Je nimeharibu gari kwa kuliendesha huku taa ya oil ikiwaka?

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
26,144
75,240
Habari wana jukwaa.
Gari yangu ni Corolla Runx Engine NZFE1 vvTi. Nimetoka kubadirisha oil (BP) kama 100km zilizopita.
Tokea siku ya Alhamis sijaliendesha hadi jana siku ya Jumanne.
Nilipoendesha kama kwa saa 1 hivi, go and stop kidogo, taa nyekundu ya oil kwenye dashboard ikawa inawaka na kuzima. Baadae ikawaka moja kwa moja. Nikapanic. Nikalizima gari, nikaliacha kama dakika 15, nikacheck oil level, iko vizuri. Nikawasha ile taa haikuwaka tena. Kwakua nilikua mbali na home nikaondoka. Baada ya kama dakika 10 issue ikajirudia. Nikafanya tena kuzima, kutulia dakika 15 kuwasha, taa haikuwaka tena. Ila baada ya dakika 10 hivi ikarudia. Nikajisogeza hadi nyumbani, nikapaki.
Asubuhi leo nikawasha ili nije kazini hafu nimuelekeze na fundi (alienibadirishia Oil), nikaondoka. Taa haijawaka. Ila baada ya dakika 15 ikaanza ule mchezo. Kwenye foreni nikizima hafu nikawasha gari, ile taa inapotezea kuwaka kama dakika 20 ila itajirudi.
TATIZO LIKAONGEZEKA.
Taa ya Check Engine nayo ikawaka. Mungu Wangu. Hapo ndio nikapanic. Ila nikajisogeza hadi kazini nimepak namngojea fundi.

Je, nimeharibu engine components nini jana nilipoendesha gari wakati oil light imewaka? Kwanini taa ya Oil imewaka wakati oil level iko vizuri? Msaada wakuu.

NB. Tokea taa ya oil iwake jana, jumla nimetembea kama KM 40 hivi hadi sasa.
 
Maana yangu ni kwamba oil pump kama haifanyi kazi oil hautazunguka kwenye engine ndio maana unaona taa nyekundu,kingine kama filter ni mbovu yaweza block oil kupita pia.ndio maana unashauriwa ukibadilisha oil mwambie fundi aliwashe kwa muda wa 5-10 minutes ujiridhishe na mzunguko wa oil kwenye injini yako.
 
Thanks.
Je, kuna uwezekano kwamba nimeua internal parts za engine? Nimesoma mtandaoni naona kitu nilichokifanya (kuendesha under low oil level or pressure) ni dumbest thing hatari.

Na hiyo Oil Pump kama imeharibika, it need to be repaired or replaced?

Thanks
 
Fundi atakufanyia uchunguzi na kukwambia ukweli wa tatizo,pengine waweza kuta ni short ya Umeme imesababisha taa kuwaka tu.
 
Ndugu yangu nataman kukulaumu ila naona nikae kimya maana sijajua kama una uzoefu gani na gari. Umefanya jambo baya sana na usije ukalirudia kabisa, nashangaa unavyosema gari ilifika nyumbani alafu we asubuhi ukaiamsha hivyohivyo ukijua unawasha taa ya oili?? Ikafikia wakati ikawasha check engine we ukaendelea kuendesha tu??? Usirudie jambo hilo tena siku nyingine , ni hatari kubwa kwa engine ya gari!!! Kwa kilichotokea lazima mfumo wa kusambaza oil una matatizo na lazima kutakuwa na adhari kwenye engine ndio maana taa ya check engine ikawaka, msubiri fundi atakupa maelekezo ila nakushaur kama hataona tatizo utafute break down uipeleke garage!!!
 
Hapo kwanza lazima ujue aina gani ya oil aliyokuwekea,pili aina ya Filter aliyokuwekea na tatu acheki hiyo oil pump.Kama ni oil zetu za kutunga hiyo inaweza kuwa tatizo,kama Filter aliyotumia ni sub standard nayo ni tatizo.Lastly anaweza kukuchekia sensors zinazopeleka taarifa kwenye dash board yako kama zinafanya kazi vizuri.Mimi nilishawahi kupata shida ya kuwakiwa na taa ya check engine,baada ya kufanya diagnosis kwa kutumia computerized engine check system ikagundulika ni Oxygen sensor imekufa ,nikatembea na gari kwa zaidi ya km 100,nikashauriwa nifanye replacement na baada ya kuibadilisha taa ilizima na ninapeta mpaka leo,
 
Mkuu mtoa mada anasema kwanza iliwaka taa ya oil then ikawaka ya checkengine hapo ndio napata waswas kama tatizo linaweza kuwa sensor ila pia mtoa mada atueleze kama kulikuwa na mabadiliko katika perfomance ya gari??? Shida ya mafund wetu unaweza mwambia tatizo kama hilo akawasha gari na kupiga resi tatizo likawa kubwa zaidi.
 
