Je, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar ina Sifa za Kuratibu Maafa ya Gongo la Mboto? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar ina Sifa za Kuratibu Maafa ya Gongo la Mboto?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Feb 18, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu wa mkoa bado ni yule yule, William Lukuvi

  MBAGALA
  Watu waliandikishwa kuzingatia upenzi wao wa vyama vya siasa
  Orodha ya wahanga ilikuwa na kasoro nyingi
  Tathmini ilikosewa kwa makusudi, aliyepoteza nyumba kalipwa fidia ya ufa
  Wahanga hewa waliingizwa kwenye orodha na wakalipwa pesa nyingi
  Hadi leo kuna wahanga ambao hawajalipwa
  Zoezi liliendeshwa kibabe na hakuna nafasi ya wananchi kukata rufaa


  KIPAWA
  Fidia isiyo sawa na thamani
  Majina bandia yaliingizwa kwenye orodha na kulipwa wa kwanza
  Ubabe kuliko maridhiano

  Kutokana na uzoefu huu, ni vigezo gani vinafanya ofisi hii chini ya kiongozi huyo huyo kupewa jukumu jingine kubwa kuliko hayo ambayo ilishindwa kutekeleza vema na haijawajibika hadi leo.

  Je, michango yetu kwa wahanga kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar iko salama? Itawafikia wahanga?
   
 2. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wangekuwa wanaangalia sifa na kujifunza kwenye makosa hata haya mabomu ya Gmboto yasingelipuka bana. Wacha wale tu
   
 3. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ndugu Gurudumu ungefanya la maana sana kama unganika majina hata moja tu la aliyepewa fidia bila kuwa na sifa stahiki. Pili ingekua ni busara kubwa sana kama ungetenda wema wa kumchukulia hatua uliyemuona anapewa stahiki isiyi yake (mwizi) kama kumripoti kwa vyombo vya habari unavyoviamini, polisi, wanaharakati wanaoshughulikia haki za binadamu na hata kwa waziri mkuu. Nasema hivyo maana watu wanalalamika tu badala ya kuweka mambo wazi. Sijaona mtu analalamikia waliokuwa wanaishi wenyewe lakini wanaenda kuleta ndugu zao sehemu nyingine na kuwaambia waseme walikua wapangaji, au aliyekua anasema alikua na wapangaji nane ilihali nyumba ina vyumba vinne. Hapa wa kulaumiwa ni sisi maana tunashuhudia alaufu hatusemi ila tunapiga kelele kisiasa tu.

  Cha muhimu katika hili maana tumeshajifunza ya mbagala ni kutoa ushauri stakihiki. Mfano mimi nimepeleka pendekezo kwa maandishi kuwa wakati wengine wanahudumia walioathirika wengine wapite msituni kutafuta walikimbilia msituni na vichanga vilivyozaliwa njiani, wengine wafanye kazi ya tathmini ya awalimaeneo yanayozunguka kikosi cha gongo la mboto kwa angalao umbali wa kilometa 10 kila upande wakianza na tathmini ya awali kwa utumia helcopta na kupiga picha ya karibu ili isaidia kubaini ukumbwa wa makazi yaliyoharibiwa na baadae wafanye wenye makazi husika wakiwepo. Mwisho zoeozi zima liongozwe na jeshi na zoezi la kugawa stahiki za walioathirika lifanywe na wanajeshi wa kujitolea wakisaidiwa na mashirika ya kujitolea kama msalaba mwekundu na makanisa ya ukweli na siyo watu wanaotafuta malipo au cha juu. Kwa aliyetoa mada ni kweli ofisi ya mkuu wa mkoa haiwezi kufanya zoezi hilo maana siyo watu wa kujitolea na kwa sababu hiyo hawana sifa.

  Mwisho natoa mwito kwa wana JF wenye nafasi, wanahabari, wanasiasa wote bila kujali chama, polisi, mashirika ya kujitolea na ya kutetea wanyonge; tusaidie sana kumonitor zoezi zima la kuwasaidia wailoathirika kuanzia walipo sasa mpaka watakapokuwa wanagawiwa stahiki ama fidia zao. Pili natoa mwito kwa wale wote wanaoweza kuwasaidia waathirika kisaikolojia kuwasaidia kuwapa ushauri wa kisaikolojia.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WANANCHI HATUKO SALAMA TENA NA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA
  KUONGEZEKA HIVYO SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
  YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI


  Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake. Jukumu la msingi halijazingatiwa; wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

  Hatutaki tena tume kwa hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

  Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

  Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

  Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????
   
 5. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu nashukuru sana kwa uchambuzi na ushauri. Hatimaye baadhi ya hoja zako umezijibu mwenywe na nakubali pia.

  Niongeze tu kwamba;
  1. Wahanga waliodhulumiwa stahili zao walihangaika sana kulalamika kwa mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ya temeke. Vyombo vya habari vilifanya kazi nzuri sana kutuhabarisha na kuwapa nafasi waathirika nafasi kujieleza

  2. Tv na radiozilifanya kazi kubwa kuwahoji wananchi na wengi tuliufahamu ukweli kwa njia hii

  3. Wahanga walilazimishwa kusaini kabla hawajajua check zao zimuandikwa kiasi gani. Matokeo yake nyumba ya 50mil ililipwa fidia Laki saba

  4. Nenda mbagala utakuta watu hadi leo hawajapata fidia kabisa au wamepata kidogo haikutosha kujenga au kukarabati nyumba husika
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sometimes huwa nashangaa... sasa mfumo uliowekwa ndio huo.. hivi tulitaka nani afanye?? na kama kila kitu wafanye wengine do we need the government??

  will there be any law and order??

  Nadhani ni better ku-volunteer kusaidia kuliko kila wakati ku-crash, nijuavyo mimi ofisi ya mkoa ikiwezeshwa inaweza

  tuwasaidie ofisi ya mkoa kwa taarifa na ushauri
   
 7. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kwamba huwa hatuna tabia ya kufanya evaluation na kujifunza kutokana na makosa
   
Loading...