Sikupenda kutamka chochote hapa kwenye hii thread lakini naona nikinyamaza stalala na amani leo. Najiuliza, hivi, kama jambazi likinivania leo humu ndani ya nyumba yangu, mimi nina ka silaha kangu, Sime tuu. Nimtishie kwa kelele kuwa nina sime nakukata au nimvizie huko huko gizani nimkate shingo yake afe??
Polisi, wamedokezwa kuwa hawa jamaa wana vya moto. Wamewaambia mikono juu, jamaa kaamsha. Hivyo tunataka polisi wakajifiche ili majambazi yakimbie ati kwa sababu askari polisi haruhusiwi kuua?? Hiyo bunduki aliichukua 'amare' kwenda kuionesha wahalifu kuwa polisi wanazo silaha??
Jamani, Hakuna polisi mwenye kiu ya kuua, njiani waliwapita watu wengi tu, wangewamaliza. Jambazi, hana roho ya utu, ameshavaa roho nyingine kabisa, haogopi kumwua mtu asiye na silaha acha polisi mwenye silaha. Kama akiisha kukamatwa, Polisi, msimpige wala kumwua. Lakini akiwa bado na silaha yake, msimwache. Alichokuwa amekusudia moyoni mwake kumtenda mwingine, kama kilikuwa chema, mpeni.
Wito, kila raia, ajitahidi kujitafutia chake mwenyewe kwa njia halali, wala si kuua wengine, ili nawe usiuawe. Big up sana Polisi. Fanyeni kazi yenu kwa weledi tu.
Mtu ambaye hajawahi kuvamiwa na majambazi, si rahisi kuyajua magumu yaliyo wapata wengine. Usiombe kupatwa na mkasa huo, haswa mbele ya familia yako weye mwanaume