Je ni serikali ya jamhuri ya Tanzania au?

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
wadau mtanisamehe,mimi nimekua nikitatizwa na utambulisho wa Serikali yetu hii pendwa,naomba msaada,hivi serikali yetu ya muungano inapaswa kutambulika vipi kati ya SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AU SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA?Kuna moja ina makosa lazima je ipi sahihi?
 
Chunguza majina yafuatayo:

1. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
2.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
-Hapa chukulia kwamba 'Tanzania' ni contracted form ya 'Tanganyika na Zanzibar'.
3.Serikali ya Jamhuri ya Tanzania
-Hapa chukulia kwamba 'Tanzania' ni contracted form ya 'Muungano wa Tanganyika na Zanzibar'.

Nina uhakika na usahihi wa jina number 1 lakini number 2 na 3 inabidi tuamue maana haiko wazi ni scenario ipi kati ya hizo mbili inatumika.
 
Neno Tanganyika viongozi wetu si wanatuambia ni dhambi kulitaja?hebu tujaribu kutii marufuku hiyo....je serikali yetu ya mungano tunaitambulishaje?ni serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania au ni serikali ya jamhuri ya muugano ya Tanzania?
 
Naomba majibu jamani mbona mmenichunia,hii inanisumbua kweli kweli....
 
mkuu umepewa jibu ukasema kuna marufuku na unatii hiyo marufuku basi tii na hiyo Jamhuri ya Muungano!
 
sasa ni jamhuri ya muuungano wa tanzania au jamhuri ya muungano ya tanzania?

Yote hayo ni makosa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar! Itakuwaje ya Serikali ya Muungano wa Tanzania (Tanzania na ipi). Itakuwaje Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (kiswahili hakikubali) lakini umesema kuna marufuku basi tukubaliane na watawala na tuitambue kama ilivyo hadi hapo tutakapopata fursa ya kuijadili. Lakini pia nasikia hilo si suala la kujadili wakati wa kujadili katiba mpya! Naona fursa zimefungwa basi ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Kuna wakati nilikuwa napit uwanja wa ndege mmoj hivi huko africa magharibi nikaulizwa unatoka wapi basi nikasema kwa mbwembwe kuwa natoka United Republic of Tanzania nikaulizwa what do you mean by united republic ikabidi nianze maelezo mareefu!
 
Back
Top Bottom