Je ni kipi sahihi?

tian

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2007
Posts
1,770
Reaction score
538
Kama upo kwenye mahusiano na unaona kuwa haya mahusiano yenu hayana future ni njia ipo iliyobora ya kumweleza kwa mahusiano yafike kikomo?

1.Kumwambia sababu wazi wazi hata kama utamuumiza moyo.

2.Kumwacha kimya kimya.

Jamani nahitaji hoja ambazo ziko wazi zaidi,a honest answer from your heart.
 
ukitaka kuhamisha mlima unaanza na mawe madogo dogo
 
Wakati mnaanza tongozana kwani mlizevezana kimya kimya?

Kwa ustaarabu ule ule mliotumia wakati wa kufukuziana, ustaarabu huo huo utumike maji yakizidi unga.
 
Watu


kuna wengine makupe hawataki kukubali utafukiri mlisign mahali kwamba hamtaachana.
 
Last edited by a moderator:
Sahihi ni kumpa mwenzi sababu za wewe kutaka kuanza kurasa nyingine.ukishindwa hilo utawezaje kutoa notisi ya kuacha kazi,tunahitaji majasiri bana...
 
Watu

Ila nasikitika sana wengi huwa wanaacha kimya kimya.
 
Last edited by a moderator:
tian

Ni future ya aina gani unayo itaka katika mahusiano?

Usiongee tu future kumbe hata wewe wenyewe unaetaka kumwacha mwenzako hujui unachokitaka eti unacho kijua ni future
We kama unadhani future ni kuhaidiana kuoana wakati hizo ni ahadi sio future, na ahadi sio lazima zitimie
Utabadilisha wanaume wote kwa kuitafuta hiyo future na hautaipata unaishia kukutana na ahadi tu
Kabla haujaidai hiyo future lazima kuna mambo ya kujiangalia kwako wewe mwenyewe na ulikotokea yani kwa wazazi wako!!!

Sio eti uko chuo umekutana na mvulana wewe binti mtoto wa shekhe kijana mtoto wa mchungaji mmenogewa tu na mapenzi hapo napo unatafuta future.
Utatafuta sanaaaaa tu.

Mwenye mipango ya mwanadamu ni Mungu pekee sasa we unapanga hizo future zako unamshirikisha Mungu na kama ni hivyo je, haumu chukizi kwa kufanya dhambi ya uzinzi? unasubili ndoa hata kama uko kwenye mahusiano?

Future future future ni kitu gani hiki?
 
Last edited by a moderator:
Inategemea na mazingira na sababu za kuua uhusiano.
 
Its bora umwambie ataumia muda mfupi than kimya kimya itaumiza zaid na itamsumbua kisaikolojia. Be a man mpe fact aone ni sahihi unaloamua
 
Namba 1 ni bora zaidi umeamua kuachana na mtu mpe sababu
 

Maana yangu hapo ni kwenye malengo ya baadaye kama kuoa ama kuolewa,

Labda umekaa na mtu umeona kuwa tabia zenu hazishabihiani na wala hazivumiliki nahisi hapo hamtakuwa na any future plans especially kwenye swala la ndoa,

Na pia wewe unadhani kwa nini mahusiano mengi hayafikii kwenye ndoa??Ukinipa jibu basi hilo swala la future utakuwa umelielewa
 
Last edited by a moderator:
future katika mahusiano ukoje...?

Kwani wewe lengo kuu la kujihushisha na mwanamke inakuwa ni nini?

Lazima kila mahusiano unayofanya na mtu wa jinsi nyingine unakuwa na malengo na madhumuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…