Je, Raila Odinga atakuja kusaidia kumpigia kampeni rafiki yake?

Je, Raila Odinga atakuja kusaidia kumpigia kampeni rafiki yake?

fmlyimo

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
331
Reaction score
210
View attachment 267625

Je, serikali ya Uhuru Kenyata imepokea vipi uteuzi wa JP?

Kuchaguliwa kwa John Magufuli kuwa Rais wa Tanzania, kutakuwa na impact kwenye uhusiano wa Tanzania na Kenya. Magufuli na Odinga ni marafiki wakubwa sana. Inasemekana urafiki ulianzia kwa wazazi wao. 2017 wakati wa uchaguzi nchini Kenya lazima Magufuli atatia mkono wake na balaa litaanzia hapo.

Kuna masuala kadhaa kama barabara ya Serengeti na kiwanda cha magadi kule ziwa Natron kwenye wale ndege ain ya korongo (Flamingo). Sijajua msimamo wa Pombe Magufuli kwenye masuala hayo. Pia lipo la kujenga ma hoteli kwenye hifadhi ya Serengeti.

Kama mtakumbuka Magufuli alipata kusema kwamba kama sheria ingeruhusu basi angemwachia Raila Odinga aongoze jimbo lake huku Tanzania.

Hiyo ilikuwa ni wakati wa kampeni za uchaguzi za Urais kule Kenya.

Wengi walilaani kitendo cha Magufuli kushiriki kampeni zile. Hoja ilikuwa kwamba ni makosa kwa WAZIRI wa nchi moja kwenda kushiriki ktk kampeni za kisiasa ktk nchi jirani.

Binafsi sijapata kusikia mwanasiasa mmoja akimsifia mwenzake kama alivyofanya Magufuli. Siyo jambo la kawaida pia kwa wanaume kumsifia mwanaume mwenzake kiasi kile.

Sasa najiuliza, Raila Odinga ana influence kiasi gani kwa John Magufuli?
 
Magufuli ni wa kwetu. Hayo ya Kenya hayatuhusu
 
Km urafiki ni wa kwao cc tunahitaji maendeleo katika nchi yetu na co hoja za urafiki
 
Back
Top Bottom