Je, ni kweli Dola leo hii inanunuliwa kwa zaidi ya shilingi 2300?

Potential effects of the anticipated drastic measures to be adopted by the EU to punish Tanzania for the abuse of human rights and lack of respect for the rule of law.
 
Tumenunua sana fedha kuliko kuuza, miradi yote mikubwa imechukua kodi zetu kwenda kulipa nje ni had tumalize kulipa.Ukifanya miradi mingi mikubwa lzm dola ipande
 
hahahaha mmesharukia kwenye dola hahaha hili la dola bora mliache maana haliwezi kudumu kabisa mbona ikishuka hampost? kwani ilikuwa Tsh ngapi? hahahaha

Sio kurukia hiyo inaonyesha kufeli kila idara yaani unashindwa hata kustanilize bei ya chumvi
 
Wadau utalii wazungumzia BoT kufunga maduka ya kubadilisha fedha

By
Mtanzania Digital
-
November 22, 2018
0

113



Share














ELIYA MBONEA Na ABRAHAM GWANDU-ARUSHA
WAKATI maduka ya kubadilishia fedha Arusha yakiwa bado yamefungwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na operesheni ya kukagua biashara hiyo juzi, wadau wa utalii jijini humo wamezungumzia hatua hiyo na maendeleo ya sekta ya utalii.
Mfanyabiashara mkubwa katika sekta ya utalii mkoani hapa Wilbert Chambulo, jana aliliambia gazeti hili kuwa hatua ya BoT haijaathiri sekta ya utalii kwa vile watalii wanaweza kupata huduma hiyo kwenye hoteli wanazofikia.
Chambulo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (TATO) aliyewekeza katika Kampuni za Kibo, Tanganyika, hoteli na kambi hifadhi tofauti nchini, alisema yeye binafsi anakubaliana na utaratibu uliotekelezwa na BoT.
“Kwa ujumla sekta ya utalii haijaathiriwa… Kama athari zipo basi walioathirika ni wale wafanyakazi wa sekta ambao ni Watanzania waliotaka kubadilisha fedha za kigeni wapate shilingi.
“Utaratibu huu, binafsi nakubaliana nao…hata kama ikiwezekana maduka yote yakafungwa na sheria ikatulazimisha kwenda kubadili fedha BoT bado itakuwa ni sahihi.
“Umeona wapi Dola ya Marekani imekuwa ya shida hapa mjini? Nenda kwa wachuuzi wa bidhaa zinazouzwa kwa wageni…wote wanatumia dola. Hoteli za kawaida, shule mpaka migahawa ya kawaida nao wanachaji kwa Dola,” alisema.
Chambulo ambaye pia anamiliki duka la kubadilisha fedha eneo la Mnara wa Saa jijini hapa, alisema operesheni ilichelewa kufanyika kiasi cha kuruhusu wafanyabiashara kulipisha wanunuzi wa huduma mbalimbali kwa kutumia fedha za kigeni.
“Kitu hiki ni aibu na tusi kwa sarafu yetu ya Tanzania, tofauti na jirani zetu sisi tulifanya uzembe. Ukienda Kenya au Afrika ya Kusini hawaruhusu haya mambo holela holela.
“Ukipata dola zako kabadilishe ukajieleze ulivyozipata ndipo uende kulipia huduma unayotaka, si vinginevyo,” alisema Chambulo.
Kuhusu madai kuwa BoT iliondoka na fedha za watalii kwa baadhi ya maduka, alisema madai hayo hayana ukweli kwa sababu watalii hawabebi fedha taslimu bali hulipia huduma zao moja kwa moja kupitia wakala.
“Wengine wanasema eti watalii wanahaha, huo ni uwongo, watalii watahaha vipi wakati wameshalipa huduma zao zote za safari?
Hata kama wana kiasi kidogo cha fedha taslimu wanabaki nazo ndizo wanazolipia ‘tip’ baada ya safari au ununuzi wa vitu mbalimbali na hulipa kwa fedha za kigeni,” alisema.
Nao baadhi ya madereva wa watalii walisema pamoja na umuhimu wa hatua hiyo, bado kwao kulikuwa na usumbufu hususani walipotaka kuacha fedha za matumizi kwa familia zao.
“Hatua si mbaya isipokuwa lilileta usumbufu kwetu, madereva tuliokuwa tunasafiri na wageni. Kama unavyojua ukiwa na familia huwezi kusafiri bila kuiachia familia hela ya matumizi,” alisema Alex Murro na kuongeza:
“Tulipata usumbufu, familia zetu ziliathirika kwa sababu tulikuwa na fedha za kigeni na hapakuwa na mahali pa kubadilisha”.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Walter Maenda, alipoulizwa kuhusu wanachama wake walioathirika na hatua hiyo, alisema hakuwa na taarifa yoyote inayoelezea kufungiwa maduka yao.
“Sijapata taarifa zozote kutoka BoT kwa nini hawa wamefungiwa maduka yao, asante sana,” alisema Maeda na kukata simu.
MTANZANIA lilimtafuta kwa simu Mkurugenzi wa BoT Tawi la Arusha, Charles Yamo kufahamu idadi kamili ya maduka yaliyokumbwa na opWadau utalii wazungumzia BoT kufunga maduka ya kubadilisha fedha Wadau utalii wazungumzia BoT kufunga maduka ya kubadilisha fedha | Mtanzania via @Mtanzaniaeresheni hiyo lakini alisema bado ni mgeni na ana wiki moja tu kwenye ofisi hiyo.
 
Kupanda na kushuka dola ni kawaida..asubui unakuta 2100,
Mchana unaweza kuta 2200..kesho tena tofauti..zito sasa ameamua kushinda mjini kuokoteza habari..ishu ya dola si habari..enzi za jk ilifika hadi 2400
Actually ilifika 2500
 
Kupanda na kushuka dola ni kawaida..asubui unakuta 2100,
Mchana unaweza kuta 2200..kesho tena tofauti..zito sasa ameamua kushinda mjini kuokoteza habari..ishu ya dola si habari..enzi za jk ilifika hadi 2400
......
......labda lumumba
 
Back
Top Bottom