Je, ni kweli kwamba yule kada wa CCM anayehusishwa Kuhamia ACT ni huyu?

Nachofahamu jamaa hatorudi bungeni na zengwe linasukwa kwa ustadi mkubwa sana, maana kwenye orodha ya waliokua wanamsemasema jiwe pembeni vibaya na wakiwa karibu wanamsifia yumo, tusubiri muda ufike.
 
Wafanyakazi wa serikali mmeshapata mshahara?? tuanzi kwanza hapo
 
Hili hata sio fumbo. SUBIRINI MWINGINE. NINA AKILI TIMAMU NISHINDWE KUSHIBA WALI ULIOKO KWENYE SINIA NIKATEGEMEE KUSHIBA WAKUOKOTA CHINI. ? SIO MIMI WA KUHAMA CCM, SIO MIMI WA KUHAMIA ACT
Kumbe siasa kwako ni wali tu wa kwenye sinia?
 
Hili hata sio fumbo. SUBIRINI MWINGINE. NINA AKILI TIMAMU NISHINDWE KUSHIBA WALI ULIOKO KWENYE SINIA NIKATEGEMEE KUSHIBA WAKUOKOTA CHINI. ? SIO MIMI WA KUHAMA CCM, SIO MIMI WA KUHAMIA ACT
Aliyezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi. Uondoke huko bao la mkono umuachie nani?
 
Ukisikia mtu anataja jiwe jua no binadamu dhaifu na mwoga sana
Yaani nina hamu kweli nimjue huyu JIWE kwani kila Siku huwa naona Watu wakimuandika na kumtajataja sana hapa ila nimejitahidi Kumjua nimeshindwa hadi hivi leo. Ni nani huyu JIWE jamani?
 
Umesahau kitu kimoja .Ni yule aliyekusanya nyuki kibao kwenye sandarusi mwaka fulani wa uchaguzi akaenda kuwaachia kwenye mkutano wakati mpinzani wake akihutubia, baada ya hapo mkutano wa mpinzani wake ukavurugika baada ya nyuki kuwauma sana wananchi waliookuwa wanamsikiliza mpinzani wake.
 
Jiwe..nasikia mason wameshindwa kabisa nyundo zao zimeharibika sababu yako..Jiwe yasemekana umegoma kupasuka hata kwa baruti..chembechembe zako ni mchanganyiko wa chuma cha pua cha SGR na mwamba moto..hakuna tena ulaji kila mason anarudi mikono mitupu..utasikia "ahh narudi nyumbani"
 

Huyu mtu ni muoga sanaa, na amezoea vya bure na vya kutafuniwa. Hivyo basi, mikiki mikiki ya upinzani hawezi kabisa, na akienda upinzani basi atarudi chama dola kabla hata uchaguzi wenyewe wa 2020 kwisha, maana haitokuwa uchaguzi, bali ni ujambazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…