Je, ni kwanini asilimia 66 ya raia wa Nigeria hawatumii kondomu?

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
15 Februari 2020

Asilimia 34 pekee ya raia wa Nigeria wanatumia mipira ya kondomu wakati wa kufanya mapenzi, kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la NOIPolls.

Shirika la NOIPolls limesema matokeo yanaonesha kwamba asilimia 28 pekee ya idadi yote ya watu wanaotumia kondomu hutumia mipira hiyo kila wakati wanaposhiriki mapenzi.

Hilo linajitokeza licha ya kwamba wengi waliohojiwa wana uwezo wa kununua mipira hiyo.

Chike Nwangwu, Mkurugenzi Mkuu wa NOIPolls, ameiambia BBC kwamba dini na wapenzi kukataa kutumia kondomu ni miongoni mwa sababu kuu za wapenzi kukataa kutumia mipira ya kondomu.

"Maono na mitazamo ya watu juu ya kondomu, asilimia 63 ya raia wa Nigeria walisema kwamba cha kwanza kinachowajia akilini ni kwamba wanaposikia neno kondomu mtu anataka kujifurahisha kingono, huku asilimia 45 wakisema kwamba wao moja kwa moja kinachowajia akilini wanapomuona mtu na kondomu ni usherati," amesema.

Akitangaza matoeko ya utafiti huo huko Abuja, Nwangwu alisema asilimia 83 ya raia wa Nigeria wanaamini kwamba mipira ya kondomu inastahili kutumiwa lakini ni asilimia 34 pekee waliokubali kwamba wanaitumia.

Aidha alisema kwamba asilimia 26 ya waliohojiwa wanatumia mipira ya kondomu kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.

Bwana Nwangwu alisema kwamba utafiti huo ulifanywa kupitia maswali na kufasiriwa kwa lugha nne kuu nchini Nigeria, Pidgin, Yoruba, Hausa na Igbo.

Katika hotuba yake, Mkurugenzi Mkuu wa NACA, Gambo Aliyu, alisema matokeo ya utafiti huo yatawezesha serikali kubaini mianya iliyopo na kusaidia kukabiliana na virusi vya ukimwi.

Bwana Aliyu alisema kwamba uhamasishaji wa matumizi ya mipira ya kondomu siyo kuendeleza usherati miongoni mwa raia.

"Hatuendelezi usherati, bali kuhamasisha watu kuhusu kuzuia, maadili na tunataka watu kuwajibika.

"Tunahamisha watu kuwajibika lakini katika mchakato huo kuzuia ugonjwa wa Ukimwi ni jambo muhimu na ugonjwa huo unastahili kudhibitiwa ndani ya kipindi kifupi kabisa.

Chanzo: BBC
 
Hao ni wengi sana. Tanzania sijui kama asilimia 10 inafika. Mfano mzuri ni hawa wasanii wetu. Kila mademu wanaotembea nao wanalalamika kuwa wanamimba au wametoa. Kwahiyo niwapongeze sana Wanaìgeria kwahiyo 34%. Wanajitahidi sana.
 
Hili lile suala kuwa kuna condom mil 2 zilikamatwa bandarin zina virus vya ukimwi tayar ni kweli au ilikuwa kufitinishana? Tuwekane sawa hapo kwanza. Isiwe anayetumia anamtangulia wa peku kufa!
 
Lengo la tendo la ndoa kwa wanandoa ni kushirikishwa kazi ya Mungu ya uumbaji kupitia agizo la kuijaza dunia.
 
Hizi tafiti sio za kuziamini sana japo zinaashiria uhalisia.

Majibu yake ysnategemea sana utashi na utayari wa mhudika anayeulizwa maswali.

Hapo unaweza kukuta kuna watu wamesema wanatumia hata kama hawatumii, kwa muktadha huo kupata ukweli wa uhalisia wa jambo inakua ngumu hasa hasa Afrika.
 
Kutumia kondom ni kwenda kinyume na lengo la Mwenyezi Mungu kwa tendo hili takatifu.

Na kimsingi hadi kuitwa tendo la ndoa inamaana linatakiwa lifanywe na wanadoa tu.

Kondom zenyewe ni kuwahakikishia usalama watumiaji na hazihusiki na tabia ya watu kufanya tendo la ndoa.

Ni kama ilivyo na utata kumfukuza binti aliyepata ujauzito na kumruhusu aendelee na masomo wakati bado kuna sheria inayosema meanafunzi awe wa kike au wa kiume ikithibitika amejihusisha na mapenzi adhabu ni kufukuzwa shule. Mjamzito tayari ana ushahidi kwamba kafanya. Sheria ipitiwe upya.

Japo sio moja kwa moja lakini kuhamasisha matumizi ya kondom ni kuhamasisha tabia za uasherati na zinaa.
 
Na kimsingi hadi kuitwa tendo la ndoa inamaana linatakiwa lifanywe na wanadoa tu.

Konfom zenyewe ni kuwahakikishia usalama watumiaji na hazihusiki na tabia ya watu kufanya tendo la ndoa.

Ni kama ilivyo na utata kumfukuza binti aliyepata ujauzito na kumruhusu aendelee na masomo wakati bado kuna sheria inayosema meanafunzi awe wa kike au wa kiume ikithibitika amejihusisha na mapenzi adhabu ni kufukuzwa shule. Mjamzito tayari ana ushahidi kwamba kafanya. Sheria ipitiwe upya.

Japo sio moja kwa moja lakini kuhamasisha matumizi ya kondom ni kuhamasisha tabia za uasherati na zinaa.
Lakini kondom hazina usalama. Kitu chochote kisichokuwa salama kwa 100% maana yake chochote kinaweza kutokea.
 
Kutumia kondom ni kwenda kinyume na lengo la Mwenyezi Mungu kwa tendo hili takatifu.
Binadamu hufanya ngono kwa asilimia 99 kama starehe na asilimia 1 kwa kuzaliana.

Hii ni tofauti na wanyama ambao mpaka jike awe na yai lililo tayari kwa ajili ya uzazi ndipo dume atapata hamu ya kumpanda.

Hivyo binadamu wanahitajika kuwa na namna nyingine ya kuzuia mimba pamoja na maradhi ya zinaa hasa wale ambao hawana mke zaidi ya mmoja.

Pia binadamu kwa kiasi kikubwa inampasa apange kwanza kabla ya kuamua kuwa na mtoto. Malezi na kusomesha binadamu ni gharama kubwa sana hasa kama unataka kumjenga mtu anayejitambua na atakayeweza kuzikabili changamoto za dunia ya leo.

Sikubaliani na tafsiri rahisi ya kuwa ngono kwa binadamu ni kwa ajili ya uzazi pekee.
 
Starehe ni mengineyo, lengo la tendo la ndoa ni kuendeleza uumbaji. Linapaswa kuwa kati ya Wanandoa. Usipokubaliana na hiyo tafsiri haubadilishi uhalisia.
 
Starehe ni mengineyo, lengo la tendo la ndoa ni kuendeleza uumbaji. Linapaswa kuwa kati ya Wanandoa. Usipokubaliana na hiyo tafsiri haubadilishi uhalisia.
Uhalisia wa wapi huo?

Ingekuwa hivyo Mungu angezizuia hizo homone mpaka yai la mwanamke lifikie wakati ndipo upate hamu ya kulala naye.

Uhalisia ninaouoa hapa kwa mke wangu ni kuwa 99% ni kufurahishana na asilimia 1 kuzaa.
 
Shida upo busy kubishia vitu usivyovijua. Nenda ukasome concept of Freewill ndio uje tujadiliane.
 
Back
Top Bottom