Mkuu J33 thanks kwa ushauri.
Najua nimefanya ujinga wa kulahumiwa sana. Ila mazingira yalikua mabaya ndio maana nikalazimika kuendelea.

Performance ya gari haikubadirika, ilikua kawaida Tu, I mean ata nikizima radio, sikusikia any weird car engine noise wala gari kua nzito.

Tokea last oil change and filter, nimetembea kama KM 100-150 hivi. Niliweka Oil ya BP.

Fundi bado hajaja ila nilitaka nifanye kwanza diagnosis kwa kutumia computer (bila kuondoa gari hapa) na fundi aje aangalie kwanza kama tatizo linatibika.

Ushauri zaidi? Thanks wadau.
 
Kwa oil ya BP uko sahihi,akishakuja fundi wako utatujuza kwa faida ya wengine ili waweze kuelimika.Kuna thread humu ilianzishwa na mshana jr ilikuwa nzuri sana ilihusisha matatizo ya aina mbalimbali kwa wenye magari.
 
Vipi fundi bado hajaja??
Hapo inaonekana kuwa kuna tatizo kwenye engine. Yaani umetengeneza tatizo jingine kwa kuendesha wakati taa nyekundu ya oil ikiwa imewaka.
 
Jamani mbona mnanitisha maana mimi naweza kutembea na gari inawaka na kuzima taa ya oil hata mwezi mzima.Pia kuna taa ya hand break huwa inawaka na nikimuuliza fundi anasema inatakiwa adjustment tu hivyo hata nikiendelea kutembea ikiwa inawaka haina tatizo.Kwa wazoefu hili limekaaje wakuu.
 
Vipi fundi bado hajaja??
Hapo inaonekana kuwa kuna tatizo kwenye engine. Yaani umetengeneza tatizo jingine kwa kuendesha wakati taa nyekundu ya oil ikiwa imewaka.
Mkui, bado hajaja. Nimeliacha tu. amepromise Tomorrow. Ila amesema possibly oil imegandiana au imejazana kwenye sump so atasafisha kesho. Also sijafanya comp diagnosis bado, jamaa mswahili.
 
Jamani mbona mnanitisha maana mimi naweza kutembea na gari inawaka na kuzima taa ya oil hata mwezi mzima.Pia kuna taa ya hand break huwa inawaka na nikimuuliza fundi anasema inatakiwa adjustment tu hivyo hata nikiendelea kutembea ikiwa inawaka haina tatizo.Kwa wazoefu hili limekaaje wakuu.

Mkuu kwa kawaida ukiwasha Gari huwa haitakiwi taa yoyote pale kwenye Dashboard iwe inawaka.
Ukiwasha Gari ikawaka taa zote kwenye Dashboard zinatakiwa zizime, ukiona Gari ipo silence au kwenye mwendo halafu taa ikawaka au inawaka na kuzima ujue kuna kasoro.
Taa ambazo zinaweza kuwaka hata Gari ikiwa silence na haziusiani na mambo Engine ni ya Seat belt, na ukifunga itazima, ya mlango Kama hujafunga vizuri nayo pia ukifunga mlango itazima, Overdrive Kama utakuwa ume switched off overdrive ujue taa itawaka, uki switched on taa itazima, na taa nyingine ni ya kukuonesha umewasha full, taa hizi nilizoorodhesha hapa haziusiani na mzunguko wa Engine, vinginevyo ukiona taa inawaka tofauti na hizo baada ya kuwasha Gari bila ya shaka ujue Gari yako itakuwa na kasoro.
Kiujumla haitakiwi taa yoyote iwake kwenye Dashboard Gari inapokuwa kwenye mwendo.
 
Nakushauri uanzie kwenye sensors, plugs na ignition coils. Gari yangu ilishanisumbuaga sana kwenye kuwaka taa ya check engine kumbe tatizo lilikuwa kwenye coil na sensors.
 
Back
Top Bottom