nkhamilongo
Member
- Jan 3, 2014
- 11
- 0
Raisi hana kosa lkn watendaji wake ndo wanamaomrudisha nyuma
Tatizo ni uelewa mkielewa mtakaa kimya
Maadam Rais amewarudisha mizigo tafsiri nyepesi siyo mizigo kwake. wale waliokuwa wakitangazia umma kuwa mawaziri hao ni mizigo (Nape Mnauye na Abdulhaman Kinana) basi rais aangalie kwenye chama chake inawezekana wao (Nape na Kinana) ndiyo mizigo awatue mapema
Pia tukumbuke ni katika kipindi hiki tumeshuhudia yafuatayo pale IKULU
1. Kualikwa kwa TEJA RAY C
2. Kualikwa kwa MATEJA na kufanya sherehe pale IKULU
3. Kualikwa wanamziki wa BONGOFLAVA na BONGO MOVIE kula bata pale IKULU
4. FBI kuishikiria IKULU kwa siku 3 wakati wa ziara ya OBAMA
Hayo niliyoyaorodhesha hayajawahi kufanywa na Marais wa awamu zote 3 zilizopita isipokuwa kwa huyu wa awamu ya 4
Raisi hana kosa lkn watendaji wake ndo wanamaomrudisha nyuma
huo ni mtazamo wako. na hao wasomi unaoongelea ni kina nanini? au ni wivu tu unaokusumbua. acha wivu fanya kazi ulishe familia yako.Naitazama Ikulu kama Taasisi ya juu sana hapa nchini kwetu na ndivyo ukweli halisi ulivyo. Lipo tatizo kubwa katika Taasisi hii hasa katika awamu hii ya nne ya Urais wa Tanzania. Ikumbukwe kuwa hii ni Taasisi yenye wataalamu mbalimbali wanaofanya/wanaotakiwa kufanya kazi kwa kumsaidia na kumwongoza Rais kufanya jambo jema kwa mustkabali wa Taifa hili kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Tangu rais wa Awamu ya Nne aingie madarakani amefanya uteuzi wa Mawaziri (Baraza la Mawaziri) takribani mara kadhaa:- Mwaka 2005 (mara baada ya uchaguzi), 2008 (Kashfa ya Richmond), 2010 (mara baada ya Uchaguzi), 2012 ( kashfa ya Nishati na Madini, Mgogoro wa Wizara ya Afya), na sasa 2014 (Kashfa ya Operesheni Tokomeza) ( .ikiwa pana mwaka nimeruka au tukio halijakaa sawa I stand to corrected)
Katika mara zote baraza la Mawaziri halijawahi kutangazwa lile lililo/litakaloleta tija kwa watanzania kwa mwonekano (machoni pa wasomi wengi) hata utendaji achilia mbali gharama linazotumia. Kitu cha ajabu ambacho mara kadhaa nimekuwa najiuliza hivi ni kweli kuwa Rais anachagua Mawaziri peke yake? Jibu ni hapana. Anapochagua mawaziri lazima ashirikiane na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Lakini hao wawili hawatoshi bila kupata taarifa za Mawaziri wanaowapendekeza toka kwa Maafisa wa Ikulu kwa kuzingatia Dira, Maono, Vipaumbele katika Mipango Mkakati na Sera ambazo Ikulu inapaswa kuzisimamia kwa mustakabali wa nchi. Sasa, unajiuliza huwa wana-shauri nini?
Hivi pamoja na makosa yote yalifanyika huko nyuma, basi kwenye kuelekea mwisho wa awamu hii wameshindwa kabisa kufikiri vyema hata kuchagua Baraza la Mawaziri bora? Hivi inahitaji kuwa na Phd kujua kuwa kuwa Shukuru Kawambwa hafai kuwa kuwaWaziri kwani katika Wizara zote alizopitia hakuna aliyo-deliver? Kama haitoshi, ikiwa ameleta majanga kwenye Wizara ya Elimu, kuna sababu gani kuendelea kumbakiza mtu anayesababisha majanga zaidi? Ofisi yenyewe ya Ikulu katika nukuu ya leo wameweka "Human history becomes more and more a race between education and catastrophe."H. G. Wells (1866-1946). Sasa ninajiuliza Kawambwa wa nini? Hebu tafakari orodha ya Mawaziri ambao wanaoitwa ni mizigo; kama haitoshi mnaongezewa mawaziri majanga wengine yaani Mwigulu Nchemba na Juma Nkamia ( hata Jenister Mhagama wanaomfahamu wanasema ni bomu hilo). Wanavyochagua wanazingatia dira, dhima na Maono ya ofisis ya Rais kweli? Ndiyo maana nasema Ikulu lipo Tatizo. Kama mtasema hakuna tatizo basi Ikulu ni Tatizo kwa watanzania.
Mwaka 2010 wakati viongozi na wazee mablimbali (akiwemo Butiku, Warioba na Salim) walipokuwa wanalalamikia juu ya ombwe la uongozi, walifika mbali kidogo na kusema Washauri wa Rais hawamshauri vizuri, japo wengine tukajiuliza, kama rais anashauriwa vibaya kwanini apokee kila ushauri mbaya ikiwa mwenyewe haupendi? Je hajui kuwa hawa watu/washauri wanaweza kumdharau kwasababu kila mara wanampa ushauri mbovu naye anaukubali? (zingatia kauli ya Mwalimu Nyerere pale New Africa Hotel,akizungumzia sifa za Rais ajaye, 1995).
Nikifanya marejeo ya Baraza Jipya la Mawaziri lilitangazwa jana, ninafikiri hadi sasa kuwa lipo tatizo kwenye Taasisi ya Ikulu yetu nikilinganisha na maandishi juu ya Dira, Maono na Dhamira ya Ofisi ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, ni la kiuongozi au kiutendaji? Sijui, ila karibu kuchangia.
Tanzania ni nchi yangu sina pakwenda zaidi ya nchi yangu hii ninayoipenda sana, ndiyo sababu nimeandika haya.