Je, ni kifungu gani cha katiba kinachotamka kuwa kutakuwa na wabunge waliopita bila kupingwa?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,300
Wadau nawasalimu.Nimepitia KATIBA ya NCHI sijaona POPOTE ambapo Kuna Kifungu ktk KATIBA kinachotamka kuwa kutakuwa na WABUNGE WALIOPITA BILA KUPINGWA ktk Majimbo yao.

Lakini kupitia UCHAGUZI wa 2020 walipatikana WABUNGE WALIOPITA bila KUPINGWA Je kwa MUJIBU wa KATIBA yetu JE NI HALALI kuwa na WABUNGE HAO.

na je ni KUFUNGU gani cha KATIBA kinachowataja? Na kama HAKIPO je WABUNGE WALIOPITA BILA KUPINGWA ni HALALI kuendelea kuwa WABUNGE?

Naomba KUELIMISHWA​

20230918_000710.jpg
20230918_000722.jpg
20230918_000740.jpg
 
katiba yetu imezeeka, hakuna inayemshitua. Najiuliza watu wanahukumiwaje jela ilihali sheria mama za nchi (katiba) hazifuatwi na watawala? cheo cha naibu waziri mkuu kipo kwenye sheria gani ndani ya katiba? sheria ya uchaguzi inasemaje kuhusu haki ya mtu kupiga ama kupigiwa kura? watu wajinga wanasema katiba haileti maji wanashinda kujua kwamba maji na maendeleo haviwezi kuja bila sheria madhubuti inayotamka kuletwa kwa vitu hivyo. Kiongozi makini hawezi kuita katiba ya nchi et ni kijitabu.
 
Mkuu kuna mambo mengi sana yanafanyika nje ya matakwa ya katiba ambavyo ni sheria mama. Kuna maamuzi mengi yanafanywa kwa ajiñi tu ya kutaka kulinda maslahi binafsi ya kikundi kidogo cha watawala badala ya yale ya umma mzima wa Watanzania..

Yapo maamuzi yaliyojaa utata mwingu yanafanyika kwa kisingizio cha amri kutoka juu. Watawala wanajipa majukumu ambayo hata hayajahainishwa popote pale ndani ya vifungu vya katiba. Ukimya wa katiba iliyopo katika mambo mengi ya msingi na yaliyopitwa na wakati, ama mapya yanayopaswa kuwekwa kuendana na matakwa ya wakati, yanaipa mwanya serikali kujifanyia shughuli zake kwa mazoea, hisia na mihemko badala ya uhalisia, umakini na tija.

Mathalani, katika sakata la DPW tuliliona Bunge linajipa jukumu jipya na la ziada kutoa elimu kwa umma ili liweze kushawishi watu badala ya jukumu lake la msingi katika kuisimamia na kuishauri serikali. Aidha, tunashuhudia hivi sasa kuna takwa la wakati la hitaji la uwepo wa katiba mpya, lakini badala yake tunaishuhudia serikali ikijipa jukumu jipya la kutaka kuelimisha wananchi ili eti wailewe vyema katiba!

Hakuna anayejali kuhusu gharama kubwa iliyokwisha kutumika katika mchakato wa awali wa rasimu ya Warioba. Kuna mgogoro mkubwa sana wa kifikra, kimaudhui na kimantiki kutokana na akili ndogo kutawala akili kubwa.
 
Mkuu umeandika ukweli mtu Katiba inasema Waziri Mkuu atokane na Wabunge wa KUCHAGULIWA lakini Nchi hii ina WAZIRI MKUU wa KUPITA BILA KUCHAGULIWA
 
Wadau nawasalimu.Nimepitia KATIBA ya NCHI sijaona POPOTE ambapo Kuna Kifungu ktk KATIBA kinachotamka kuwa kutakuwa na WABUNGE WALIOPITA BILA KUPINGWA ktk Majimbo yao.

Lakini kupitia UCHAGUZI wa 2020 walipatikana WABUNGE WALIOPITA bila KUPINGWA Je kwa MUJIBU wa KATIBA yetu JE NI HALALI kuwa na WABUNGE HAO.

na je ni KUFUNGU gani cha KATIBA kinachowataja? Na kama HAKIPO je WABUNGE WALIOPITA BILA KUPINGWA ni HALALI kuendelea kuwa WABUNGE?

Naomba KUELIMISHWA​

View attachment 2752846View attachment 2752847View attachment 2752848
Uchafuzi wa 2020, ilikuwa ni kazi ya JPM na Mahera. Nawashangaa mnataka tujadili as if kulikuwa na uchaguzi.
 
Back
Top Bottom