Je ni athari zipi serikali ya CCM itazipata kwa kuendelea kumweka mbunge Lema mahabusu?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,834
Naomba tujadili Kama kuna namna yoyote ambayo CCM itapata kwa kuendelea kumshikilia mbunge wa CHADEMA kwenye gereza la Kisongo
 
athari iko kwa chaderma na wananchi waliomchagua watakosa mwakilishi bungeni
 
Lema si alitoka jana? Au karudishwa tena tujuzane. Athari zitakuwa za kisiasa zaidi kwani wanampromot lema na chadema kwa ujumla na watu wanamchukulia lema ni shujaa kama Nelson Mandela
 
athari ni kubwa kwa serikali na ccm kwa sababu wanajiongezea chuki kwa wananchi bure! leo mtoto wangu ameniambia baada ya kuona taarifa ya habari kuwa anaichukia thithiem kama anavyochukia shetani
 
Akikubali kutoka wafuasi wake wengi wataanza kuamini kwamba alikataa dhamana ili kupata umaarufu wa kisiasa ni heri aendelee kusota kwa muda zaidi asing'ang'anie kuachiwa kwa huruma ya CCM
 
uombe kubaki jela kisha usumbue wakati wa kutoka haina mantiki ni sawa na hakunaga
 
Naomba tujadili Kama kuna namna yoyote ambayo CCM itapata kwa kuendelea kumshikilia mbunge wa CHADEMA kwenye gereza la Kisongo

Athari moja wapo ni chama na serikali kuchokwa na watendaji wadogo wa idara ya polisi na usalama kwa ujumla, Kwa Mfano hadi leo alfajiri ktk purukushani za mabomu pale NMC kuna polisi wawili ambao hata kwa sura siwajui ila chakushangaza gafla baada ya mabomu kurindima FFU mmoja alitukuta tumejibanza (tulikua watatu) katika migomba na ukuta wa Arusha sport near arusha secondary.

Na alikua kashika mtutu ila wenzake walivyomuuliza kwa mbali kama kuna watuhumiwa eneo hilo yeye aliwajibu kuwa hakuna mtu na akatuambia tusipite njia ya msikiti wa baniani kwani kuna polisi wenzake wengi sana ivyo tuelekee na njia ya town, na tukiulizwa na askari wenzake tuwajibu kuwa tunaelekea sokoni na hatukua NMC.

Baaada ya hatua chache maeneo ya geti la shule ya msingi uhuru gafla mbele yetu akatokea FFU mwingine akiwa kavaa yale mavazi yao ya kazi na kashika mtutu akavua elemet yake akatuambia tukimbie kwa kupitia njia ya NSSF tuvuke mto then tutakuwa salama bila kutiwa nguvuni na askari wenzake.

Askari wote hawa wawili hatuwafahamu wala hawatufahamu na wala hatukuwaomba msaada huu walioutoa pia hawakutuomba rushwa na hatukuwapa rushwa.

Tulitimua kwa kupitia njia zile kama tulivyoelekezwa na polisi hao tusiowajua na tulifanikiwa kufika nyumbani salama na kupumzika kwa uchovu wa kukesha pale NMC.

Nashindwa kuelewa askari hawa waliopewa order kutukamata wakeshaji hapo NMC inakuwaje wanashiriki kututorosha tena ukizangatia askari hao wametoa msaada huo bila kuombwa wala kulaghaiwa na sisi wakeshaji.
 
Naomba tujadili Kama kuna namna yoyote ambayo CCM itapata kwa kuendelea kumshikilia mbunge wa CHADEMA kwenye gereza la Kisongo

Hakuna athari zozote yeye mwenyewe ndio alingangania kwenda Jela alikataa dhamana kwa hiyo lazima wasubiri mpaka tarehe 14 kwa mujibu wa sheria
 
Wale wanaofuatilia historia za siasa duniani anzia hapa karibu athari walizopata makaburu kwa kumfunga mzee mandela! Kumuua Steve biko! na wengine wengi , unachotengeneza ni kutengeneza wakina lema wengine wengi kwa sababu hulka ya binadamu alivyoumbwa ni kumtukuza anayethubutu kama lema Viongozi warudi kwenye vitabu wakasome wanachokifanya sio kipya duniani!!
 
Wote mnakwepa hoja hapa, Lema hakuwekwa ndani na polisi au mahakama kwani katika kesi aliyoshitakiwa nayo dhamana ilikuwa wazi isipokuwa Mh Lema alikataa kudhaminiwa ili kuonyesha kuchoka kwa vitendo vya polisi kumsumbua kila anapokuwa katika shughuli zake za kila siku.

OCD Zuberi alishasikika wazi akitamka lazima atamfunga sasa kuonyesha yeye yu tayari kufungwa ili mradi anatetea haki akaamua kujipeleka yeye mwenyewe magereza

Sasa watu waasiipotoshe fikra yake! Ni shujaa anaye simamia anachoamini.
 
Lema alitaka kutikisa kiberiti. sasa amegundua kuwa kimejaa.

Hivi Lema toka awe mbunge wa Arusha, amefanya kitu gani cha maendeleo kwa waliomchagua? Je ameweza kutengeneza japo mita kumi za bara bara ya lami katika jimbo lake lisilokuwa na hata barabara moja ya lami ya manispaa?
 
Lema alitaka kutikisa kiberiti. sasa amegundua kuwa kimejaa.

Hivi Lema toka awe mbunge wa Arusha, amefanya kitu gani cha maendeleo kwa waliomchagua? Je ameweza kutengeneza japo mita kumi za bara bara ya lami katika jimbo lake lisilokuwa na hata barabara moja ya lami ya manispaa?

masabur wewe. Je unajuwa kazi na wajibu wa mbunge jimboni. Kwani anatumia mshahara wake kujenga barabara au anatumia gvment funds zilizokuwa alocalleted?
 
Lema alitaka kutikisa kiberiti. sasa amegundua kuwa kimejaa.

Hivi Lema toka awe mbunge wa Arusha, amefanya kitu gani cha maendeleo kwa waliomchagua? Je ameweza kutengeneza japo mita kumi za bara bara ya lami katika jimbo lake lisilokuwa na hata barabara moja ya lami ya manispaa?

Sisi watu wa Arusha hatuhitaji maendeleo ya kuletwa na Mbunge. Maendeleo yetu tutajiletea wenyewe. Kikwazo kikubwa kinachotukabili wana wa Arusha katika kujiletea maendeleo yetu wenyewe bila kutegemea mbunge ni CCM na serikali yake. Huko pwani na Mtera mnakotegemea kuletewa maendeleo na mbunge endeleeni kusubiria hayo maendeleo. Maana nimekuja maeneo ya huko hamna cha maana cha kuonesha. Afadhali ya huku kwetu Arusha.

Lema tumempa kazi moja ya kupambana na CCM hadi kieleweke.
 
Nimegundua kwanini wachaga wabinafsi suala la sisi Arusha na kudharau Mtera haijengi ndugu yangu hata huku Mtera tuko chadema na tunasupport
 
hakuna athari yeyote.... serikali ipo makini na watu kama hawa wanaotaka kuchafua amani ....

lema amecheza karata zake vibaya
 
Back
Top Bottom