Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 308
- 424
Jana Agosti 29, 2025, Humphrey Polepole kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii alidai kwamba mtungi wa gesi ya kilo 15 nchini Cuba unauzwa kwa shilingi 2,000 za Kitanzania.
Kauli hii imeibua mjadala, lakini inapochunguzwa kwa makini kwa kutumia takwimu na taarifa rasmi, inabainika kwamba ni madai hayo hayana ukweli wowote na wengine kusema kwamba, pengine amesema vile kwa ajili ya mtaji wake wa kisiasa. Kabla ya kujua hali ya halisi ya mtungi wa gesi wa Kg 15, kwanza tutambue hali ya sasa kwenye gesi ya kupikia nchini Cuba.
Hali ilivyo Cuba
Kwa mujibu wa taarifa ya Havana Times (Prieto, 2025), Cuba inaendelea kukumbwa na uhaba mkubwa wa gesi ya kupikia. Tangu mwishoni mwa mwaka 2024, miji na mikoa kadhaa ikiwemo Matanzas, Camagüey, na Pinar del Río ilisita kuuza gesi “hadi taarifa itakapotolewa,” kutokana na kutokuwepo kwa akiba ya bidhaa hiyo.
Wakazi wengi wanalazimika kutumia kuni na mkaa kama mbadala, hali inayorudisha nyuma maisha ya kila siku na kusababisha madhara ya kiafya kutokana na moshi na vumbi. Wengine wanalazimika kupanga foleni ndefu, mara nyingine kwa siku nzima, bila uhakika wa kupata hata silinda moja.
Kwa hali ilivyo, gesi haiwezi kuuzwa chini ya USD 1, yaani TZS 2000, hali ya gesi ya kupikia nchini Cuba ni mbaya.

Bei halisi na soko
Kinyume na madai kwamba gesi inauzwa kwa TZS 2,000 (takribani USD 0.75), hali halisi ni kwamba gesi nchini Cuba imegeuka bidhaa ya kifahari.- Sokoni, bei ya gesi Kg 15 ni kati ya 35,000–40,000 peso za Cuba, sawa na takribani USD 100.
- Hii ni mara nane ya mshahara wa mwezi mzima wa raia wa kawaida wa Cuba (ambao ni wastani wa 4,648 peso).
Kwanini gesi haiwezi kuwa TZS 2000
Kwanini Gesi Haiwezi Kuwa TZS 2,000 Nchini Cuba
- Gharama za uagizaji na uhaba wa fedha za kigeni
Cuba haina vyanzo vya ndani vya gesi ya kupikia (LPG). Gesi yote huagizwa kutoka nje, jambo linalohitaji malipo ya fedha za kigeni. Kwa kuwa nchi hiyo ina matatizo makubwa kwenye sekta ya utalii na vikwazo vya kiuchumi (sanctions) kutoka kwa mataifa ya magharibi hivyo, kuwa na akiba finyu ya dola. Haiwezekani gesi iingizwe na kuuzwa kwa bei ya chini ya dola moja. - Mfumuko wa bei na sarafu ya ndani
Uchumi wa Cuba unakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei. Kiasi cha sarafu yao (peso) inapoteza thamani kila mwaka, na bidhaa zinazotegemea uagizaji zinakuwa ghali zaidi. Kwa mfano, mshahara wa wastani wa raia wa Cuba ni 4,648 peso (sawa na karibu USD 13). Kwa hali hii, haiwezekani bidhaa muhimu na adimu kama gesi ibaki kwa bei ya sawa na robo ya dola ya Marekani. - Uhalisia wa soko la magendo
Ripoti zinaonyesha gesi ikipatikana sokoni kwa njia ya magendo, bei yake ni 35,000–40,000 peso (takribani USD 100). Hii ndiyo bei ambayo wananchi hulipa kwa uhalisia, si bei ya nyaraka za serikali. Ikiwa bidhaa moja sokoni inauzwa mara 100 zaidi ya bei inayodaiwa na Polepole, basi dhahiri bei ya TZS 2,000 haiwezi kuwa kweli. - Kanuni ya scarcity (Uhaba)
Kitaalamu, uchumi hufundisha kwamba kadiri bidhaa inavyopungua sokoni, ndivyo bei yake inavyoongezeka. Katika hali ambapo gesi inapatikana kwa foleni na muda mwingine haipatikani, hivyo gesi haiwezi kuwa TZS 2000, lazima itakuwa juu zaidi. - Ulinganisho na uchumi wa kawaida
Hata katika nchi zilizo na ruzuku kubwa (mfano India au baadhi ya mataifa ya Kiarabu), gesi ya kupikia hufikia angalau USD 8–15 kwa mtungi kwa kg 15. Kwa hiyo, kudai kwamba nchi ya Cuba yenye changamoto za kiuchumi na upungufu mkubwa wa fedha, bei ni chini ya USD 1, haiwezekani.