Je, Profesa Assad aongezewe ulinzi?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,496
Reaction score
272,168


Huyu mtu kiukweli anayajua madudu mengi mno ya nchi hii , na kwa jinsi ya maelezo ya kamati ya maadili ya bunge , kuna chuki kubwa sana iliyochanganyika na wivu wa kimasikini uliojaa ushamba mkubwa sana ndani yake dhidi ya Assad.

Nashauri kwenye kipindi hiki cha mpito Profesa huyu aongezewe ulinzi .

Wenye akili wamenielewa .
 
Acha tu wammiminie Richachi Mwana wa kulitafua Mwana wakulipata
 
Mimi ninachoweza kusema ni
Sifa za kuwa mbunge ziangaliwe.
Hakuna haja ya kutafuta mchawi ni nani.

Huwezi kuwa na bunge ambalo ili uwe mbunge eti sifa iwe ni kujua kusoma na kuandika alafu unaingia bungeni kuisimamia serikali.

Haya ni maigizo ambayo kama hayataisha, maendeleo tutaishia kuyaona kwenye tamthilia za kifilipino
 
Ulinzi uongezwe huko kwenye ujenzi wa SGR na Stigler HEPD tujue raslimali zinazotokana na eneo linalo husika na ujenzi ni kiasi gani na taifa linafaidika vipi nazo?. Mfano magogo ya miti itakayo katwa.

Yasemekana wachina waliojenga TAZARA baadhi yao ni matajiri wa kutisha huko china kwa utajiri walioutoa kwenye raslimali walizopata maeneo yale yaliyopitiwa na ujenzi.

Tuwe macho tusizalishe matajiri wengineWaturuki, Wabeligiji na Waarabu contractors.

Yuko jamaa mmoja alijenga nyumba yake hakuingia gharama za mchanga. Mchanga aliupata kwenye eneo la ujenzi alipochimba mashimo ya maji taka.

Tuone sasa magogo ya miti itakayo katwa selous yatasaidia vipi kupunguza gharama za ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme.

Yawezekana uranium iko jirani hapo yote hayo na mengineyo serikali inayojali watu wake iyaangalie..
 
Lakini viongozi wa bunge akiwemo Job Ndugai wana elimu nzuri tu .
 
Serikali inayojali haya uliyoyaandika ingethubutu kumtimua CAG anayeibua madudu ?
 

Ndo umeandika nini sasa
 
unashauri aongezewe ulinzinzi? kwa matishio gani aliyo nayo na unamshauri nani?ndugu/familia au serikali?
 



😏
 
Wewe mchawi ni kuiondoa CCM madarakani hata kwa bunduki!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…