Je, ni kweli Mgeja kugombea Msalala?

Je, ni kweli Mgeja kugombea Msalala?

kama uwezekano wa kushinda upo hakuna shida. cha msingi ccm itoke kwanza madarakani. mengine baadae...

Nimekufurahia sana uelewa wako. Huo pia ndio msimamo wa upinzani na msimamo huo ndio uliounda ukawa. Madhumuni ya vyama vilivyounda ukawa yalikuwa mawili makubwa.Moja kutetea katiba nzuri ya wananchi bunge la katiba na pili kuiondoa madarakani ccm na mfumo wao m-bovu wa kukumbatia wezi,waingizaji madawa ya kulevya na kuogopa kuwafikisha mafisadi mahakamani eti nchi itatikisika. Fisadi anaambiwa lipa kidogo hutapelekwa mahakamani. Maamuzi hayo yalifikiwa na wenyeviti na makatibu wa vyama hivyo na walikubaliana kuwa katika kutimiza lengo mapungufu yoyote yatakayojitokeza yataangaliwa baada ya zoezi. Kwamba watamsimamisha mgombea yeyote toka chama mshirika atakaeonekana ana uwezo na ushawishi na pia anaeuzika kwa wananchi ili kupata mafanikio.Sasa ndio zoezi lipo katikati lakini tayari tumeshawagundua na wasaliti wa makubaliano na wenye kudai mimi nimekitumika chama zaidi ya aliyependekezwa. Kwanini hawataki kuheshimu makubaliano na wanayoyaona ni mapungufu yakasubiri hadi mwisho wa zoezi?.Mwenyekiti wa chadema kwenye hotuba yake alisema mwanachama alieingia chama miaka kumi iliyopita ana haki sawa na aliyejiunga leo.Kutumikia chama kwa muda mrefu ni wajibu kwa mwanachama. Katika hatua tuliyo nayo na kwa wote wenye mapenzi mema kwa ukawa watakuwa tayari kukubali kuachia chochote ili lengo lifikiwe.
 
Back
Top Bottom