Je nimsubiri?

wa zion

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2013
Posts
223
Reaction score
486
Ilianza kama utani kutumiana message za kirafiki,kuchekeshana hadi leo ninavyoandika hivi.

Mwaka jana ilitokea nimetokea kumpenda mkaka ambaye tulikua marafiki na alikua ananishauri kwenye mambo mengi tofauti ya maana, urafiki uliendelea huku akionesha kuwa hana mahusiano yoyote yale hadi siku nlipogundua kuwa yupo kwenye mahusiano na mdada mwingine.

Baada ya kugundua na kumuuliza alisema nimvumilie ananipenda kwa dhati na mimi ndio mwanamke wa maisha yake,kwa kua nilimpenda nilivumilia yote aliniambia aliangukia mikononi mwa huyo dada mwingine baada ya kuumizwa na binti aliekua akimpenda kwa dhati nikaona sababu amekua wazi na kumpenda nampenda kumpoteza sitaki nikavumilia hadi pale maji yalipofika shingoni....

Pale ambapo yule dada alipoanza vitimbwi nikaona sio kesi nikamwambia kaka chagua moja kama ni mimi au huyo mwenzangu nikampa muda wa kukaa kutafakari yupi anaona kwake atamfaa kwenye maisha yake siwezi kuficha niliumia sana kutowasiliana naye kwa kipindi kile hadi siku atakayotoa maamuzi.

Siku ikafika kaka akasema nimeona bora kuwa na wewe na sasa tupo kwenye mahusiano halali nilifurahi sana nikaona sasa nimepata mtu wa kufa na kuzikana.

Kwa kufupisha sasa amesema hawezi kuwa na mimi kwa sasa maana hatafanikisha malengo yake kwa kua akiwa na mimi namdekeza,namfanya aone kama yupo likizo anaomba arudi kwa x wake akakamilishe mipango yake baada ya hapo turejeshe mahusiano yetu rasmi hadi sasa tunaonana,hatujaachana rasmi ingawa huyo dada hajui hiki kitu imekua siri kubwa kati yetu sisi.

Maumivu ninayopitia kumuona yupo na huyo dada mwingine ni makubwa na mazito nimejaribu kila njia labda atatoka kichwani nimeshindwa..nampenda kutoka moyoni sio siri.

Moyo unaniambia mvumilivu hula mbivu akili inaniambia niondoke Uran amefanya nifunguke hapa Bado najiuliza je nivumilie maana aliniambia hadi mwezi wa saba mambo yatakuwa sawa atarudi rasmi kwangu baada ya kupata anachokitaka huko Kwa kua nakijua anachokitaka naona kama ana point maana mimi sitamsaidia na sina uwezo wa kumsaidia hicho anachokitaka kwa huyo dada.

JE NIMSUBIRI?
 
Ebu tuambie kwanza anachotaka kwa huyo dada ni kitu gani!
Ndo tukushauri vizuri!
 
..Hapa kijijini kwetu kuna jamaa ana mke na watoto ila kwa sasa ''ameolewa" na mbibi wa kizungu na mkewe ameridhia hali hiyo kwasababu kama zakwako ulizozitoa hapo juu. Nilikua namshangaa sana yule Mama ila wewe umenifungua..
 
Tafuta njia kuu ,hyo ni service road....mtu kashasema hajielewi ,why u wanna sit there and wait??au waamini mambo ya tamthilia za kifilipino?km ilitokea ukampenda huyo u can love again..
Nisikuchoshe,MY POINT IS...usimuweke mtu a PRIORITY in ur life wakati he's not even considering u ryt now as an OPTION...
 
Yaani upo KIMARA unataka kwenda MANZESE umeona upitie GONGO LA MBOTO ili ufike haraka MANZESE,duh dunia ina mambo!.
 
Bila kukijua hicho kitu ni ngumu kujua pa kuanzia maana ndio msingi mkubwa wa stori na maumivu unayoyapata baada ya jamaa kuamua kurudi kwa huyo dada.

We vumilia tu maana haujaamua kuweka wazi,, kufa kizungu na tai shingono.
 
Tuwe pamoja basi hadi mda atakaorudi.jejejejejejejejejejeee


hivi kama hata rudi, mda wako, future yako utairekebishaje? Tengeneza future yako sasa na usisubiri mtu mwingine
 
Kaona hauna msaada kwake dats y amekutia kapuni huyo alokuwa mpenz wake wakwanza ndio anamalengo nae alikuja kwako kwa tamaa tu ya kufunua malinda binti shtuka unamsubir mwanaume? me nkajua unamsubir mungu mweee dunia ina mambo pole xana
 
Jamani, una umri gani mpendwa? Manake hicho ulichoandika bado nashangaa, yani ww na huyo msichana mwingine mnakubali kutumika kias hicho, alimchoka akaja kwako now amekuchoka amerud kwake loh, ni hv the minute ulipogundua yuko kweny mahusiano ulipaswa kufuta mawazo yoyote ya kimapenz ukiyokuwa umeanza kuyajenga kwake na ungebakiza urafiki tu tena wenye mipaka ili uwe safe, huyo mwanaume anaonekana hana msimamo si wamapenz wala wa maisha yake na kamwe usijekubali kuwa na mwanaume anaekwambia anataka kumuacha mpnz alienae kwa ajili yako kwani na ww mwisho wa cku utaachwa kwaajili ya mwingine
 
aisee dunia hii natamani ningekuwa na namba yako nikutumie audio 2 hici nadhan utaacha kupoteza muda sikiliza myn usione kwamba hakuna atakaeweza kukupenda dunia bado kubwa na kuna watu wanatamani huo upendo wa dhat huyo jamaa hakupendi na najua kinachokuumiza sio yeye kwanda kwa mwanamke mwingine bali WHY JAMAA HAKUPENDI kiu yako ni kupendwa then ondoka hapo hupendwi hapo honey!!
 
Mmmh!!!.. una moyo mgumu bidada kusubiria mtu yuko kwa mtu mwingine. Tafuta wa kwako
 
Duuuuh....
Kupanga ni kuchagua!!! Chagua lililo jema kwako kama anakupenda mwambie umechoka kuvumilia arudi kwako na muishi hvyo hvyo bila kupata hiko kitu maana inaonekana mwanaume yupo kifaida zaidi sasa we mkishazoeshana hayo mambo kuna siku mpo kwenye ndoa atakuambia sasa wife kuna jimama huko inabid aje kuish hapa na wewe uwe hausigel just kwa week na tutapata kitu kikubwa sana.......
 
Kweli mtu mnataka kujenga nae maisha ya ndoa anakwambia hivyo?
Je huu ndo msingi/mtaji wa maisha yenu ya mbele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…