Je, ni Mambo gani yalikuwa ya kawaida sana miaka ya 1980s - 1990s ambayo Vijana wa sasa hawawezi kuyajua?

1999 ulikuwa wapi weye
Nilianza vibaya huo mwaka, nilishindwa kuripoti chuo, nilimtandika demu mimba, nikamkimbia(hofu ya utoto),mara paap!!! Kwenye foleni ya kumuaga Mwalim pale Taifa ndugu wa demu hawa hapa....
Ahsante Mungu kijana amesha kua leo tumetoka kutazamana utadhani mabeberu ya mbuzi.

Disco show kipindi cha Uncle J Nyaisanga...
 
Duh! Kwa hiyo jamaa wakaku tight au ikawaje bro?
 
Viwanja vya michezo vilijengwa kwa nguvu za wananchi,lakini ujio wa mfumo wa vyama vingi ulipoingia CCM wakajimilikisha bila ridhaa ya wananchi wala Serikali.
Ilipaswa viwanja vya michezo virejeshwe kwa wananchi ili visimamiwe na Halmashauri husika.
MFANO:
1. Tabora:Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,urudishwe Manispaa ya Tabora.
Ujenzi wake ulihamasishwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Marehemu Lawrance Gama,na Kufanikisha kuwa na Timu ya Ligi kuu iitwayo Milambo FC.
2.Songea:Uwanja wa Maji Maji,ilikuwa ni michango ya nguvu za wananchi,vile vile ikihamasishwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Ruvuma Marehemu Lawrance Gama,vile vile alihamasisha kuwepo timu ya Maji Maji FC.
Uwanja huu urejeshwe kwa wananchi kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Songea ili usimamiwe vizuri,na kutoa ajiri kwa vijana kwa kukuza michezo kwa uratibu wa afisa michezo ngazi za Halmashauri.
3.Mbeya:Uwanja wa Sokoine,vile vile nguvu za wananchi zilitumika kufanikisha ujenzi.
Uwanja urejeshwe kwa wananchi kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Mbeya.
4.Shinyanga:Uwanja wa Kambarage,uerejeshwe kwa wananchi kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,ili iweze kutoa ajira kwa vijana na kukuza michezo.
5.Mwanza:CCM Kirumba,nayo irejeshwe kwa wananchi kupitia Halmashauri kwa ajili ya matunzo,usimamizi,maboresho na kutoa ajira kwa vijana.
6.Arusha:Amri Abeid,na wenyewe urejeshwe kwa wananchi kupitia Halmashauri ili kuimarisha michezo kupitia idara za utamaduni na michezo ili kuwapa vijana ajira.
7.Tanga:Mkwakwani
8.Iringa:
9.Singida:iliyokuwa uwanja wa Namfua
10.Kigoma:
11.Rukwa:
12.Mtwara:
N:B:
1.Viwanja vilijengwa kwa hamasa kubwa wakati mi
ji ikiwa na matarajio ya kuandaa sherehe za kitaifa "enzi hizo"
2.Hii Rais Magufuli akiweza kurejesha viwanja vya namna hii Serikalini,nina uhakika na yafutayo:
(a).Viwango vya michezo kitakuwa nchi nzima
(b).Mapato na kodi itaongezeka Serikalini
(c).Usimamizi wa viwanja utakuwa madhubuti
(d)."Uhamisho huu wa Viwanja kutoka CCM kwenda Serikalini"unawezekana,kwani hata Mwenge ulikuwa unakimbizwa na chama,lakini baadae chama kikaona ni mzigo kusimamia na kuendesha,Hatimaye "mbio za mwenge"zikapelekwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya uratibu na usimamizi.!!!!
 
Nakukbuka kama ukienda na demu wako disco au dada ako yaani msichana yeyote wako unaporwa na magenge ya wahuni wanacheza nae wanamkumbatia na wewe usemi lolote kimyaaaa!maana kwanza mmetoroka home kwenda disco.
 
nakumbuka tukiwa tunaoga mtoni, huku kwetu kuna mto kulikuwa na sehemu ya kuoga wanawake na wanaume.... mida ya saa kumi jioni kila mtuu anaelekea huko..
dah. Sahii huo mto hakuna tena umebakia kamfereji kadogo mnoo...
 
Kutembea huku unasikiliza radio ndogo,
Au mziki kupitia "Walk man"kifaa kidogo unaweka Kanda/tape yenye muziki,unasikiliza na head phone,
 
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…