Je ni kweli Africa inaongoza kwa ajari za ndege?

Isimilo

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
217
6
Sisi watu weusi ni wa ajabu sana.hatuwezi hata siku moja tukawakosoa hawa wenzetu hata pale wanapotubambikizia mambo ambayo sio ya kwetu.
mimi nimekuwa nikifanya utafiti wangu ambao hauhitaji elimu ya juu utaona ajari nyingi au tuseme ajari kubwa kubwa au tuseme ajari za ndege kubwa kama boeing, nyingi zinatokea Asia halafu labda ulaya na amerika kusini kwa kusema ukweli.tuache mambo ya hivi vindege vya miguu miwili mbele mmoja nyuma. lakini utakuta ulimwengu umetujengea sisi weusi hali ya kuonekana kwamba kila jambo bovu linatoka Africa. hata viongozi wetu au wataalamu wetu kwa kujipendekeza kuwalizisha hawa wenzetu mabosi wao nao unakuta wanaponda usafiri wa Anga kwa Africa. na hata zile zinazotokea katika anga ya Africa bado utakuta labda ndege yenyewe sio ya hapa Africa.
ajari za ndege za Africa labda za viongozi wetu nyingi unakuta kuna hujuma ndani yake. sasa huwezi kuhukumu mfumo mzima wa usafirishaji wa Ndege kwa Africa ukiingiza kwenye takwimu vitu kama hivyo.
mimi ajari kubwa kwa africa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita kwa ndege za abiria wa kawaida sanasana ni ile ya ndege yetu ya Kenya Airways KQ kule katika misitu ya Cameroon.
mara wanaita ndege za Africa moving coffin
lakini kwa huko ulaya ndege hasa Asia ndege za abiria wengi kuna kipindi zilifululiza mpaka nikawa nawahurumia huku waafrica tunadunda na hayo ma-moving coffin yetu.
ule ukanda wa ulaya inayokaribia kupakana na Asia vile vinchi vyote unakuta usafiri wao ni mgogoro
tufanye mathalani ndege ya Africa ikipata hitilafu angani wataishia kukosoa na kutulaani sisi waafrica lakini sivyo kwa upande wao
wao ndege zao zikipata hitilafu halafu ikatua salama utakuta hilo shirika linapewa sifa marubani wanafanywa maonyesho .kama ile British Airways iliyozimika wakati inajiandaa kutua pale hearthrow.rubani kasifiwa sana naye akawa anavunga hataki sifa kwa kusema nilichofanya ni wajibu wangu na nimefanya ninachotakiwa kufanya.haya hii ndege ya Australia Qantas iliyotoboka juzi wakalazimika kutua Philipine wakati ikienda Melbourne pia rubani kasifiwa kishenzi. Lakini ingekuwa ni ndege ya huku Africa tunge shambuliwa kweli na vyombo vya mahgaribi kwa kutuchafua.
sasa hebu ona huyu anayeleta hizi takwimu zake kwenye hii report hapa chini kwenye gazeti la nipashe.kiongozi wenu wa njia za Anga hapa Tanzania. yaani ikiwa ajari za Africa ni asilimia kumi then anasema africa inaongoza duniani kwa Ajari za Anga kwa hesabu zipi?
tena jambo moja limenifurahisha sana. Kenya marubani wao labda wote ni wazawa na tena ni washkaji wadogowadogo tu wanabuluza hayo maboieng yao bila wasiwasi. hapa tanzania kama hmjui hata zile speed boti za kwenda Zanzibar wameajiri wazungu ndio makepteni.siku moja kuna speed boti moja ilkwepa kuokoa watu waliopata ajari na jahazi sasa wakawa wanahojiwa na vyombo vya habari. kepteni aliye kuwa anajieleza alikuwa mzungu.Aibu gani hii jamani
mimi hatanikikutana na Air Zimbabwe napanda waache kutuyeyusha na data za uongo
hebu soma huu upuuzi hapa chini2008-08-07 09:41:30
Na Dunstan Bahai
Anga ya Afrika inaongoza kwa kuwa na ajali nyingi za ndege duniani.

Kauli hiyo ilitolewa na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga la Afrika Mashariki (CASSOA), Bw. Mtesigwa Maugo.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati shirika hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) lilipotangaza kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa warsha ya kimataifa ya kuimarisha usalama wa usafiri wa anga, inayoanza Agosti 12 hadi 14 mjini Arusha.

Alisema wastani wa asilimia 0.8 ya ajali zilizotokea duniani katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2004, Afrika ilikuwa ni karibu mara tano ya ajali zote.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu huyo, katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2007, wastani wa asilimia 1.1 ya ajali zote duniani, asilimia 10.1 kati ya hizo zilitokea Afrika.

``Warsha hiyo itakayoshirikisha wataalam mbalimbali wakiwemo watengenezaji wa ndege, itabainisha na kuelekeza maeneo yanayochangia kutokea kwa ajali hizo na jinsi ya kuyasimamia ili yasijitokeze tena,`` alisema.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bi. Margaret Munyagi, alisema mkutano huo ni muhimu kwani ni wa kimataifa.

Alisema mkutano huo umeandaliwa na Kamisheni ya Uongozaji wa Ndege wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO), TCAA, CASSOA, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege duniani (ACI), mashirika makubwa ya ndege kama Airbus na Boeing.

Bi. Munyagi alisema mkutano huo utafunguliwa na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa.

Aidha, alisema usafiri wa anga ni wa salama kuliko usafiri mwingine wowote duniani, hivyo mikakati inatakiwa kuwekwa ili kuimarisha usalama huo.

Alisema karibu asilimia 70 ya ajali za ndege duniani ni makosa ya kibinadamu, kama rubani akiwa angani ghafla anakutana na milima.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa TCAA, mkutano huo utafanyika kwa kanda kwani kwa nchi moja moja haiwezekani, ambapo nchi washiriki wa kanda ya Afrika Mashariki ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.
• SOURCE: NIPASHE
 
Back
Top Bottom