Je,nikweli waafrika tumetokana na manyani??

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
13,068
15,923
wakuu,nakumbuka kipindi nasoma hasa history vitabu viliandikwa jinsi mwanadamu hasa mwafrika alivyobadilika badilika mpaka kufikia kuwa kama hivi tulivyo,na mpaka sasa kuna documentary nyingi sana tu wanaonyesha ktk tv jinsi mwafrika alipokuwa nyani mpaka kuwa mwanadamu,juzijuzi hapa naangalia documentary moja ilikua inaonyesha kama hayo manyani(sisi) hapo nyuma tulikua tunaishi na wanyama na chakula chetu kilikua mifupa kabla hatujaweza kuwinda,yaani ilikuwa simba akiua mnyama akila akabakisha fisi nao wanakula kisha manyani hayo(sisi)tunawafukuza fisi tunakula masalia!,ni documentary nyingi zinaonyesha haya mambo,sasa je swali ambalo najiuliza ni kwamba je ni kweli sisi waafrika tulitokana na manyani?kivipi binadamu atoke kuwa nyani mpaka awe binadamu?na kama ingekuwa hivyo manyani si bado yapo si tungeendelea kuona jinsi nayo yanavyobadilika na kuwa binadamu?halafu sijui kama watoto bado mpaka sasa wanafundishiwa hivyo vitabu vya historia kwamba tulikua manyani,haya wanasayansi na wandugu nawasilisha hoja hapa tuijadili.
 
Inategemea unaamini nini, ukumbuke kuwa History ina-base katika evolution na dini ina-base katika creation.,sasa kwa mwana historia ataamini kuwa binadamu (tena si waafrika tu) tumetokana na nyani, lakini kama unaamini katika creation huwezi kuupa nafasi upuuzi huo wa kwamba zamani tulikuwa manyani.,hizo documentaries hazina mpango,zimetengenezwa na wazungu ambao wanaona kuwa waafrika si lolote.,hushangai mbona wao hawasemi kuwa nao walikuwa manyani?, sote si binadamu sasa iweje sisi asili yetu iwe hiyo na wao iwe nyingine?.
 
ndio hicho nnachoshangaa kwasababu kama ni manyani basi hata wao walikua hivyo pia.
 
Back
Top Bottom