Je! Ni anguko la ccm? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je! Ni anguko la ccm?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by falesy, Apr 3, 2012.

 1. f

  falesy Senior Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 15, 2006
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TANZANIA NA CCM TUNAKOELEKEA (Kuna makosa ya kutofumbia macho)

  Niliwahi kusema (miongoni mwa post zangu kuhusu uchaguzi wa Arumeru Mashariki) katika mtandao wa jamii wa Face book (FB) kuwa "ARUMERU ndo start point ya COUNTDOWN ya vitu viwili ama;
  1. Ukombozi wa Nchi kwa njia ya BARROT; Ama
  2. Tungeanzia hapo kuhesabu siku za mwisho wa CCM hii ya sasa;
  Sasa kwa yale yaliyotokea huko (Lusinde issue na mengine); ni wazi tumeanzia pazuri maana kwa sehemu zingine za Tanzania watasema "kwani Arumeru wameweza wana nini; na sisi tushindwe tuna nini?"
  Pia watasema "tumejua sasa CCm si mahali salama maana wamekuja watatukana wazee wetu (Maana Slaa kwa kule si tu mwanasiasa bali ni mtu wa heshima kwao kama wengine kina Lowassa) Kwa hiyo; kuanzia sasa; CCM wakiwa na mkutano wakileta mjumbe wa NEC wategemee kutokuona mtu mkutanoni maana watu hawako tayari kuona wanatukanwa Pia CCM wakimpeleka Mkapa popote; wasitegemee kuona mtu maana wanaogopa kutangaziwa kuwa wao si wa ukoo walioko
  Kwa sasa nguvu pekee ya CCM iliyobaki (naomba nistaje) pekee ambaye wakimtumia bila hila watafika mbali. Pia hakukuwa na ubaya wowote kuendelea kumtumia Mzee Malecela kwani ni Mjumbe wa kudumu CC na NEC
  Lakini; Am sorry to say: CCM, it is too late; and in the end only the true Legends of the party wll remain in others (most of them) will go to their new parties (CCK---CCJ); join other weak parties now like AFP and form their new parties kama hiki cha juzi from CUF (is another CCm follower)
  Wito kwa mwenyekiti wangu; Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete;
  i. Ni wakati wa kuwajibisha wahujumu ndani ya Chama; maana kwa jinsi ambavyo mambo yameendeshwa Arumeru na kwingine(kama Kirumba Mwanza); ni wazi wajumbe wa Chama hawakuwa kwa ajili ya kutafuta ushindi wa Chama bali ama kukoroga mapishi ya kubomoa chama, ama kujijenga wao wenyewe kwa siasa zao
  ii. Kamati kuu ya NEC ya CCM lazima itoe maamuzi na tamko dhidi ya kauli za viongozi wa Chama wawili ambao wamesababisha upotevu wa kura; ya kwanza ni ile ya Mwenyekiti wa Chama Mstaafu juu ya ukoo wa Nyerere, jambo ambalo halikuwa na tija kwa kampeni za Arumeru na la pili ni ile hotuba ya Livingstone Lusinde ambayo imetuchafua na itaendelea kutuchafua kila tunakopita
  iii. Ushiriki wa kampeni wa Mh. Lowassa na Mh. Sitta Arumeru na Kirumba (kwa mfuatano huo) haukuwa kwa ajili ya kampeni za waliyoendea bali walifanya kampeni zao binafsi (wanatakiwa watoe maelezo kwa nini walifanya hivyo)
  iv. Je! mh. mwenyekiti; kwa nafasi yako kama rais wa jamhuri una kisasi kuwa huwezi kushirikiana na wabunge wa upinzani? Ninavyokuelewa la hasha; ila kwa kampeni za Arumeru imeonekana kuwa utakuwa tayari pamoja na mawaziri (hasa wa ardhi) kusuluhisha matatizo ya wana Arumeru iwapo tu wangemchagua Siyoi; je huo ndiyo msimamo wako?
  v. Kwa hali ilivyo sasa; na hasa kuzingatia kuwa wananchi wa Tanzania hatuna tena imani na CCM; CC ya NEC ya CCM ifikie uamuzi kuwa; ikitokea kuna uchaguzi mdogo umetokea hapa katikati kabla ya 2015, basi CCM isisimamishe mgombea ili kuwasahaulisha watanzania (angalau kwa kipindi) yaliyotokea Arumeru, ama kama itashiriki basi viongozi wa kitaifa waende tu wale wa sekretariet na si wengine kama hawa kina Lusinde, Pia kwa wakti huu kwa vile wapiga kura wengi ni vijana basi tuwaamini vijana kama (mimi Falesy Mohamed kibassa), January Makamba, mwigulu Nchemba; Hussein Bashe maana ndo wenye mvuto (usiniulize mimi mvuto nimeutoa wapi, wewe nipe kazi)
  v. CCM tumekuwa na kampeni saidizi kwa CHADEMA na kwa muda mrefu hakuna aliyelisemea isipokuwa kwenye miongoni mwa vikao Mh. Lowassa aliligusia kwa kusema "Kampeni dhidi ya UFISADI ilikuwa ni ya CHADEMA hivyo kuibeba kama ya ccm ni hatari (maneno nimehaulisha); na NEC haijatoa msimamo juu ya hii kampeni; hivi hatujui kuwa kutaja hilo neno tu UFISADI lina link na CHADEMA? Au tumeisahau Operesheni SANGARA ambayo mzee wangu Makamba aliwahi kuibeza na kuiita Operesheni Dagaa? Au tumesahau kuwa CDM walishafanya hii kampeni hadi ikaingia vichwani mwa watanzania na wakaelewa? Au tumesahau kuwa hii ina hatimilki ya CDM? Au hatujui kuwa wao wakiisema kwa maneno mepesi wanaeleweka kuliko sisi? Ninakuomba mwongozo mwenyekiti!
  Mwisho; natoa mwito kuwa CCM ijiimarishe kwa kuchukua wataalamu wa kweli na kuwaweka hadharani badala ya kufanya nao kazi kwa siri ili wasaidie chama katika mipango mikakati na watakaofanya tafiti yakinifu kuelekea maeneo ya mapambano (Angalia CDM wana maprofessor makini kama Prof Safari, Prof Baregu na vijana wasomi makini). Kwa nini CCM tumefanya siri wakati siri za chama zinavuja kila siku? Ninalipenda wazo lako la kutumia vijana wasomi lakini kujitegemeza sana na walioko vyuoni si wakati wake maana hawana "mentors" wa uhakika!!! napenda tuwe na maprofessor ambao tutawatumia kwa ajili ya Coaching na Mentoring ya vijana kutoka vyuoni si kiitikadi tu bali kitafiti kitaifa na Chama ili wanapokuwa na ukada wa Chama wanjua Taifa ndo namba moja!

