POTOSHI Je, ni kweli shahidi kesi ya Lissu alisema 'Makatibu wa wilaya CHADEMA walipewa milioni 10 kukinukisha nchi nzima

POTOSHI Je, ni kweli shahidi kesi ya Lissu alisema 'Makatibu wa wilaya CHADEMA walipewa milioni 10 kukinukisha nchi nzima

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
1771500795968.png
 
Tunachokijua
Kesi ya mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kuhusu mashitaka ya uhaini, imeendelea katika mahakama kuu huku mashahidi wa Jamhuri wakitoa ushahidi wao.

Madai

Kumekuwapo na nakala ya ukarasa wa mbele wa gazeti la Mwananchi la Februari 17, 2026 lenye habari kubwa ukurasa wa mbele ikidai kuwa Shahidi ameeleza makatibu wa wilaya Chadema walipewa Milioni 10 kukinukisha nchi nzima.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia nakala hiyo na kubaini kuwa inapotosha uhalisia.

Nakala hiyo yenye ujumbe wa kuwa shahidi amesema vingozi wa Chadema walilipwa kukinukisha ni potoshi kwani ni maneno ambayo hayapo katika nakala halisi ya Februari 17, 2026 ya gazeti la Mwananchi.

Ufuatiliaji umebaini kuwa nakala halisi ilikuwa na ujumbe unaoseomeka;

"Mnyukano wa shahidi, Lissu" na siyo "Shahidi: Makatibu wa wilaya Chadema walipewa milioni 10 kukinukisha nchi nzima"

Aidha, Februari 17, 2026 kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Taifa, Tundu Lissu iliendelea katika mahakama kuu ambapo mashahidi wawili wa Jamhuri walitoa ushahidi wao.

Mashahidi hao walikuwa ni ASP Geofrey Agrey Lutufye pamoja na shahidi wa kificho P4 ambao walitoa ushahidi wao bila kutaja suala hilo la Makatibu wa Chadema wilaya kupewa pesa ili wakinukishe.

Hivyo nakala hiyo yenye ujumbe tofauti ilihariririwa kutoka kwenye nakala halisi ili kupotosha uhalisia.
mashahidi wa kificho hata script yao waliyoandikiwa hwaijui loh, nchi ngumu sana hiyo mara zote mambo yakubumba na kutunga mwishowe wacheza sinema hupoteana. Nasubiri pia shahidi Samuya na wambura na majaliwa nao wapande kizimbani, kama hawajazikana jinsia zao hadharani.
 
Back
Top Bottom