Je, ni nani aliwasilisha pingamizi la Mahakama kwenye Uchaguzi wa Meya?

Determinantor

Platinum Member
Mar 17, 2008
57,757
92,185
Kuna taarifa kwamba Mahakama ya Kisutu haikutoa zuio la Kimahakama kuzuia uchaguzi wa U-meya Dar es salaam na kwamba zuio la mwisho kutolewa na Mahakama hio ilikua ni February 23 mwaka huu, kama kweli taarifa hii, Je ni nani aliwasilisha ZUIO hilo siku hio ya uchaguzi? Nani alilipokea? Document hio ni nani anayo?

Je, kama ni kweli hakukua na ZUIO halisi la kimahakama, sharia inasemaje kuhusu watu waliopeleka zuio hilo? Mods tuiche kidogo hii tusichanganye na ile.

UPDATE
Kwakua ZUIO lilikua feki basi walioleta zuio feki wakamatwe, na kwa kauli moja SIRRO awaachie huru na kuwataka radhi wabunge waliokamatwa. Walioleta zuio feki ndio chanzo cha vurugu hao ndio wa kukamatwa. Huu ni upuuzi
 
Amri ya Uchaguzi huo ufanyike tarehe ya juzi ilikuwa ni ya Simbachawene waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi. Maana yake ni amri ya ofisi ya rais ambayo Tamisemi iko chini yake.
Sasa kumbe hakuna zuio lolote la mahakama kama alivyosema Kaimu mkurugenzi wa jiji akiahirisha uchaguzi huo.
Maana yake ni nini? Ni kwamba Amri iliyotolewa imedharauliwa na kutengenezewa hila kwa kuisi gizia mahakama.
Hii imeonyesha Waziri muhusika kaonekana bwege na ofisi ya Rais Tamisemi sii lolote wala chochote kwa Mkurugenzi wa jjiji na hawamuwezi na kwamba hizi mbwembwe za hapa kazi tuu ni wimbo kama zile za Diamond zenye wapenzi wengi
 
Hakuna zuio la mahakama, na kama lingekuwepo waziri asingetoa amri uchaguzi ufanyike, mi nadhani Makonda alimpigia simu mkurugenzi akazuie uchaguzi, na waziri akija kuhoji Makonda anaweza kumpiga Magufuli alikosea kumsifia makonda hadharani.
 
Hakuna zuio la mahakama, na kama lingekuwepo waziri asingetoa amri uchaguzi ufanyike, mi nadhani Makonda alimpigia simu mkurugenzi akazuie uchaguzi, na waziri akija kuhoji Makonda anaweza kumpiga Magufuli alikosea kumsifia makonda hadharani.
Kwahio kwanini uchaguzi uliahirishwa? Aliahirisha uchaguzi alipata wapi hio mandate? Na kwanini Polisi walifanya fujo? Maswali haya yanaumiza mno...
 
Kwahio kwanini uchaguzi uliahirishwa? Aliahirisha uchaguzi alipata wapi hio mandate? Na kwanini Polisi walifanya fujo? Maswali haya yanaumiza mno...
Mkuu uchaguzi uli ahirishwa kwa sababu hawataki meya toka ukwa aliongoze jiji, kwa sababu ni lazima ukawa wangeshinda, kuhusu mandate, hiyo sasa imewekwa pembeni kila sekta maamuzi yanafanyika kwa utashi wa mfanyaji, hata sheria za kazi zimewekwa kando kwa muda usio julikana,kwa polisi lazima wajitutumue kwa kuwa wametumwa na watawala na wanataka kuuthibitishia uma wao wako gado, haya matukio ya ujambazi yanatokea ni tukio la bahati mbaya, intelijensia kubwa ipo kudhibiti wana siasa..
 
Hahahhaa lazima ukweli ufahamike, ni nani alitangaza kuwa kuna zuio la mahakama? Kama MANI hawa watu niwakufungia jiwe shingoni kisha watoswe pale baharini
Kuwatosa baharini hawa ni kutia najisi viumbe kama samaki na pweza ambao tunavifanya kitoweo.
Ni wa kuchoma moto na majivu yake kufukia porini tuu. Majitu mazima hata aibu hayaoni?
Mie nadhani ili kumshtua Magu bora siku nyingine uchaguzi ukitangazwa watu wa Dar waende na mabango pale nje na moja lisomeke: MZEE POMBE HAWA CCM WANAKUCHEZEA WANAKUONA MSHAMBA KWA VILE UMETOKA USUKUMANI. SHITUKA [HASHTAG]#HAPAKAZITUU[/HASHTAG].
Labda akiliona kwenye tv atashtuka na kuwakomesha
 
Hilo Zuio Ni Magumashi Tupu, Kuthibitisha Hilo Kuwa Ni Magumashi, Kwanza Tarehe Ya Zuio Hilo!! Pili Aliyeleta Au Kuweka Zuio Hilo Hatambuliki Na Aliyepokea Pia Hajulikani!! Tatu Ni Ile Hali Ya Naibu Mkurugenzi Kushindwa KULISOMA Kwa Ufasaha, Kana Kwamba Liliandikwa Kwa Mkono Vile, Mara Zuio Hili Litaisha Baada Ya Siku 3, Mara Ni Baada Ya Miezi 3, Ghala Ni Baada Ya Miezi 6!!!! Sitaki Kusema Mkurugenzi Hawezi Kusoma Kwa Vile Hati Ile Iliandikwa Muandiko Mbovu, Au Alikuwa Wamesahau Tarehe, Hivyo Alikuwa Akibahatisha Tu!! Ila Mwenye Akili Timamu Atakuwa Ameliona Hilo, Kama Ilikuwa Akisoma Zuio MAGUMASHI!!! Nne Kama Ilikuwa Zuio La Kweli, Why Walitoa Barua Za Kuwaalika Wajumbe Kuhudhuria Mkutano Ule Wa Uchaguzi, Na Waliandaa Mazingira Ya Kufanyika Kwa Uchaguzi Ule!!!?? Na Why Alianza Kusoma Muktasari (Dondoo) Wa Kikao Na Kusoma Akidi Ya Kikao Kile, Wkt Huo Kuna Zuio Halali La Mahakama!!!!???
 
Hakuna zuio la mahakama, na kama lingekuwepo waziri asingetoa amri uchaguzi ufanyike, mi nadhani Makonda alimpigia simu mkurugenzi akazuie uchaguzi, na waziri akija kuhoji Makonda anaweza kumpiga Magufuli alikosea kumsifia makonda hadharani.
Ni kweli kabisa hizo ni siasa za Makonda na Nape.Ingekuwa vyema.Rais ajitanabaishe kuwa ni Rais wa Watanzania wote bila kujali itikadi.
 
Kuna watu humu walikuwa wanasema matatizo ya Zanzibar hayatuhusu. Sasa hizi ndizo athari zake. Ikiwa Jecha kafuta uchaguzi mkuu na hajafanywa kitu, atakuja kuwajibishwa alofuta uchaguzi wa meya wa jiji? It's embarassing at the best!
Nilikua na mawazo kama yako.labda na jiji la dar halimuhusuu
 
Back
Top Bottom