Je, Rais anaweza kuondoa kinga ya Rais?

Je, Rais anaweza kuondoa kinga ya Rais?

Hapana, Katiba ya Tanzania haimruhusu rais aliye madarakani kushitakiwa mahakamani. Ana kinga kamili (immunity) kwa mambo yote anayofanya akiwa rais.

Hata kama angependa mwenyewe kushitakiwa, bado kinga hiyo iko kikatiba haiwezi tu kuondolewa kwa ombi lake. Tofauti na Kenya, ambako kuna masharti ya rais kuondolewa kinga kwa taratibu maalum.
 
Kinga ya rais ikutoshitakiwa kiondolewa kwenye katiba, basi ataweza kushitakiwa. Ilifanyika Zambia. Rais Chiluba alifuta kinga ya rais kutoshitakiwa, na rais Kaunda akakamatwa.

Lkn na yeye pia marekebisho hayo ya katiba yalikuja yakamsulubu.
 
Katiba yetu mbovu mno kwa mujibu wa katiba yetu Rais ni kama Mungu mtu ndo maana Wanafanya wanachojiskia
 
Hayo yote yanawezekana kwa nchi zisizojua utawala wa kisheria
 
Je, Katiba yetu inaruhusu Rais aliyepo kupeleka mswada Bungeni na kuliomba Bunge kuondoa kinga ya Rais ya kutokushtakiwa ili Rais afikishwe Mahakamani kwa makosa yake na mwishowe kuhukumiwa?

Najua Rais anaweza kumwondolea ulinzi Rais, niliona Kenya, vipi kuhusu kushtakiwa?
HAWEZI, vivyo hivyo tume yake ya uchaguzi haiwezi kumtangaza mpinzani kuwa mshindi wa kiti cha urais.
 
Je, Katiba yetu inaruhusu Rais aliyepo kupeleka mswada Bungeni na kuliomba Bunge kuondoa kinga ya Rais ya kutokushtakiwa ili Rais afikishwe Mahakamani kwa makosa yake na mwishowe kuhukumiwa?

Najua Rais anaweza kumwondolea ulinzi Rais, niliona Kenya, vipi kuhusu kushtakiwa?
Hii ni ngumu kumeza! Ni sawa na kukata tawi la mti ulilosimamia. Unamkumbuka rais wa Zambia aliyemrithi Kaunda alitunga Sheria ya kumshtaki rais na akamshtaki kweli mwishoni Sheria Ile ilikuja kumfunga mwenyewe!
Kwa nchi zetu hizi za Africa ni ngumu mno na haitakaa itokee. Mwone Ruto anavyochukua tahadhari kwa Gachagua Tena amejawa hofu na uoga.
 
Back
Top Bottom