  I remain Royal to my party CCM and my Nation TANZANIA
   

  Attached Files:

 2. M

  Malova JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hisiahazipo tena kaka. Kuna realities and facts. Salamu zenyu sana.
   
 3. kapistrano

  kapistrano JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,205
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ok mkuu
   
 4. M

  Mhamashiru Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mawazo yako ni tofauti sana na wale waliopewa dhamana kwenye chama.,chama hicho sasa hakina mwenyewe,kila mtu kivyake
   
 5. k

  kubenafrank Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana kwani magamba hawana nafasi tena katika tz
   
 6. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Marehemu ccm rest in peace!
   
 7. Van persie

  Van persie JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 916
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 60
  KWeli chama kimeshaenda na maji.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wewe CCM au Mamluki?naona kama unapiga majungu vile , ya Arumeru yamepita acha wananchi wa Arumeru wenyewe waendeshe jimbo lao siyo muda wa propaganda tena.N lini Rais alisema atashrikiana na Wana-Arumeru endapo SIOI angeshinda kama si majungu hayo.
   
 9. h

  hans79 JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Mambo mengi yataonekana 2012
   
 10. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 180
  Rip ccm
   
 11. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,087
  Likes Received: 10,443
  Trophy Points: 280
  Masikini ccm mnakazi ya ziada...
  R.I.P ccm.
   
Loading...