kamili
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 1,213
- 849
Tangu Muammar Gaddafi auawe kikatili na utawala kuchukuliwa na NTC wananchi wa Libya wameingia katika dhama mpya ya mateso yasiyoelezeka, kama ambavyo taweka baadhi ya ushahidi huo hapa.
Tuliona baada ya vita ya Iraq jinsi Marekani walivyomkabidhi Saddam kwenye mahakama ambayo walijua mwishowe itamhukumu kunyongwa, na jinsi kulivyozuka vitendo vya kigaidi ambavyo havikuwahi kutoke Iraq kabla haijavamiwa na Marekani. Tumeona pia uvamizi wa Afghanistani mwisho wake kumetokea vitendo vya kigaidi vya kujitoa mhanga, ambavyo Kabla ya uvamizi huo havikuwahi kuwepo.
Kwa kuwa Tanzani tuliwahi kuwasaidia Waganda kutoka mikono dhalimu ya Idd Amin na hakukuwahi kutoke visa vyovyote vya kigaidi.
Je itakuwa ni makosa kuamini kuwa uvamizi wa Marekani kwa kisingizio cha kuleta demokrasia, kupigana na magaidi, au kutaka kuondoa silaha kali kama walivyofanya kwa Iraq na sasa wanaitaka Iran, kuna lengo la kuzivuruga nchi na kuleta mauaji ya kikatili yasiyo na msingi?.
Na je kwanini vyomba vya habari vya magharibi havitangazi yale mateso yanayowapata Walibya kwa sasa?
Na je kwanini wauwaji wakubwa kama Charles Taylor kaua zaidi ya watu 200,000, Slovodan Milosovich aliyeuwa zaidi ya watu 100,000, na wauaji wa Rwanda walioua zaidi ya watu 800,000, wamefikishwa mahakama ya kimataifa ambayo licha ya kesi kusikilizwa kwa haki na uwazi haina hukumu ya kifo. Lakini watu kama Saddam, Osama aliyeuwa 3,500, Gaddafi (na sasa Seif al Islam) hawa ama waliuawa kikatili au walikabidhiwa kwenye mikono ya wanyongaji. Na kwa upande mwingine Joseph Kony anatafutwa ili akashtakiwe kwenye mahakama ya ICC. Je tofauti hii inaletwa na nini?
zaidi hapa. Libya S.O.S.: Torture in Libya [ WARNING: THESE IMAGES MAY SHOCK VIEWERS]
Wana JF naomba mjadala maana mwenzako akinyolewa wewe tia maji.