Je, ni kweli utajiri unapatikana shambani?

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema sekta ya kilimo nchini inatarajiwa kukua kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030 ukilinganisha na ukuaji wa sasa wa takriban asilimia 3.6.

Rais Samia amesema Tanzania imetengeneza fursa za kitaifa kwa ajili ya mabadiliko ya mfumo wa chakula unaotarajia kuongeza uzalishaji wa chakula, kuimarisha maisha ya watu na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Serikali ya Rais Samia Suluhu inajua asilimia kubwa ya watanzania wamejiajiri katika kilimo ndio maana inaendelea kukipaisha kilimo kimataifa ili vijana wengi wajiajiri kwenye maana gharama za kilimo zimepungua lakini pia jitihada kadhaa zimefanyika, ikiwemo kuanzisha mradi kwa ajili ya vijana huku wakiendelea kuimarisha ukuaji wa shoroba za kilimo.
 
Ok tumekusikia Chawa mpendwa!

FB_IMG_1674134227879.jpg
 
Ni vilee tu huo msemo haujaeleweka tu mtu akisema

Utajiri unapatikana shambani - hapo kuna vitu vitatu kama itaeleweka

1) utajiri
2) kupatikana
3) shambani

1) utajijiri - ni wingi wa kitu, na wengi tumezoea wingi wa pesa sawa ni pesa ila wingi wa vitu vingi tu ni utajiri nisiwavuruge acha tubaki kwenye wingi wa pesa.

2) kupatikana-hapa pia panajulikana kama hauelewi tofautisha upatikanaji na ukosekanaji utapata kujua maana ya neno hilo.

Shamba- hapa ndio kwenye point, shamba ni kitu chochote kinachotoa faida uenda kipo hai au hakipo hai ndio shamba, kwenye kitabu fulani cha dini shamba ilichukuliwa kama mfano wa mwanamke, kuwa yaendeeni mashamba yenu mtakavyo / shamba limetumika kama uke hapo na katazo kubwa la kuendea wake zenu kinyume na maumbile, biashara yako waweza iita shamba , kuna jamaa yetu mmoja anajiita kashamba kadogo mavuno mengi, jokes

So mama pengine ana style ya kutuelekeza tuvune katika mashamba yetu vizur mashamba ambayo sisi wenyewe tunayajua, achaneni kuhusu kilimo unaweza lima na bila kupata mbegu physical na ukapata faida pia, tunamuelewa sana mama na late kubwa sana ya watu wa vijijini wanakuja mjini na wakikaa miaka minne mpak mitano wakirudi vijijini kwao wamefanikiwa na vijiji vikiwafurahia inamaana kabisa kulima bila elimu ni kazi bure , pembejeo duni mbolea hafifu na wakishapata mazao wanapangiwa bei kwa kutishiwa na mpaka kukopwa.
 
Back
Top Bottom