NCHI JIRANI WALIOINGIA NA KWENDA DODOMA KWA KAZI MAALUM?"
   
 2. swissme

  swissme JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2017
  Joined: Aug 15, 2013
  Messages: 13,109
  Likes Received: 16,845
  Trophy Points: 280
  MDINI MKABILA MCHUKI NA ZAIDI NI MZADIKI


  Mungu shusha maono.


  Swissme
   
 3. s

  songera JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2017
  Joined: Dec 29, 2014
  Messages: 1,294
  Likes Received: 448
  Trophy Points: 180
  Atagombea na kushinda kwa kishindo
   
 4. mvuv

  mvuv JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2017
  Joined: Feb 12, 2013
  Messages: 1,605
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio kushindwa bali kushindwa na nani?
   
 5. L

  Lihove2017 JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2017
  Joined: Aug 10, 2017
  Messages: 431
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 180
  Anafanya hivi kwa sababu hana haja ya kugombea tena 2020."he has nothing to loose in 2020".Hapendi kupata kura za wafanyakazi wa Tanzania
   
 6. mvuv

  mvuv JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2017
  Joined: Feb 12, 2013
  Messages: 1,605
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Natamani kila mtanzania aweze kufaham kuwa kwa sasa miongon mwa watu wanaoweza kuimudu vizur nchi hii kiuongoz ni 'Zitto Zuber Kabwe'
   
 7. n

  niah JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2017
  Joined: Sep 26, 2015
  Messages: 3,856
  Likes Received: 4,213
  Trophy Points: 280
  Je, ni wananchi wa namna gani wanaweza kumchagua Rais wa namna hiyo endapo atagombea tena mwaka 2020? Bila shaka hakuna! Unabii utatimia!
  Nimeku quote pale ila ujue kushinda ni lazima sababu wapiga kura wengi si wafanya kazi, siyo wasomi, hawajui kama kuna upinzani, walishaaminishwa kuwa ukichagua upinzani unaleta vita kama vile vya Rwanda kama kimama kimoja cha CCM kilivyowatishia wana Bukoba Mjini baadaye upinzani ukashinda. Mikoa iliyonyuma kielimu na kimaendeleo lazima watachagua CCM na hata wasipoichagua, yatakuwa yale yale ya siku zote.
   
 8. c

  chinembe JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2017
  Joined: May 16, 2015
  Messages: 4,086
  Likes Received: 3,769
  Trophy Points: 280
  Wafanyabiashara na watumishi wa umma wasidanganyike,wamnyooshe kwa debe come 2020
   
 9. kipara kipya

  kipara kipya JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2017
  Joined: May 2, 2016
  Messages: 4,193
  Likes Received: 3,804
  Trophy Points: 280
  Unahisi hawa watu 2000 wa humu jf ndio watasababisha asishinde simuoni mpaka sasa wa kushindana nae!
   
 10. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2017
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,999
  Likes Received: 14,151
  Trophy Points: 280
  Natabiri Magufuli atavunja zaidi haki, kuangusha zaidi uchumi na kuiba kura kushinda uchaguzi.
   
 11. ndue

  ndue Member

  #11
  Oct 10, 2017
  Joined: Mar 22, 2016
  Messages: 17
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 5
  Hafai kuongoza tena 2020
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...