Je ni kweli kwamba mapinduzi ya kiislam ya Iran yalisaidiwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,201
2,000
Iran ni nchi ya kiislam ya misimamo mikali ya kutaka kuiangamiza israel
Kuna ukweli wowote kuwa wamarekani, uingereza na ufaransa walimpa sapoti khomein kuanzisha jamhuri ya kiislam ya iran
Hii ni kwasababu mbona mpaka leo israel na marekani hawajaishambulia iran?
 
Mibas

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
3,723
2,000
Kuna watu wanatapika hapa utadhani wanaijua IRAN, Mapinduzi ya Iran yalifanywa na waIran wenyewe bila msaada wa marekani wala uingereza
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,819
2,000
alichofanya REAGAN kwa kumtumia georg bush ni kumZUnguka jimmy carter kwa kudeal na khomein kisiri ili kuwezesha mateka wa marekani kuachiwa huru
 
crabat

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
4,324
2,000
Iran ni nchi ya kiislam ya misimamo mikali ya kutaka kuiangamiza israel
Kuna ukweli wowote kuwa wamarekani, uingereza na ufaransa walimpa sapoti khomein kuanzisha jamhuri ya kiislam ya iran
Hii ni kwasababu mbona mpaka leo israel na marekani hawajaishambulia iran?
Suali zuri na ukweli huku hivi .
muhumu kujua kabla ya Islamic Republic kuanzishwa kujua Iran ilikua chini ya nani ? Iran ilikua chini ya Monacrch wa zaidi miaka 2000 chini ya Shah Mohamed reza Khan Pahlavi.
ufalme huu ulikua rafiki wa Israel , USA na South Africa ya Makaburu
Shah alikua kipenzi cha west na kibaraka mkubwa.Alitumika sana kuzorotesha uhuru wa baadhi ya nchi.
  • Mfano miaka ya 70 kulikua na azimio la kuiwekea vikwazo Israel vya mafuta. Ncho zote za Opec zilikubaliana kuiwekea Israel vikwazo kutoka na ukaliaji wake wa maeneo ya Masri , Palestine, Syria na Lebanon, Vikwazo vile havikufanikiwa kwani IRAN chini ya Shah akitumiwa na West powers alivivunja na akawa ana supply mafuta Israel. Hivyo mpango ule uka fail.
  • pili Wakati UN iliwekea vikwazo South Africa ikiwamo kuuzuwa Mafuta ili kuibana kuachana na siasa zake za kikaburu...jumuiya yote ya Opec na wazalishaji mafuta walikubaliana kuto kuuza mafuta Kwa makaburu.Ni IRAN tena chini ya Shah ikavunja mpango huo na ikawa inauza mafuta kwa makburu. ( Kuja kwa Ayatollah na Islamic Republic ilikatisha kuwapatia mafuta Mkaburu na ikawa ndio chachu ya kuanguka)
Khomein mwanzo alikua akiishi Iran na kutokana na upinzani wake kwa Shah akafukuzwa hivyo akaamua kuishi Iraq . Huko Iraq chini ya Sadam ambaye alikua darling wa West akalazimishwa kumfukuza na akaamua kuhamia France.
akiwa huko ndiko aliainzisha harakati kubwa za kumuondoa Shah kwa kutumia mwavuli wa imani ya wairan ya Kishia. akapa uungwaji mkubwa mkono na raiaa wengi ambao walichoka na mambo ya shah.
France hawakumzuia kufanya siasa akiwa huko, inawezekana France haikufaidika sana na Shah ambaye alielemea sana USA. hIVYO ILIACHIA Ayatollah anedeshe harakati zake nchini ufaransa.
akaitisha migomo na maandamano makubwa yasio na kikomo...askari wa Marekani na wale wa Shah walifanya kila mbinu za mateso na mauaji lakini raia hawa kusimama wala kuvunjika moyo.
Utawala wa shah ukaanza kuporomoka na Shah akakimbia siku Ayatollah alipotangaza anarudi IRan.

kitu interesting ni kuwa France walitoa ndege yao Airbus iliyo msafirisha Khomein kutoka France akiwa na familia yake na timu yake yote ya wapinzania iliokuwa ikiishi uhamishoni. Juhudi za USA, Israel na Iran na UK kuitaka France asimruhusu kurudi hazikusikilizwa na Ufarance ...hatimae Khomein alitua Teheran na Utawala kibaraka wa Shah Ukaanguka.
Hivyo utaona USA na other western countries hawakusaidia Kuanzishwa kwa Taifa la kiislam la Iran. Ufaransa alishiriki kusaidia moraly kwa tamaa ya kuwa na influence kwa utawala mpya. Ingawa hakufikiria kama utawala utakaongia utakua too extreme ...lakini upande mmoja France ndio bado wananufaiaka sana kibiashara na Iran mpya ingawa vikwazo vilizorotesha.
Hii video inaonesha siku za mwisho za Shah
 
mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
3,625
2,000
Ndio walisaidiwa na hao mabeberu. Sio hao tu sehemu nyingi tu hasa Saudi Arabia pia.
 
well said mkuu vp ufaransa ilifaidika labda na uhusiano mwema na iran?
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,033
2,000
Tawala nyingi duniani zinawekwa na USA na mashosti wake.
Nchi chache sana ambazo haziingiliwi na Marekani.
 
Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,856
2,000
Tawala nyingi duniani zinawekwa na USA na mashosti wake.
Nchi chache sana ambazo haziingiliwi na Marekani.
Umenena vyema bujibuji sisi tunaojua mambo huwa hatupingi hilo. Nina mambo mengi ya kueleza ila siku hizi nimekuwa mvivu kweli wa kuandika.
 
crabat

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
4,324
2,000
well said mkuu vp ufaransa ilifaidika labda na uhusiano mwema na iran?
Ukweli france ilitegemea kuvuna kwa ile sapoti yao ya kumuweka Khomeini France . Na role yao ya kumpa usafiri kurudi Iran.
Lakini miak ya kwanza haikua rahisi sana, utekwaji wa balozi ya US kule Tehran , Iran kuanzisha kikundi cha Kigaidi cha Hizbullah , kuuliwa kwa mabalozi wa EA ujerumani yalidhoofisha hatua za mashirikiano.
Kuja kwa vita vya Iran na Iraq Nayo ikazorotesha uhusiano huo kwani france ilimpa sapoti zote Sadam Hussein.
Hat hivyo kabla ya sakata la vinu vya nuclea ufaransa na iran baada ya vita na iraq wakawa na uhusiano mzuri .Total ilipata tenda nyingi za kuchimba mFuta.
Waliwauzia ndege za kivita pamoja na spare za nd egezao.
Pia france alikubali kuwauzia iran uranuim cetrufuge kwa ajili ya reactors zao ili kuepuka ku process iran .
Kuja kwa Kahtaw kama rais wa france pia kulizidisha uhusiano wa biashara.
Hata hivyo kuna mikwamo ya hapa na pale kutokana na sera za iran za kupenda kujitanua na kuingilia nchi nyengine kwa kutumia madhehebu yao ya kishia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom