Je ninaweza kunywa maziwa fresh baada ya kumeza dawa?

Jaluo_Nyeupe

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
2,697
1,962
Japo sijawahi kushauriwa na daktari kwamba dawa hii ukimeza usinywe maziwa, lakini nimelelewa nikiaminishwa hivyo kwamba dawa na maziwa fresh haviendani. Sababu kuu ni kupunguza nguvu ya dawa. Je wataalam mlioko huku mnanipa majibu gani juu ya imani hii?
 
Ni vizur zaidi,
meza dawa then, after or before two hours ndio unaweza tumia maziwa.

Ila kama una njaa sana na chakula ni maziwa tu. Unaweza kunywa kiasi kisha ukanywa tena baadae.
 
Japo sijawahi kushauriwa na daktari kwamba dawa hii ukimeza usinywe maziwa, lakini nimelelewa nikiaminishwa hivyo kwamba dawa na maziwa fresh haviendani. Sababu kuu ni kupunguza nguvu ya dawa. Je wataalam mlioko huku mnanipa majibu gani juu ya imani hii?
inategemeana dawa gani mfano ALU kwa jina la mtaani mseto ni vizuri unywe na maziwa ila kuna dawa hushauriwi fano doxycline au tetracycline
 
Dawa zimegawanyika katika makund mawili jinsi zinaviyeyuka(solubilities)..yaani kuna dawa zinazoyeyuka vizur kwenye fat(mafuta)hizi zinaitwa fat soluble drugs mfano ni ALU..

Kuna dawa pia haziyeyuki kwenye mafuta zenyewe huyeyuka vizuri kwenye maji tu na hizi zipo aina nyingi sana hivyo haushauriwi kutumia chakula chenye mafuta unapotumia dawa hizi kama maziwa..
Kuna baadh ya dawa hazitakiwi kutumiwa na maziwa kwa sababu ya interaction kati yake na maziwa mfano ni tetracycline kwani hufanya complex compound ambazo huzuiwa kufyonzwa kwa dawa mwilini..

N.B fata ushauri wa daktari au mfamasia
 
Back
Top Bottom