Je, ninadukuliwa na huyu mwanamke?

Je, ninadukuliwa na huyu mwanamke?

Narasa

Member
Joined
Aug 2, 2017
Posts
7
Reaction score
7
Wana jukwaa nawasalimu,

Kuna jambo nakabiliana nalo naombeni ushauri wenu nina mchumba wangu ila tumejaliwa mtoto mmoja hatujafunga ndoa bado.

Mwenzangu alipata nafasi ya kweda China masomoni kwa muda mfupi alivyorudi akaniletea simu IPhone, sasa tatizo lililonileta hapa toka aniletee hii simu imekua kama jini.

Mambo yangu yote ananifunulia hata nikitongoza tu msichana kesho yake hata niambia directly ila ntafikishiwa vijembe mpaka najishtukia michepuko yote na majina anaijua na yeye yuko mkoa tofauti, najihoji au ni hii zawadi au maana nasikiaga aina hii ya simu sio rahisi kufanyiwa mambo ya udukuzi.

Mwenye ujuzi zaidi anijuze
 
Yawezekana kuwa anaambiwa tu na hao unaowatongoza au watu wanaokujua na wanaona ukifanya hivyo, au unadukuliwa kweli

Ila ili kuwa na uhakika, fanya experiment, unaweza ukatumia simu aliyokununulia kufanya jambo ambalo ni obvious atakukasirikia,

kisha nunua au azima simu nyingine iwe ya kufanyia control test, yaani unarudia kufanya jambo lile alilokukasirikia kwenye simu nyingine

Ukiona simu ya 1 alijua, kisha simu ya 2 hakujua, basi ni conclusion kuwa simu ya 1 imedukuliwa
 
Ni kweli hiyo simu inadukuliwa. Njia rahisi ni kununua kasimu kako Kadogo pamoja na line. Huko ndo utawasiliana na hiyo michepuko yako.

KUMBUKA:

1. MUNGU HAPENDI

2. UKIMWI UNAUA

3. MICHEPUKA INA GHARAMA
 
Acha uhuni tulia kwenye mahusiano muuoane mlee mtoto
 
Back
Top Bottom