Je, nini matokeo ya ndoa za namna hii?

Je, nini matokeo ya ndoa za namna hii?

KITAULO

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Posts
1,926
Reaction score
2,843
Wana Jf,

Ndoa ni jambo la Baraka sana..na vijana wengi waliofikia umri wa kuowa huwa wanatamani kuingia kwenye maisha ya ndoa….japokuwa huwa tunajiuliza maswali mengi mno …kuwa ni mwenza yupi atakaye fanya mambo yawe mepesi na kukuletea Furaha.

Lakini mahusiano mengi siku hizi yanakumwa na changamoto za vijana wengi kuingia kwenye ndoa tayari wakiwa na watoto au mmoja wapo akiwa na mtoto aliyempata kwenye mahusiano ya awali.Ambapo vijana hutumia usemi ali maharufu kuingia kwenye ndoa ukiwa na hali ifuatayo:

(0,0)-Wote mkiwa hamna watoto

(1,1)-Wote wawili mnawatoto

(1,0)-Mwanamke ana mototo mwanaume hana

(0,1)- Mwanamke hana motto, mwanaume ana mototo

(1,2)-Mwanaume ana watato 2 mwanamke 1

Hebu tupeane maoni …ili sisi ambao bado hatujaingia tujue pa kuanzia.Je ni sahihi kuingia kwenye ndoa mkiwa na watoto au mkiwa na moja ya hali zilizoelezewa hapo juu?
 
Kwenye suala la ndoa, kila mtu anapewa mtihani wake wa tofauti na wengine. Majibu ya mtu mwingine hayatakusaidia. Mi nikitaka kuoa nitaangalia tu ni nani moyo wangu umemdondokea. Hata akiwa na watoto tisa, i'm gonna marry the shit out of her!
 
Imagine mtu ana watoto 13 wanawake wanne,kaenda kumuoa mwanamke mwenye watoto 5,nayeye kamzalia mtoto mmoja.hana habari.mapenzi bana
 
Ndoa hata uingie kwa style gani mle ndani lazima ukutane na changamoto.No formula
 
Sawa kabisaaaaa...choice is your boss
 
W
Imagine mtu ana watoto 13 wanawake wanne,kaenda kumuoa mwanamke mwenye watoto 5,nayeye kamzalia mtoto mmoja.hana habari.mapenzi bana

Watu wanajua kupenda sana...yani watu tayari kuhamishia familia ya mtu mwingine nyumbani kwake..
 
Ndoa hata uingie kwa style gani mle ndani lazima ukutane na changamoto.No formula

🤣🤣🤣nimecheka kama mazuri vile, wengine wanaingilia mikono, wengine miguu, wengine vichwa, wengine mbavu, wengine mgongo,kila aina ya somersault na mbwembwe zake.
1582871140170.png

Andiko lako limenitafakarisha sana nikaona ni kweli.
Cha msingi kujua ni kwamba marriage is part of life, life poses challenges every now and then, sasa tegemea tambarare ukione cha moto!
 
🤣🤣🤣nimecheka kama mazuri vile, wengine wanaingilia mikono, wengine miguu, wengine vichwa, wengine mbavu, wengine mgongo,kila aina ya somersault na mbwembwe zake.View attachment 1371247
Andiko lako limenitafakarisha sana nikaona ni kweli.
Cha msingi kujua ni kwamba marriage is part of life, life poses challenges every now and then, sasa tegemea tambarare ukione cha moto!

😂😂😂😂😂😂😂 SAWA BOSS
 
Hiyo ni kama mechi ya marudiano, mnaingia dimbani ubao unasoma na ushindi utategemea ‘aggregate’ score.... sasa itategemea ‘bao’ la ugenini litambeba nani kati yenu.
 
Back
Top Bottom