Mk54
JF-Expert Member
- Dec 29, 2016
- 1,996
- 3,962
KABLA YA KUTOA MAAMUZI YA MWISHO YA KURA YAKO, TAFADHALI TAFAKARI!
1. Je, ni kweli RUSHWA imepungua?
TAFITI sizizo rasmi ni kwamba RUSHWA bado ipo kwenye taasisi za UMMA na viongozi wetu bado wanakula rushwa. Inaonekana haipo kwa sababu hakuna chombo cha habari chenye GUTS za kuripoti UFISADI unaoendelea kwa viongozi na taasisi za UMMA. Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
2. Je, ni kweli hakuna AJIRA?
Suala la kujiajiri au kutoka nje ya BOX ni UZUSHI kama hutowezeshwa. wewe kama mzazi unajisikiaje kumuona mwanao amemaliza chuo na yupo yupo tu anacheki FILM?
-
Malalamiko mengi juu ya AJIRA nyingi kupewa WANAJESHI huku wenye taaluma wakiendelea kusugua. Hata hivyo, TAFITI zisizo RASMI zinaonesha ya kwamba asilimia kubwa ya WANAJESHI hawafanyi vyema kwenye TAASISI HIZO kutokana na ukosefu wa Management and Leadership Skills. Wao wanachojua ni KOMANDI TU, Tumeona kwenye ishu ya Mkurugenzi wa TAKUKURU huku maafisa zaidi ya 5 wakifukuzwa kazi yeye akiendelea kuwepo kwenye nafasi yake. Kuna yule Brigedia mwingine aliharibu na kuingia kwenye kashfa ya UFISADI, Badala yake alipewa UBALOZI huku watumishi wengine wakitumbuliwa na kuozea segerea, je usawa upo wapi? Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
3. Je, ni kweli watumishi wa UMMA hawajaongezewa mishahara?
TAFITI za kibenki zinaonesha watumishi wa UMMA wengi wanaishi chini ya thelusi ya mshahara ghafi kwa wingi wa madeni huku wengine wakikimbilia kwenye MICROFINACE na mwishowe kuuziwa mali zao kama GARI na NYUMBA. Aidha, inasemwa PAYEE imepungua kutoka asilimia 15 hadi 11 ambayo ni sawa na ongezeko la kati ya 9 000 hadi 12,000 katika mshahara ghafi kwa kipindi cha miaka 5. Kura yako ndio sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
4. Je, ni kweli Sheria ya Manunuzi ya Umma Na.7 ya mwaka (2011) na Kanuni zake (2013) sambamba na Marekebisho (2016) haifuatwi
Wengi hawakuridhishwa na MAELEZO ya msemaji wa SERIKALI. IKama ilikuwa ni Restrictive Tendering Method ndiyo iliyotumika kumpata MSHITIRI, na kwakuwa MANUNUZI ya ndege yanahusisha Maslahi ya Taifa, kwanini hakukuwa na TRANSPARENCY? Inawezekana wazo la kununua ndege kwa CASH lilikuwa ni zuri, lakini tukubali kuwa UTEKELEZAJI wake umefeli. 90% ya mashirika ya ndege duniani yanajiendesha kwa hasara. Je la kwetu vipi? Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
5. Je, Ni kweli bodi ya Mikopo imeshindwa kusikiliza wanufaika?
Makato ya MKATABA wa awali baina ya BODI na WANUFAIKA yalikuwa ni asilimia 8 katika mshahara ghafi, mwaka 2015 ilipandishwa kutoka asilimia 8 hadi 15 kinyume na mkataba wa awali huku tozo ya asilimia 6 ikiwa ipo pale pale. Barua pamoja na malalamiko yalipelekwa Bodi ya Mikopo huku barua za malalamiko zikienda IKULU bila mafanikio. Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi. Tumia fursa ya kuomba karatasi nyingine ya kupigia kura kubadili maamuzi na mtazamo wako.
-
6. Je, ni kweli familia ya Mwalimu imesahaulika?
Mpinzani alipofika BUTIAMA, familia ya Mwalimu ilimkaribisha, akala na kulala kisha wakampeleka kuhani kaburi. Katika chakula cha usiku, familia hiyo ilimueleza Mpinzani huyo masikitiko yao juu ya kusahaulika na kusisitiza kwamba watampigia kura Mpinzani huyo ikiwa ni sehemu ya CHUKIZO. Alisikika Mama Maria akisema, kwenye kampeni ameenda kuongeza idadi tu. Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
7. Je, ni kweli TANROADS ni mtoto wa mwisho anaedekezwa?
Changamoto za TANROADS zinajulikana kwa ujenzi wa barabara chini ya viwango kwa takribani miaka yote 25, barabara ambazo kila mvua zikinyesha ni lazima ziwekewe VIKARA. Je kuna siri gani nyuma ya pazia ya TANROADS? Kila siku barabara zinajengwa na kila siku barabara hizo hizo zinaharibika, je huu ni mradi wa mtu binafsi katika kutumia kodi zetu isivyo halali? Raisi halijui hili? Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi.
-
8. Je, BIMA ya Afya kupitia NHIF, haikidhi haja za waTanzania?
Wanaofaidika na NHIF ni wale ambao wapo katika AJIRA. Ikiwa hujaajiriwa, ili upate Bima ya NHIF, ni lazima uwe na pesa taslimu 1,550,000 kwa kila mwaka ambayo kimsingi mkulima wa kawaida hawezi. Suala la Bima ya Afya kwa kila Mtanazania lipo kisheria, kuendelea kuweka kiwango cha pesa hiko ni kuwanyima watanzania haki zao za msingi. TAFAKARI SANA. Kura yako ni sauti yako, fanya maamuzi sahihi. Achana na ma TV na MATANGAZO, angalia hali halisi ya MTANZANIA WA LEO
-
9. Je, ujenzi wa SGR hauna uhalisia?
Ni takribani miaka 4 mpaka leo hii ujenzi huu haujaweza hata kufika Morogoro, je itachukua miaka mingapi kufika DODOMA? TAFAKARI, kura yako ni Sauti yako, fanya maamuzi sahihi
Mwisho, Tuliombee Amani taifa letu na usikubali kuaminishwa kuwa kila unapotoa maoni yaliyo kinyume na UTAWALA basi wewe ni MSALITI au SIO MZALENDO. Huenda wewe ni MZALENDO ZAIDI. Aidha, Taifa letu tukufu linaweza kuongozwa na mtu yoyote mwenye SIFA. Hakuna watu maalumu kuwa wao ndio FIMBO ni lazima kuongoza. Yoyote anaejaribu kupata ridhaa hiyo hutengenezewa mazingira aonekana MSALITI AU SIO MZALENDO. TUMIA Neema ya akili yako kutafakari.
Fanya maamuzi sahihi, just decide, make a difference make a choice. Dunia ni yako na wote sisi ni MAVUMBI. TUAMUE KWA MANUFAA YA VIZAZI VYETU. TUAACHANE NA MATV NA MATANGAZO TANGAZO, KITU KIZURI HAINA HAJA YA KUTANGAZWA, KINAONEKANA, HIVYO, TUANGALIE HALI HALISI YA MTANZANIA WA LEO.