Je, ni mara ngapi huwa unaenda hospitali kucheki usalama wa afya yako?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,420
40,408
Tambua hili

Viungo vya mwili, kama; moyo, mapafu, figo, ini; havijawahi kupumzika kufanya kazi, tangu ulipozaliwa.

Kama una miaka 70; ina maana viungo vyako hivyo, vimefanya kazi bila kupumzika kwa miaka yote 70, sawa na siku 25,550.

Kupumzika kwa viungo hivyo katika kufanya kazi; kunaweza kusababisha umauti, au njia ya kuelekea kwenye umauti.

Swali la kujiuliza; kama chombo cha usafiri, kikitembea umbali fulani, huwa tunakipeleka sehemu husika kwa 'service'.

Je, ni mara ngapi huwa unaenda hospitali kucheki usalama wa viungo hivyo? Ambavyo, huwa havilali wala kupumzika, muda wote vinafanya kazi tu.
 
Nadhani service ndo muhimu, piga lishe na kuushughulisha mwili kunatosha mzee.

Kwenda kuyatafuta ili uyapate halafu iwe nini? Utayajua na uwezo wa kuyakabili pengine huna, utaambiwa nenda India tu hapo kubadilia ball joint, unaanza kuuhusisha ukoo na marafiki!

Tushazoea mambo ya ghafla sisi, habari za kuambiwa eti umebakisha hardly miezi 4 kuishi na mikato ya walamba asali!
 
Kwa hiyo mkuu, inabidi tuishi kwa kubahatisha?
 
Tushazoea mambo ya ghafla sisi, hab
ari za kuambiwa eti umebakisha hardly miezi 4 kuishi na mikato ya walamba asali!
Unabadili ball joint kwa fundi Maiko mwenye gereji chini ya mwembe, ahaaaa
 
Kujitafutia mapresha tu...kwa lifestyle yetu kma uko poa ni bora kukausha tu,ukijfanya kwenda kwenda huko ipo siku jamaa watakwambia ini lako limetoboka lina mashimo ya kutosha....ukiipata hyo taarifa hapo ndo utakapoanza kuchngnykiwa na soon watu wanaweka turubai home kwenu/kwako.,Bora ni kumuomba Mungu tu atulinde kama anavyowalinda vichaa na wendawazimu.
 
Kwa hiyo mkuu, inabidi tuishi kwa kubahatisha?
Hamna kaka, unaenda sehenu kucheki, ile full medical check up, unaambiwa 800,000.

We fikiria tu mwenyewe, hata kama ni mara moja kwa mwaka, wangapi wanaweza? Na kwa bahati mbaya sasa hata ukianza sasa, kama vya ndani vilishaanza kuiva tangu ukiwa tegemezi(wazazi na walezi wachache wanafikiria hizo mambo), utaishia kujua tu, ukipeaa gharama za kuanza kurekebisha ambapo mara nyingi sio guaranteed kuwa utakuwa sawa, unaona bora umwagilie moyo, kwani nini!
 
kupima afya ya vitendea kazi haina tofauti na kupima ngoma.
kupima afya tuachie matajiri ambao ndio wako weak..kila siku kuumwa na hospitalini (spana mkononi).

sisi tunakaa huku unga limited ikitokea tumekufa ni umepigwa beto au ajali ya bike.
eti sijui marelia au uti hatuijui.
tunakunywa vitoko kwenda mbele.
hata kaswende na gono zinaisha zenyewe bila dawa
 
Kama huna uwezo wa kujitibu vizuri na ni masikini wa kipato hata usiende kabisa

Ni kujitafutia BP na Stress haswa.

Kwasababu utaweza kuambiwa una shida ya sukari kupanda au kuwa chini, au uambiwe upitishwe kwny CT scan...una pesa?

Ukiambiwa una tatizo la ini? Au ukiambiwa unapaswa ukachekiwe mishipa ya macho kwenye hospital flan kubwa ya gharama una uwezo huo?

Wakikuambia unapaswa kufanya mazoezi kila siku na kula ''balanced diet'' utaweza?

Tumshukuru Mungu kwa uzima tuishi tu.
 
