Deva
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 1,237
- 1,819
Habari za mida hii wakuu.
Mimi ni kijana wa miaka 24
Nipo chuo nasomea masomo ya afya Mwaka wa tatu ambao ni wa mwisho.
Katika mawazo yangu ninawaza kuoa mwanamke mara tu nitakapo maliza masomo yangu mwaka kesho hii kwa lengo la kupata mtoto, maana naona kuwa sitaweza kuzaa na mwanamke nje ya ndoa.
Je ni kwanini nimefikia kuamua kuoa?
Nimefikia maamuzi ya kuoa baada ya kumpoteza mwanangu wa pekee( Hii story nimeshaileta humu jinsi alivyouawa).
Sasa najiona mpweke sana kiasi kwamba sioni kama nitaweza kukaa muda mrefu bila kuwa na mtoto (naomba kudeclare interest kuwa ninapenda watoto na wala sijawahi kukataa mimba, kwangu mimi mtoto ni pendekezo namba moja kwenye maisha yangu).
Sasa ninahisi njia pekee itakayonipa faraja ya maisha ni kupata mwanamke ambaye atakuwa wangu wa maisha na kunizalia watoto.
Najua humu kuna watu wazima wenye busara za kutosha mmepitia mambo mengi yenye kuwapa ujuzi , naomba mnipe ushauri katika suala hili.
Asanteni.