Je ni sahihi kwa CHADEMA kutumia zaidi ya shilingi milioni 400 kwenye Msiba wa Alphonce Mawazo?

Weston Songoro

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
2,793
1,083
Kuna taarifa zinasikitisha na kuhuzunisha. Zinaleta simanzi kwa wasomaji wa taarifa hizo hasa ndugu wa marehemu.


Kwamba, msiba wa Alphonce Mawazo, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita umekuwa na sura mbili kwa CHADEMA. Sura ya kwanza ni kujijenga kisiasa baada ya kufanya vibaya kwenye uchaguzi Mkuu uliomalizika ambapo CCM kimeibuka mshindi kwa nafasi zote yaani Urais, Ubunge na Udiwani.


Sura ya pili ni ya kiuchumi. Kumbe kuna jamaa ndani ya CHADEMA wamepiga mpunga wa maana kwenye msiba huo. Taarifa nilizopata hivi punde kutoka kwa mtonyaji wangu ndani ya makao makuu ya CHADEMA zinasema kuwa shilingi milioni 400 zimeidhinishwa kutumika kwa ajili ya msiba wa Mawazo. Kwamba, fedha hizo ni kwa ajili ya kugharamia usafiri, chakula na malazi kwa viongozi wa CHADEMA walioenda kwenye msiba huo. Aidha, fedha hizo pia ni kwa ajili ya kuandaa mikutano au kwa jina jingine mikusanyiko ya kuuaga mwili wa Mawazo. Vile vile mtonyaji amesema kuwa fedha hizo pia zimetumika kutoa rambirambi kwa wafiwa ambapo hata hivyo, haijabainishwa ni kiasi gani cha fedha kimetengwa kwa madhumuni hayo


Taarifa zaidi zinasema kuwa wakati makao makuu wakiidhinisha fedha hizo, Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE aliwasilisha maombi binafsi kwa Edward Lowasa ili aweze kutoa shilingi milioni 200 zisaidie kuratibu shughuli za kuuaga mwili wa Alphonce Mawazo. Inadaiwa kuwa, Lowasa ametoa kiasi hicho cha fedha ambacho hata hivyo, haijulikani wapi kimepelekwa.


Mtonyaji wangu amenitonya kuwa, imekuwa ni desturi ya viongozi wa CHADEMA kutumia misiba ama matukio mengine ya majanga kujinufaisha. Anasema kuwa hata alipofariki Mohamed Mtoi, zaidi ya shilingi milioni 170 ziliidhinishwa Makao Makuu kwa ajili msiba huo. Hata hivyo, imeelezwa kuwa ni shilingi milioni 12 tu ndizo zilizotumika tena kwa matumizi ambayo hayana uthibitisho wa dhahiri.:angry:
 
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana hata wangetumia milioni 800 inakuhusu nini?umbea na unafiki peleka huko lumumba
 
Hivi, ile sheria ya makosa ya mtandao ni kwa wafuasi wa CHADEMA tu kama akina Yeriko Nyerere??? Mimi tu kuuliza????
 
endelea kutonywa nataka nikutonye na mimi unajua natembea na mkeo leo mr kutonywa mwanaume mzima unakaa kutonywa tonywa JIPU MKUBWA
 
mi nilijua baada uchaguzi Lumumba mngeacha propaganda bado mpo mnakula shushu mnaimba taarab R.I.P KAMANDA MAWAZO
 
Poor thinking capacity, hakuna hoja ya msingi hapo wala public interest. sijaona unachotaka kutuambia ni nini kwani hoja yako ya msingi ni ipi? matumizi? ingekua fedha wamepata kwa njia zisizo halali tungekuelewa.. Rudi shule
 
Umeandika mengi sana, lakini la msingi:

CCM, RC na RPC Mwanza mmeumbuka!!!

Mlitaka kufuta ile imani tuliyo nayo kuwa Binadamu wote ni Sawa.

Mlitaka Mawazo afukiwe kama mzoga wa mbwa bila kupewa heshima anayostahili.

Mlitaka kifo cha Mawazo kisitajwa, kwa kuwa kinagusa na kusuta dhamiri zenu, kwa kuwa mnajua kilichotokea mpaka akafa.

Kweli mwisho wa ubaya ni aibu.
 
Ni sahihi kabisa ukilinganisha na alivyouwawa,kwanza sio kifo cha natural which means ni watu wameamua kuyafupisha maisha yake,lakini pili huyu mtu anafamilia je mlitaka familia yake iishije?anahitaji kuanza kujipanga
 
Mwenyekiti wa CHADEMA,
FREEMAN MBOWE aliwasilisha
maombi binafsi kwa Edward Lowasa ili aweze kutoa shilingi
milioni 200 zisaidie kuratibu
shughuli za kuuaga mwili wa
Alphonce Mawazo.


Sijawahi kuwaamini Wachagga kwenye jambo lolote.
 
Katika maisha ogopa watu wanaoongea sana Mara nyingine ni waongo
 
Back
Top Bottom