Je! Nitakosea nikisema kuna tatizo IKULU?

Je! Nitakosea nikisema kuna tatizo IKULU?

Mkuu, utakuwa hujakosea ila hakikisha hupiti karibu a Rama.......
 
Naitazama Ikulu kama Taasisi ya juu sana hapa nchini kwetu na ndivyo ukweli halisi ulivyo. Lipo tatizo kubwa katika Taasisi hii hasa katika awamu hii ya nne ya Urais wa Tanzania. Ikumbukwe kuwa hii ni Taasisi yenye wataalamu mbalimbali wanaofanya/wanaotakiwa kufanya kazi kwa kumsaidia na kumwongoza Rais kufanya jambo jema kwa mustkabali wa Taifa hili kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo.

Tangu rais wa Awamu ya Nne aingie madarakani amefanya uteuzi wa Mawaziri (Baraza la Mawaziri) takribani mara kadhaa:- Mwaka 2005 (mara baada ya uchaguzi), 2008 (Kashfa ya Richmond), 2010 (mara baada ya Uchaguzi), 2012 ( kashfa ya Nishati na Madini, Mgogoro wa Wizara ya Afya), na sasa 2014 (Kashfa ya Operesheni Tokomeza) (…….ikiwa pana mwaka nimeruka au tukio halijakaa sawa I stand to corrected)

Katika mara zote baraza la Mawaziri halijawahi kutangazwa lile lililo/litakaloleta tija kwa watanzania kwa mwonekano (machoni pa wasomi wengi) hata utendaji achilia mbali gharama linazotumia. Kitu cha ajabu ambacho mara kadhaa nimekuwa najiuliza hivi ni kweli kuwa Rais anachagua Mawaziri peke yake? Jibu ni hapana. Anapochagua mawaziri lazima ashirikiane na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Lakini hao wawili hawatoshi bila kupata taarifa za Mawaziri wanaowapendekeza toka kwa Maafisa wa Ikulu kwa kuzingatia Dira, Maono, Vipaumbele katika Mipango Mkakati na Sera ambazo Ikulu inapaswa kuzisimamia kwa mustakabali wa nchi. Sasa, unajiuliza huwa wana-shauri nini?

Hivi pamoja na makosa yote yalifanyika huko nyuma, basi kwenye kuelekea mwisho wa awamu hii wameshindwa kabisa kufikiri vyema hata kuchagua Baraza la Mawaziri bora? Hivi inahitaji kuwa na Phd kujua kuwa kuwa Shukuru Kawambwa hafai kuwa kuwaWaziri kwani katika Wizara zote alizopitia hakuna aliyo-deliver? Kama haitoshi, ikiwa ameleta majanga kwenye Wizara ya Elimu, kuna sababu gani kuendelea kumbakiza mtu anayesababisha majanga zaidi? Ofisi yenyewe ya Ikulu katika nukuu ya leo wameweka "Human history becomes more and more a race between education and catastrophe."H. G. Wells (1866-1946). Sasa ninajiuliza Kawambwa wa nini? Hebu tafakari orodha ya Mawaziri ambao wanaoitwa ni mizigo; kama haitoshi mnaongezewa mawaziri majanga wengine yaani Mwigulu Nchemba na Juma Nkamia (…hata Jenister Mhagama wanaomfahamu wanasema ni bomu hilo). Wanavyochagua wanazingatia dira, dhima na Maono ya ofisis ya Rais kweli? Ndiyo maana nasema Ikulu lipo Tatizo. Kama mtasema hakuna tatizo basi Ikulu ni Tatizo kwa watanzania.

Mwaka 2010 wakati viongozi na wazee mablimbali (akiwemo Butiku, Warioba na Salim) walipokuwa wanalalamikia juu ya ombwe la uongozi, walifika mbali kidogo na kusema “Washauri wa Rais hawamshauri vizuri”, japo wengine tukajiuliza, kama rais anashauriwa vibaya kwanini apokee kila ushauri mbaya ikiwa mwenyewe haupendi? Je hajui kuwa hawa watu/washauri wanaweza kumdharau kwasababu kila mara wanampa ushauri mbovu naye anaukubali? (zingatia kauli ya Mwalimu Nyerere pale New Africa Hotel,akizungumzia sifa za Rais ajaye, 1995).

Nikifanya marejeo ya Baraza Jipya la Mawaziri lilitangazwa jana, ninafikiri hadi sasa kuwa lipo tatizo kwenye Taasisi ya Ikulu yetu nikilinganisha na maandishi juu ya Dira, Maono na Dhamira ya Ofisi ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, ni la kiuongozi au kiutendaji? Sijui, ila karibu kuchangia.

Tanzania ni nchi yangu sina pakwenda zaidi ya nchi yangu hii ninayoipenda sana, ndiyo sababu nimeandika haya.

Utawala wa awamu ya nne .lazima ufanyiwe utafiti baada ya kufika mwisho wake.haiwezikana kusema tuu.nchi imeendeshwa kama genge la kuuza nyanya.
 
Mi nalia mfumuko wa bei awamu hii, Mkapa alisema "mtanikumbuka ndugu wananchi"
 
Rais yupo kimyaa umeme TANESCO na EWURA wanajipandishia bei, hafikirii ukipandisha bei umeme kila kitu kitapaa juu.
 
