Je, ni benki gani inatoza gharama nafuu?

Hata hapa bongo zipo benki nyingi ambazo ukiweka pesa hata kwenye account ya Savings kawaida kila muda fulani unapata interest.

Tatizo lenu mmeshazoea benki zenu hizo 3.

Mkuu ni Benki gani hizo naomba uniambie na sio interest inakuwa senti mbili alafu wanakata service charge mia tatu..;

ngoja nikupe mfano ukiweka hapa pesa zako lets say elfu 3000 (CRDB) na ukiziacha ukirudi baada ya mwaka utakuta pesa yako yote ishaisha (kwa service charge wanayokata kila mwezi)

Ukiweka pesa yako lets say hata pennies (50p) kwenye Benki UK (iwe barclays, HSBC, TSB au yoyote ile) ukirudi baada ya mwaka utakuta hio 50p yako imezaa vi-pennies vingine (that's what am talking about)

Benki ni biashara ya kukopesha watu na makampuni na pesa za kukopesha inatoka kwa watu kama mimi na wewe na wengine wanaoweka pesa Benki.., hivyo kutumia pesa yangu kukopesha watu alafu wanikati pesa kila mwezi eti service charge ni wizi (inabidi mimi ndio wanipe interest kwa kuwasaidia kuzalisha faida)
 
Sasa si ndo ufunguke uzitaje..na ndio lengo la thread..

Halafu hawa BOT si ndio kaz yao kudhibiti hiz gharama.

BOT nao pamoja na haya mabenki yote ni wezi.., inabidi kuwe na consumer protection act ya kuweza kuwabana hawa watu, sababu wanachokifanya sio haki (just imagine service charge zote wanazochukua kwenye kila account ya mtu) sijui nikiweka pesa yangu benki wanaajiri mlinzi ili ailinde ?.., wakati ukweli ni kwamba nikiweka pesa yangu wanamkopesha mtu mwingine na wanakula faida.., bila aibu bado wananikata tena pesa kama shukrani ya kuwawezesha wao kupata faida
 

Sawa. jibu swali basi la kuhus hiyo benki isiyo na makato makubwa.. mbona unakwepa swali la msingi
 

Hii BOT ilitakiwa iwe regulatory body kama Ewura au Sumatra...
 
Hivi nitanyaje haya maoni yafike kwa Prof. Ndulu, kila nikiona na kusikia tangazo kuhusu benki ya CRDB nahisi kukatwa. Je ndio kukwepa haya makato ndio sababu ya Waislam kupigia debe Islamic Banking?
 
Sawa. jibu swali basi la kuhus hiyo benki isiyo na makato makubwa.. mbona unakwepa swali la msingi

Zion Daughter,

Sijakwepa swali mamdogo mimi nina avoid kuonekana nafagilia benki fulani fulani ndio maana nataka na wewe ukafanye homework yako. Kabla hujafungua account kaa chini na umuulize afisa wa benki transaction charges kwenye kaunta sh ngapi? kwenye Atm sh ngapi? je nikitoa pesa kuna limits? Je akaunti hiyo inaingiza riba kwa akiba yako? Je makato ya mwezi yapo? je kuna gharama ya kutumia kadi ya ATM ?

My advice is try hizi benki mpya mpya na ndogo kama Equity,FBME, AZANIA, BOA, FNB,ABC,DTB,I&M,NIC wao focus yao ni kuongeza wateja.
 

Hicho chambo hata samaki huwa anaonyeshwa hiyo kitu huku nyuma kuna ndoano. Hii uliyoona kama ni kitu kizuri sana yaani International debt Master card ni kamba shingoni usije ukaitumia katika benki nyingine kwani watakata pesa yako mpaka ulie. Wanakata 6,000/= ukitoa pesa mara moja. Juzi kanda ya ziwa nilipoteza 18,000/ kwa kudraw 600,000/= we acha tu
 

Hii ya mastercard achana nayo ila gharama zingine ulizotaja hapo si sahihi
 
nimeweka pesa zangu bank "waaameekaataaaaaaaaaaaaaaaaaaaa"
ha ha ha! dogo weka hela ndani tu hakuna makato wala nini
 

Mkuu haya unayosema hata mimi nimeambiwa na rafiki yangu,tena ni mfanya kazi wa huko exim.
 
benki nzuri ni pamoja na kuwa na matawi mengi

Inategemea ni account ya aina gani.

Kwa mtu kama mimi wa Savings account ambayo ina card Visa, nikiwa popote Tanzania napata huduma.

Plus, my bank is just a call away nikiwa na tatizo nawafahamisha.
 
Mkuu Kimbori hawa jamaa wana matawi Kariakoo, Quality centre pale kwa Manji na Posta Opposite na Serena Hotel. Pia naskia wanafungua Mwanza, Arusha na Mbeya.
Kufungua akaunti mimi nilipeleka kitambulisho changu yaani Driving Licence pamoja na barua ya serikali ya mtaa, bhaas..hakuna cha wadhamini wala nini...halafu walinipa na internet banking bureeeeeeeeeeee
 
Naomba kujua kutoka kwa wenye experience Bank ipi hapa Tanzania wana makato kidogo kulinganisha na wengine, sina experience na mabank mengine apart from ninayotumia (CRDB) ambayo nayo nilifungua account lakini sikua nimefanya research kujua ipi afadhali.
 
Kwa mazingira ya Tz, kiukweli kwangu mimi njia nzuri ya kuhifadhi pesa ni kukata fixed deposit account ambayo ni "cancellable" kupitia banks kama TPB et al. Wale ambao wanaeza kua-access Saccos/Vicoba zilizo na similar arrangement nazo ni bomba pia. Tofauti na hapo mi naona ni bora ela nikae nayo tu mwenyewe.
 
Equity Bank
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…