Ndo maisha yetu wenyewe, mpaka life span imefikia 49, mdogo mdogo...si umeona mambo ya korona, ile ndo ilikuwa medical check up yetu, kama umetoboa, basi huko ndani piston ring na mabering nini yako pouwa! Ipe mzigo
W

We jamaa Una ufala ujue 🤣🤣
 
Tambua hili

Viungo vya mwili, kama; moyo, mapafu, figo, ini; havijawahi kupumzika kufanya kazi, tangu ulipozaliwa.

Kama una miaka 70; ina maana viungo vyako hivyo, vimefanya kazi bila kupumzika kwa miaka yote 70, sawa na siku 25,550.

Kupumzika kwa viungo hivyo katika kufanya kazi; kunaweza kusababisha umauti, au njia ya kuelekea kwenye umauti.

Swali la kujiuliza; kama chombo cha usafiri, kikitembea umbali fulani, huwa tunakipeleka sehemu husika kwa 'service'.

Je, ni mara ngapi huwa unaenda hospitali kucheki usalama wa viungo hivyo? Ambavyo, huwa havilali wala kupumzika, muda wote vinafanya kazi tu.
Tuanze na wewe tujibu.
What I know to know,to talk is easy the hardest part is to do with what you know or you talk
Ni kama vile wewe unavyomponda huyo Mama ukiwa hujui vilevile kama wamelipia au wamechukua Tu!
 
Screenshot_20220620-233846_1.jpg
 
Ndo maisha yetu wenyewe, mpaka life span imefikia 49, mdogo mdogo...si umeona mambo ya korona, ile ndo ilikuwa medical check up yetu, kama umetoboa, basi huko ndani piston ring na mabering nini yako pouwa! Ipe mzigo
Ila mpaka iwe ume ugua
 
Hii ni kwa mbele na wados mzee.
Ni muhimu lakini kipato ni changamoto kubwa sana.

Hospitali gharama ni kubwa mno kwa hizo mambo, unaua mtaji ama lah utalaza vijana na njaa.
Kwanza wadau watakushangaa unaendaje hospital na huumwi😁😁
 
Nahisi siku nikienda kucheki afya yangu labda ndio siku ambayo nitaanza kudorora kiafya kwa msongo wa mawazo. Ngoja nitulie tu.
 
Tambua hili

Viungo vya mwili, kama; moyo, mapafu, figo, ini; havijawahi kupumzika kufanya kazi, tangu ulipozaliwa.

Kama una miaka 70; ina maana viungo vyako hivyo, vimefanya kazi bila kupumzika kwa miaka yote 70, sawa na siku 25,550.

Kupumzika kwa viungo hivyo katika kufanya kazi; kunaweza kusababisha umauti, au njia ya kuelekea kwenye umauti.

Swali la kujiuliza; kama chombo cha usafiri, kikitembea umbali fulani, huwa tunakipeleka sehemu husika kwa 'service'.

Je, ni mara ngapi huwa unaenda hospitali kucheki usalama wa viungo hivyo? Ambavyo, huwa havilali wala kupumzika, muda wote vinafanya kazi tu.
Mie siamini vipimo vya mabeberu
Naendaga kwa mganga wa jadi Dr Kalumanzila kupiga ramli kila baada ya miezi mitatu
Ramli ikisoma wingu jeusi au nyota chafu napigwa nyungu ya mawe na vichale kidogo vya makalio mambo yanakaa sawa
Ila siwezi kwenda kupimwa vipimo vya mabeberu nikaambiwe bure kwamba nina ngoma maana hizi mbususu za wauza pombe mwitu wa hapa Dom najipigiaga pekupeku tu
 
Kujitafutia mapresha tu...kwa lifestyle yetu kma uko poa ni bora kukausha tu,ukijfanya kwenda kwenda huko ipo siku jamaa watakwambia ini lako limetoboka lina mashimo ya kutosha....ukiipata hyo taarifa hapo ndo utakapoanza kuchngnykiwa na soon watu wanaweka turubai home kwenu/kwako.,Bora ni kumuomba Mungu tu atulinde kama anavyowalinda vichaa na wendawazimu.
Hii comment nimecheka sana aisee
 
Ukihisi tofauti ndo unapaswa kwenda kucheki tatizo ila kama unafeel good ukapime ya nini kama sio kiherehere?
 
Back
Top Bottom