Je Ndoa Uhalalishwa kwa Tendo?

Je Ndoa Uhalalishwa kwa Tendo?

Masulupwete

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
2,366
Reaction score
2,438
Mke asipotoa (tendo), tayari kunakuwa na hisia, anatoka nje ya ndoa. Vivyo hivo kwa mume asipotoa.

Je huu ndio muhimili pekee wa kudumisha ndoa?

Je pasipo tendo hamna ndoa?
 
Ndoa ina mambo mengi na ni kuishi pamoja kwa shida na raha, kwa upendo na uvumilivu. Tendo la ndoa (sex) ni hitaji la mwanadamu na tunaoana ili kukidhi hitaji hilo pia mbali na mengine mengi

Tendo ni muhimu sana kwa kuwa ni hitaji la binadamu ina maana kulikosa katika ndoa yako utaenda kulitafuta kwingine kwa kuwa mwili unahitaji

Kama mwenzako akiwa na tatizo kama ugonjwa au chochote kinachopelekea kutowezafanya tendo basi hapo mwingine avumilie kwa kuwa mlikubaliana shida na raha. Hata hivyo tendo la ndoa, upendo, uvumilivu na vingine ni nguzo kuu katika ndoa
 
Mke asipotoa (tendo), tayari kunakuwa na hisia, anatoka nje ya ndoa. Vivyo hivo kwa mume asipotoa.

Je huu ndio muhimili pekee wa kudumisha ndoa?

Je pasipo tendo hamna ndoa?
Tendo la ndoa ni mojawapo ya vitu vinavyohitajika kwa ndoa kuwa halali. Kuna vitu vinne ambavyo lazima viwepo ili ndoa iwe halali.
Kwanza, waoanaji wawe mwanaume na mwanamke. Baadhi ya nchi siku hizi zimehalalisha kuoana kwa watu wa jinsia moja. Nyingi zinabakia na sheria hiyo.

Pili, lazima ndoa ifungishwe na mtu anayetambulika kisheria kuwa na madaraka ya kufungisha ndoa. Mtu huyo anaweza kuwa kiongozi wa dini; au afisa wa serikali au mahakama; na tatu kiongozi wa kijadi anayetambulika hivyo kisheria. Bila kushuhudiwa na mtu mwenye madaraka hayo, hata kama mwanamme na mwanamke watakaa miaka kumi wakazaa na watoto bado hawatatambulika kuwa wanandoa. Kwa sheria za Tanzania, watu kama hao, pamoja na kwamba hawatambuliki kama wanandoa, sheria inawapa mafao fulani kama vile urithi wa mali ikiwa mmoja wapo atakufa. Lakini bado hawatambuliki kama wanandoa.

Tatu, ni budi ndoa ikamilishwe kwa tendo la ndoa baada ya kufungishwa na mtu mwenye madaraka hayo. Hiyo inaitwa consummation of the marriage. Imewahi kutokea usiku baada ya sherehe za arusi bwana arusi alikatalia tendo la ndoa kwa madai kwamba amechoka na shughuli za sherehe. Siku ya pili akawa anaumwa kichwa na sababu zikaendelea hivyo hivyo mwezi ukakatika.

Baadaye ikajulikana kwamba hawezi kufanya tendo la ndoa wala hasimamishi. Ndoa hiyo ilitenguliwa kwa kitu kinachoitwa annulment; yaani matamshi (by a competent authority) kwamba ndoa iliyofungwa ilikuwa batili. It is as good as not having been there although they had been declared as husband and wife. Watu kama hao hutenganishwa kwa annulment ambayo siyo sawa na talaka. Kupeana talaka ni lazima kwanza muwe mulioana. Kwa kuwa hawa, in the first place, walikuwa hawajaoana basi talaka haiwezi kuwepo.

Nne, wanandoa lazima wasiwe ndugu wa damu; kama mtu na dada yake; au mtu na mtoto wake wa kuzaa. Kwa mfano anaweza kutokea mtoto alitupwa na mama yake baada tu ya kuzaliwa akaokotwa na kwenda kukulia mbali. Baadaye anakuja kukutana na ndugu yake bila kufahamiana kwamba wao ni ndugu wakaoana. Hiyo inaitwa incestuous marriage na ni batili.

Hata kama mpaka wamezaa watoto mara ikithibitika kwamba hawa ni ndugu, ndoa hiyo hutenguliwa kwa annulment na siyo talaka.
Kwa kumalizia, tendo la ndoa ni lazima liwepo ili kukamilisha ndoa. La sivyo, kutakuwepo na annulment, ambayo ndiyo njia pekee ya kufuta ndoa katika Kanisa Katoliki ambalo halina talaka.
 
upendo ndo chanzo cha ndoa... bt sex ni muhimili wa ndoa au mahusiano kwa walio mwili mmoja.... hvo sex ina umuhm wapekee xana ktk ndoa
 
Back
Top Bottom