Benki ya Dunia imetoa Mkopo wa zaidi ya Shilingi Bilioni 700 Kwenye Kilimo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Haya wakulima mshindwe wenyewe mabilioni ndio hayo

======
Benki ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wa Dola za Marekani milioni 300 za Marekani, sawa na zaidi ya Sh700 bilioni kwa ajili ya kuchochea uzalishaji na kuimarisha sekta ya kilimo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mkopo huo uliotolewa chini ya programu ya matokeo (PforR) ambayo inafadhiliwa na na Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA), unalenga kusaidia utekelezaji wa programu ya kuendeleza kilimo awamu ya pili (ASDP II).

Miongoni wa mambo yatakayotekelezwa ni pamoja na na kuboresha utoaji wa huduma katika utafiti, ugani, na mbegu, kuendeleza miundombinu ya kilimo maeneo ya vijijini pamoja na kuimarisha usimamizi wa rasilimali fedha na uwekezaji.

Wakulima 300,000 sawa na asilimia 2.5 ya wakulima waliopo nchini wanatarajiwa kunufaika moja kwa moja na mkopo huo ambapo nusu yake watakuwa ni wanawake huku wengine milioni 1.8 wakinufaika kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, zaidi ya Watanzania milioni 12 wanajishughulisha na kilimo ambacho kinachangia asilimia 26 ya pato la Taifa na asilimia 65 ya ajira.

Hivi karibuni kumeibuka msukumo wa kuimarisha sekta ya kilimo nchini Tanzania ambapo kwa mara ya kwanza Wizara ya Kilimo imeidhinishiwa na Bunge bajeti ya Sh970.7 bilioni ambapo iliongezeka kwa asilimia 29 kulinganisha na bajeti ya mwaka 2022/23.

Nathan Belete ambaye ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania amebainisha kuwa kutokana na umuhimu wa sekta ya kilimo katika ukuaji wa uchumi, mkopo huo utachochea ukuaji wa sekta hiyo pamoja na kusaidia kuimarisha uhimilivu wa chakula.

"Kilimo ni ufunguo wa ukuaji wa uchumi shirikishi na kupunguza umaskini vijijini nchini Tanzania. Programu hii itasaidia kuimarisha ukuaji wa sekta ya kilimo pamoja na mifumo himilivu ya chakula pamoja na kutengeneza ajira,” amesema Balete.

Programu hiyo ya PforR ni awamu ya pili kati ya tatu za utekelezaji wa mradi wa kuimarisha mifumo na uhimilivu wa chakula kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika ambao utagharimu jumla ya Dola milioni 903 za Marekani (zaidi ya Sh2.1 trilioni) ambapo nchi nyingine wanufaika ni pamoja na Kenya, Malawi, Somalia, Ethiopia pamoja na Madagascar.

Mabadiliko ya tabianchi, janga la Uviko-19 na vita ya Urusi na Ukraine ni miongoni mwa mambo yaliyoathiri upatikanaji wa chakula kote duniani huku nchi masikini zikiathirika zaidi.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, watu zaidi ya milioni 83 waliopo Kusini na Mashariki mwa Afrika wapo katika hatari ya kukabiliana na uhaba wa chakula au baa la njaa.

“Kuimarisha mifumo ya chakula, uhimilivu pamoja na kuiongezea Tanzania uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kunahitaji mabadiliko katika taasisi pamoja na namna ya kufanya kazi. Programu hiyo itakuja na njia za namna ya kukabiliana na ukame, pamoja na teknolojia za kutoa mwelekeo wa hali ya hewa,” amesema Emma Modamba mtaalam wa masuala ya uchumi na kilimo wa Benki ya Dunia.

NUKTA
 
Back
Top Bottom