Je! Ni Kweli BVR Machine zina Background Database of Pseudonames?

Mwaka huu patachimbika UHUNI hautavumiliwa.
 

Vilevile kuna haja ya kujiuliza inakuwaje NEC wanasema wamepita malengo yao ya uandikishaji kwa kiasi kikubwa wakati watu wengi wanalalamika wameshindwa kujiandikisha.
 

Ni kweli kabisa zina kuwa na majina maana machine hizo zilitumika Mikoa /vituo vingine...kazi ya wakala ni kutunza kumbukumbu za kila siku mmeandikisha watu wangapi siyo kuangalia kwenye Database kuna watu wangapi..unaangaliaje kabla zoezi halijaanza mnakagua vitabu vyafomu ambacho kila Kitabu kinafomu 50 kila mkimaliza unaandika Kitabu namba ili mwisho Wa siku ujue Ni fomu ngapi zimetumika..
 
mashine hizi zimetoka kutumika mikoani ila inategemea kama hayo majina 1000 yaliandikwa eneo/mtaa huohuo ambapo ndo mtu wa kwanza alikuwa anaanza kuandikishwa ni hatari tupu.
Yani hii serikali ni pasua kichwa balaa
 
Hilo linawezekana, tena kirahisi sana kuingiza majina fake kwenye database. Kimsingi swali hiyo database ipo inasimamiwa na nani? Na hao waandikishaji wamepewa uhuru kiasi gani wa kuingiza majina kwenye database
 
Cha msingi ni kuhakikisha kila mmoja wetu anapiga kura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…