Mnyamahodzo,

Sidhani kama utakuwa unakosea kusema kuna shida Ikulu.
Ni katika awamu hii ya Uongozi ambapo vioja vingi tumeviona na kiukweli katika historia ya Tanzania, ukiachilia kipindi kile cha Vita ya Uganda na miezi michache baada ya vita, tumekuwa katika wakati mgumu Kiuchumi, Kielimu, Kiafya,Miundo mbinu, Ukinzi na Usalama, Utawala bora n.k.

Sijui kama Raisi ana washauri wabaya au anapenda ushauri mbaya anaopewa, either way bado inamfanya aonekane kituko(no offence).

Ni Raisi huyu aliyeanza kwa mbwembwe nyingi za kutembelea kila Wizara(Kabla ya kuanza "kuzurura" huko nje ya nchi, akitoa mabilioni kwa kila mkoa "Mabilioni ya JK" lakini yaliishia wapi hayo?

Kuna thread inayomuongelea Mwigulu Lameck Nchemba, kuwa "anadai yeye alikuwa best student..." hata kama ni kweli, Uongozi ni zaidi ya Academic Performance. Kuna Uadikifu pia!

Binafsi sijafurahishwa/kutegemea uteuzi huo(Ofcourse si kila raia aridhike)..Na si kwa ajili ya chuki binafsi, au chama cha siasa alichotoka, ila Mzaha, Uchochezi, Kejeli na majibu mepesi ya KIJINGA ya Mwigulu mbele ya Bunge "tukufu" na hata nje ya Bunge yanam-disqualify. Sasa iwapo haya yanatokea na bado watu kama hawa wanapewa Wizara, basi kuna shida mahali. Labda Raisi hajui(kutokana na kuzurura kwake/kutotulia nyumbani/nchini mwake) au anajua lakini anafurahia/anapendezwa na haya (Kejeli, Uchochezi, Majibu mepesi.)
 
Last edited by a moderator:
Angemchagua nani mbona wote ni kopo na mwenzie mfuniko? nani kasalimika ccm? huu ni ukoo wa Panya wote wezi na wachumia Matumbo 2. Na wamepata madaraka kwa rushwa, Dawa Mtanzania Usirudie kosa 2015 ikatae ccm na mambo yake yote, Na huu utakuwa ndo uzalendo
 
nashukulu kwa hotuba yako nzuri inaonesha wewe ni mwananchi kweli. alichofanya mkuu ni kuwapa mafao ya vyeo maswahiba wake ila si viongozi wakuleta maendeleo. tukitaka mabadiliko tujitolee wenyewe kuwapiga chini hawa wakoloni na mfumo wao ndio pona yetu tukiwaacha watatutesa hata kutu vua nguo tuwe uchi maana hawana huruma na hawana utu kabisa. Tanzania tunajanga kubwa la kutawaliwa na hawa maccm with no future. pia kumbuka deni la taifa linaendelea kwakasi na wanataka kuwepo madarakani. hawa mm nawasubiri hapa njombe niwatawanye kabisa 2015
 
nyinyi mnakariri mambo migulu lamek nchemba anatatizo gani au mko kiupinzani tu,kuwakabili chadema ndo tatizo kwa taarifa wanatakiwa kulalamikiwa ni makatibu wa wizara siyo mawaziri,makatibu ndo wataalam(wasomi)hebu tulieni acheni Nchemba afanye kazi big up saaana Nchemba
Mwigulu hana integrity ndio maana wananchi wanakataa uteuzi wake ukweli atakuwa waziri wa Kikwete kwa sababu huyo sasa yupo under wananchis survailance atachekechwa chekechwa mapka Raisi ataona aibu sana
 
Nilitegemea mtu wa kwanza kutoka katika baraza la mawaziri angekuwa Waziri wa Elimu, kweli CCM na kiongozi wake hawana nia nzuri na nchi hii.
 
kipindi hiki kazi tutaiona,mpaka tuseme poooo.
na sisi watanzania tumeoza...
 
Nililiona tatizo ikulu miaka miingi iliyopita, sio sasa. Kibaya zaidi 'devide and rule' ndo imetufikisha hapa tulipo.

Kuna watu hapa hawakuelewi maana wimbo wao siku zote ni 'serkali ya jk ni sikivu'. Wengine watakuona mdini (kwa nini jk), wengine watakuona mpizani ( kwa nini ccm) wengine watakuona mkabila (kwa nini kasikazini)......

Ninachokiona shida na umaskini utatuunganisha kuwang'oa matajiri ccm na ikulu haitakuwa dhaifu tena. Umaskini na elimu duni havitakuwa tatizo tena maana tumeunganisha nguvu.
 
WABONGO HAWAPENDI KUAMBIWA UKWELI, MNYIKA NJIE MBUNGE PEKEE ALIYE WAHI KUTHUBUTU KUSEMA UKWELI WA MATATIZO YA NCHI HII BUNGENI. WENGINE WANABWABWAJA WAKIOGOPA! Lakini wanajua tatizo ni rais.
 
Mkuu, hapo new africa hotel, siyo. Ilikuwa kilimanjaro hotel kabla ya kuuzwa. Kwa mengine nakupa heko. Nadhani bwana mkubwa anajiandaa kwenda ughaibuni kupumzika baada ya kutuachia mizigo na kutuongezea rumbesa juu!!!
 
ukisema utaitwa m-cdm. Uksema utaitwa mdini, uksema watasema huna shukran (serikali hii hii imekusomesha). Haya watafanya pengne hadi watakapokosekana wenye uwezo wa kupaza sauti (uwezo wa kufkri na kuhoji utauwawa na elimu duni) ili waendelee kututawala milele.
 
Back
Top Bottom